Sifa ya mwanamke kutokujua kila kitu

Sifa ya mwanamke kutokujua kila kitu

Tundusami

Senior Member
Joined
Feb 7, 2026
Posts
116
Reaction score
262
Demu atakiwi kujua kila kitu . Sio demu anamjua mpaka komando kipensi.

Inatakiwa ukimuuliza “baby unamjua Lukaku?” akujibu “ni yule rafiki yako wa kijijini?”
Ukimuuliza “baby, Haaland unamjua?” akujibu “si ndo yule mtoto wa mama James?”

Sio demu anajua timu za mpira Bongo mpaka Ulaya, anamjua hadi Gabriel Jesus mshambuliaji wa Arsenal. Dem anamjua mpaka Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio. Dem anajua vita vinavyoendelea duniani Urusi na Ukraine, Iran na Israel, Israel na Palestina.

Demu ukiangalia nae The Walking Dead au Wrong Turn hata hashtuki. Amekodoa macho tu mwanzo mwisho.

Inatakiwa akiangalia movie za kutisha anakukumbatia akisema “baby toa bando, mi nitaota” au “maskini, si atamuua sasa.” Huyu zombie.

Sio demu anaangalia picha la mavampire anashabikia “bora life, lina kiherehere sana.”

Mimi napenda demu nikimwambia “leo Chelsea anacheza na Man U,” yeye aniambie “kumbe Kombe la Dunia limeanza?”

Sio demu anakutajia mpaka first eleven ya Burnley. Demu gani huyo?
 
Hakuna mtu duniani anayejua kila kitu ,kuna vitu utajua kwenye angle yako na vingine utavijua kijuujuu tu na si deep.
 
Wewe una tatizo lako binafsi..
Ki mfumo dume.. Kizaidi

Wale akina sie hakika wa aina yako hamtufai pia
 
Au unamwambia nitajie timu tatu za ulaya anaanza na saint atienne
 
Aisee nimetoka kwenye hizo mamboo ila nitarudi soon huwezi kuwa mbumbu kisa mwanaume wa hovyooo .

Mke au dem kujua vitu ni raha ndio maana mnaliwa sana siku hizi nasio pesa kidogo kwa maana nyie hamtaki watu wajuaji
 
Back
Top Bottom