GE2025 Sigrada Mligo amtuhumu mgombea CCM Njombe Mjini kuanza Kampeni Mapema kabla ya uteuzi

GE2025 Sigrada Mligo amtuhumu mgombea CCM Njombe Mjini kuanza Kampeni Mapema kabla ya uteuzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Mgombea Ubunge kwa Jimbo la Njombe Mjini kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Sigrada Mligo amelalamikia uvunjwaji wa kanuni za kiuchaguzi kutokana na Mgombea Ubunge wa Chama Chama Mapinduzi (CCM) kwa Jimbo hilo Deo Mwanyika kuanza kufanya kampeni akiwa bado hajateuliwa bado na Tume Huru ya Uchaguzi (INEC).

Akizungumza na Manara Tv leo Agosti 27, 2025 Sigrada amesema ameshangazwa na kitendo kilichofanywa na Mwanyika cha kuanza kubandika mabango ya kampeni usiku wa kuamkia leo pamoja na asubuhi ikiwa Tume bado haijafanya uteuzi.

"Maelekezo tuliyokuwa tumepewa na msimamizi wa Uchaguzi ni kwamba huruhusiwi kufanya kampeni kabla ya uteuzi lakini cha ajabu zaidi mtia nia mwenzangu toka jana usiku naona yametandazwa mabango mji mzima" amesema Sigrada

 
Back
Top Bottom