Sigmud Freud na Cocaine

torvic

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
3,806
9,300
cocaine ni moja wapo ya mimea ya zamani sana, miaka elfu 3 kabla ya kuzaliwa kwa Yesu inasemeka cocaine ilikuwepo.
ebu tanzie hapa kwanza,,, 'Incas' hii ni jamii flani ya watu ambao walikuwa wanapatikana colombia america lakini kwa sasa ni meru. hii jamii ilikuwa na taboo yao kwenda milima ya andes, uko milimani walikuwa wakitafuna coca leaves ili kukaribiana na hali ya hewa ya uko sababu majani hayo ya coca yalikuwa yakiongeza mapigo ya moyo na kasi ya kupumua....


sitaki kuwazungumzia hawa incas ila nilitaka kuonyesha kidogo chimbuko la cocaine na matumizi yake kwa karne hizo.


sasa tukija kwenye karne zetu hizi miaka ya 1859 hadi 1880 kuna huyu german chemist, Albert Niemann yeye alianza kuitumia cocaine kwenye taasisi za afya kama dawa ya matibabu


lakini pia kwenye kipind iko iko kulikutoa na mtu flani, binafsi naona kama ndio aliharibu mtazamo wote wa hii kitu "cocaine" mpaka sasa naona athari za huyu mtu
jina anaitwa Sigmud Freud, huyu ni austrian alikuwa psychoanalyst na neurologist pia vilevile ni muanzilishi wa psychoanalysis kama njia ya kufanya maojiano baina ya mgojwa na psychoanalyst.
huyu kiumbe alitoa mchango hasi mkubwa sana kupotosha jamii kuhusu matumizi ya cocaine ikiwa yeye binafsi alikuwa ni mtumiaji wa cocaine mara kwa mara , na kwa kuanza aliipigia debe na kuikuza cocaine kwa madai yake kwamba cocaine ni tonic ya kutibu msongo wa mawazo na inasaidia kwenye tendo la ndoa(tendo la ndoa!!!!!! mjamaa nahisi alikuwa JJ mwaka kwa karne hizo....joke)


kwenye miaka ya 1884 Sigmud alichapisha makala kwa jina la "uber coke" (about coke) makala hayo yaliikuza na kuisifia cocaine na kuipachika jina la "magical substance" (kitu cha maajabu)

Sigmud kutokana na matumizi yake binafsi ya cocaine alifanikiwa kumshauri mpenzi wake na marafiki zake wa karibu kutumia cocaine na vilevile alishauri kwamba cocaine itumike kwa matumizi ya kila siku

kwajuhudi hizo za Sigmud na mashauri yake kuhusu matunizi ya coke mwisho zilileta matokeo hasi kwa rafiki yake wakaribu ambaye alipagawa na kupata wazimu akilalamika kuwa kuna nyoka wanatembea kwenye mwili wake.

mwisho kabisa bwana Sigmud Freud aliipotosha jamii kwa imani yake,,,
kwamba cocaine haina madhara yoyote ata ikitumiwa kwa dose kubwa (overdose) na kwa imani yake iyo alifanikiwa kuleta matokeo (-100) na hili ni baada ya wagonjwa wake kufariki kwa kuandikiwa dose kubwa ya cocaine.


~~~~
 
Sigmind Freud alitoa mchango mkubwa sana katika kuelezea HUMAN GROWTH AND DEVELOPMENT pia alikuwa mtu wa kwanza kuelezea hulka za mwanadamu ID, EGO na SUPER EGO.
Mawazo yake hadi leo yanafundishwa vyuo mbali mbali katika kada za afya.
HAKUWA KILAZA KAMA UNAVYO MFIKIRIA,

Kupitia yeye ABRAHAM -MASLOW alipata kuibikia kwa mgongo wa Sigmud freud
 
Sigmind Freud alitoa mchango mkubwa sana katika kuelezea HUMAN GROWTH AND DEVELOPMENT pia alikuwa mtu wa kwanza kuelezea hulka za mwanadamu ID, EGO na SUPER EGO.
Mawazo yake hadi leo yanafundishwa vyuo mbali mbali katika kada za afya.
HAKUWA KILAZA KAMA UNAVYO MFIKIRIA,

Kupitia yeye ABRAHAM -MASLOW alipata kuibikia kwa mgongo wa Sigmud freud
ni kweli akabisa mkuu sigmud anamchango mkubwa kama ulivyo zungumza lakin kwa upande mwingine wa shilingi habari yake ndio hiyo.....
aliitukuza cocaine kwa kasi anyoijua yeye na bila shaka yoyote alikuwa teja!
 
kifo cha father of psychology (Sigmund Freud) kilisababishwa na matumizi yaliyozidi ya mihadarati

kwa kifupi na yeye alikua ana matatizo ya kisaikolojia
 
Once u AR teja,,,u will always b moko,,
Hata kama we ni genius.
 
Segmund Freud alikuwa Ni hodari Sana ktk nyanya za akili na ukuaji wa binadamu na afya kwa ujumla mf. Ali take part kubwa ktk medical psychology humu Dr na psychologist wanakaa meza moja
 
Back
Top Bottom