Sifa ya Uandishi

Sifa ya Uandishi

Bueno

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2022
Posts
34,610
Reaction score
59,577
[Chorus]
Sifa ya Uandishi
Tunga bila Sifa
Nikifa
na Sifa nzuri
Ni Sifa kwa alionisifu

Mistari 16
Uvumi unasikika
Lini mistari ya Mhuni itakwisha?

Tungo zaidi ya Sifa
Mdundo wa Kibabe
Mikunjo ya Kimista
Gumzo za Kipambe

Nachana
Kisha naepuka lana
Kichwani ni mtindo wa Rap
Nimeusuka toka zama

[Verse: IDENTITY]
Tungo zaidi ya Sifa
(Halafu)
Mdundo wa Kibabe
Mikunjo ya Kimista
(Kwa hio)
Gumzo za Kipambe

Mzunguko kila dakika
Kama nina Tumbo kwenye Gambe
Chonde na Utumbo
Bingwa utageuzwa Mfugo
Wakung'ate

(Eeeh)

Fundi wa Makeke
(Eeeeh)
Mtungi nipe Cheche
Kama Mbishi na una-perform
Huu ndio Ukumbi wa Kasheshe
(Paaaah)

Sina Mfuko wa Chupi
Kama Buzi la Vicheche
Wanakuita Kiwembe
Nakupa News Mi Machete

Wese la Kampuni
(Kwa hio)
Misele ya Kiafisa
(Hahaha)
Kwenye Pesa nipo On time
Kama Kengele ya Kanisa
(Duiuuh)

Nachemsha Bongo
Kama nina Cooker kwenye Kichwa
Mbabe utapunguza Mwendo
Hili ndio tuta la Mabingwa
(Achaa)

Baharia Mvuvi wa Noti
Na kila nikipewa Shavu
Naacha Utunzi wa Makofi
(Yeeeah)

Sifichi Njaa
Kama Suti ya Kiongozi
Naacha Pesa Iongee
Kwa hio Sizungumzi
Kama Kinyozi
(Ayaa)
 
Kukitafuta Kigawe Kidogo cha Shirika
Sasa hapo itategemea hicho kigawe kipo shirika lipi, kwa mfano kigawe cha shirika la umeme kipo pale Ubungo, kama ni kigawe cha shirika la utangazaji kipo pale Bamaga - Kijitonyama karibu na chuo cha ustawi wa jamii 😎
 
Sasa hapo itategemea hicho kigawe kipo shirika lipi, kwa mfano kigawe cha shirika la umeme kipo pale Ubungo, kama ni kigawe cha shirika la utangazaji kipo pale Bamaga - Kijitonyama karibu na chuo cha ustawi wa jamii 😎
Na Kigawo Kikubwa cha Shirika kipo wapi?
 
Vigawe vikubwa vyote vinakaa kwenye wizara husika na sio kwenye mashirika na makatibu ndio watendaji wakuu hadi kufika huko kwenye mashirika
Kwa hio hapo unataka kusemaje? Kikokotoo kiingizwe Bungeni wabunge wakwanguliwe posho mpaka seating allowance?
 
Back
Top Bottom