Sifa kuu za polisi wa Tanzania

Sifa kuu za polisi wa Tanzania

GHULA

Member
Joined
Mar 3, 2013
Posts
77
Reaction score
66
SIFA ZA JESHI LA POLISI TANZANIA.

Yawezekana tunalalamikia sana jeshi la polisi, na halijaweza kubadilika. Leo nimeona niweke humu sifa za jeshi la polisi nchini, ili wakisoma kasoro zao pengine watajirekebisha. Nitaambatanisha na mifano michache, ila wenye nayo mingine wanaweza kuongeza ili tuliboreshe jeshi kwa manufaa ya nchi yetu.

1. Jeshi la polisi ni la Kijambazi, Askari wengi wamehusishwa na matukio ya ujambazi, kuvamia, kuiwaibia wananchi mali zao. Turejee mifano ya Ngorongoro, au hata tukio la hivi karibuni pale Kariakoo walipoamua kujigeuza kuwa majambazi kwa kuchukua pesa za mtu waliyeenda kumsaidia (150,000,000/-), au tukio la kumpiga risasi mfanyabiashara wa Geita na kuiba pesa na madini yanayokadiriwa kuwa na thamani ya milioni 300.

2. Jeshi la Polisi wa Tanzania ni la vitisho,halifuati sheria bila kushurutishwa, japo linahubiri vile, linasisitiza polisijamii lakini halitekelezi kwa matendo. Na kwa kuwa ni la vitisho ni la kigeugeu,hugeuka geuka kwenye maamuzi……..mifano linavyotishia waandishi wa habari, nawanaharakati kwa kisingizio cha kuandika uchochezi, kuwakamata au kuwajengea hofu.

3. Jeshi la polisi Tanzania ni WAONGO SANA,Hudanganya sana watanzania na kuwaona watanzania ni wajinga sana, Mfano liliunda Kamati ya Sakata la Ulimboka halijatoa majibu, mpaka ikafikia hatuawanaikana tume waliyoiunda ikawa haipo, jana wameunda tume ya kufuatilia sakata la Kibanda, aliyetangaza ni Kova mwenyewe aliyeitangaza ya Ulimboka baadayeakaikana.Kova amesema kuwa Kibanda ndiye anafaa kuwa shahidi wa kwanza katika tukio hilo, je mbona Ulimboka hajawahikuwa shahidi wa kwanza kwa kesi yake?

4. Limeunda tume nyingi sana za mauaji namateso ya watu halijawahi kuleta majibu, mfano la Ulimboka na Mwangosi IGP alisema ni siri ya Taifa.

5. Hawataki kuwajibishana, wanalindana,wanaogopana. Mfano halikumchukulia hatua zozote Michael Kamuhanda pamoja nakutuhumiwa kusimamia mauaji ya Mwandishi Daudi Mwangosi.

6. Jeshi la polisi hubambikizia raia kesi iliwapewe pesa, na wanapotajwa katikaukweli hukaa kimya hawachukuliani hatua. Walitajwa maafisa waandamizi wa polisikutaka kumbambikia kesi ya madawa ya mtoto wa Reginald Mengi, tukaambiwa napesa ambazo walipewa hadi sasa kimya………hili limeisha wapi?

7. Hupokea rushwa na kuwaachia watuhumiwa,kisha hujitokeza kwa waandishi au mbele ya raia kudanganya kuwa watuhumiwawamekimbilia kusikojulikana.

8. Katika vitisho na uongo, tujiulize mkwarawa meseji 400 za matusi kwa Spika uliishia wapi?, Mkwara wa kesi ya Mkenya aliyemtesa Ulimboka, ukimwangalia tu na kulinganisha aliyofanyiwa Ulimboka, eti kumteka, kumwendesha kwenye gari, kutesa Mabwepade, kumngoa kucha, kumng’oameno, eti Mkenya alikuwa peke yake hadi sasa jeshi halijamkamata Ighondu anayetajwa na Ulimboka

9. Barabarani wanaongoza kwa kupokea rushwa naukipeleleka malalamiko kwa wakubwa hakuna hatua

10.Wanafuatilia kesi zilizokosewa kidogo kuwabana wakosaji, zilizo wazi na zenye mambo makubwa yenye maslahi kwa nchihufanywa kuwa ni ‘siri kubwa
 
Ni vizuri wakachukua maoni yako kama changamoto na si kukuingiza kwenye black list yao ...
 
Mimi siwategemei Polisi kwa lolote hata ikitokea majambazi wamewashinda walinzi wangu sitopiga simu polisi, na nimeapa sitawapa ushirikiano polisi kwa lolote lile
 
Polisi mikoani na wilayani ni miungu watu.kuna huyu mkuu wa usalama barabarani RTO wa arusha ni mbabe anatukana watu amekuwa anachagua watu wa kusaidia akiwaona hawa matajiri wa mabasi hata wamekukuta anawaambia ingia anateta nao akimaliza mbele hao matajiri anaanza kuwafokea watu mlioko hapo mnataka nini toka hapa,yaani amekuwa tabu sana hapa arusha.
 
Yote uliyosema ni kweli. Ushahidi wa wizi ninao kabisa. Pia polisi wote wana tabia moja. Tabia ya kutetea uovu unaofanywa na wenzao upo kwa wote. Muone kova au mwema anavyotetea polisi wauaji, vitu vyenye ncha kali
 
[/S)]SIFA ZA JESHI LA POLISI TANZANIA.
Yawezekana tunalalamikia sana jeshi la polisi, na halijaweza kubadilika. Leo nimeona niweke humu sifa za jeshi la polisi nchini, ili wakisoma kasoro zao pengine watajirekebisha. Nitaambatanisha na mifano michache, ila wenye nayo mingine wanaweza kuongeza ili tuliboreshe jeshi kwa manufaa ya nchi yetu.
1.
Jeshi la polisi ni la Kijambazi, Askari wengi wamehusishwa na matukio ya ujambazi, kuvamia, kuiwaibia wananchi mali zao. Turejee mifano ya Ngorongoro, au hata tukio la hivi karibuni pale Kariakoo walipoamua kujigeuza kuwa majambazi kwa kuchukua pesa za mtu waliyeenda kumsaidia (150,000,000/-), au tukio la kumpiga risasi mfanyabiashara wa Geita na kuiba pesa na madini yanayokadiriwa kuwa na thamani ya milioni 300.

2. Jeshi la Polisi wa Tanzania ni la vitisho,halifuati sheria bila kushurutishwa, japo linahubiri vile, linasisitiza polisijamii lakini halitekelezi kwa matendo. Na kwa kuwa ni la vitisho ni la kigeugeu,hugeuka geuka kwenye maamuzi……..mifano linavyotishia waandishi wa habari, nawanaharakati kwa kisingizio cha kuandika uchochezi, kuwakamata au kuwajengeahofu.
3. Jeshi la polisi Tanzania ni WAONGO SANA,Hudanganya sana watanzania na kuwaona watanzania ni wajinga sana, Mfanoliliunda Kamati ya Sakata la Ulimboka halijatoa majibu, mpaka ikafikia hatuawanaikana tume waliyoiunda ikawa haipo, jana wameunda tume ya kufuatilia sakatala Kibanda, aliyetangaza ni Kova mwenyewe aliyeitangaza ya Ulimboka baadayeakaikana.Kova amesema kuwa Kibanda ndiye anafaa kuwa shahidi wa kwanza katika tukio hilo, je mbona Ulimboka hajawahikuwa shahidi wa kwanza kwa kesi yake?
4. Limeunda tume nyingi sana za mauaji namateso ya watu halijawahi kuleta majibu, mfano la Ulimboka na Mwangosi IGPalisema ni siri ya Taifa
5. Hawataki kuwajibishana, wanalindana,wanaogopana. Mfano halikumchukulia hatua zozote Michael Kamuhanda pamoja nakutuhumiwa kusimamia mauaji ya Mwandishi Daudi Mwangosi
6. Jeshi la polisi hubambikizia raia kesi iliwapewe pesa, na wanapotajwa katikaukweli hukaa kimya hawachukuliani hatua. Walitajwa maafisa waandamizi wa polisikutaka kumbambikia kesi ya madawa ya mtoto wa Reginald Mengi, tukaambiwa napesa ambazo walipewa hadi sasa kimya………hili limeisha wapi?
7. Hupokea rushwa na kuwaachia watuhumiwa,kisha hujitokeza kwa waandishi au mbele ya raia kudanganya kuwa watuhumiwawamekimbilia kusikojulikana.
8. Katika vitisho na uongo, tujiulize mkwarawa meseji 400 za matusi kwa Spika uliishia wapi?, Mkwara wa kesi ya Mkenyaaliyemtesa Ulimboka, ukimwangalia tu na kulinganisha aliyofanyiwa Ulimboka, etikumteka, kumwendesha kwenye gari, kutesa Mabwepade, kumngoa kucha, kumng'oameno, eti Mkenya alikuwa peke yake hadi sasa jeshi halijamkamata Ighonduanayetajwa na Ulimboka
9. Barabarani wanaongoza kwa kupokea rushwa naukipeleleka malalamiko kwa wakubwa hakuna hatua
10. Wanafuatilia kesi zilizokosewa kidogokuwabana wakosaji, zilizo wazi na zenye mambo makubwa yenye maslahi kwa nchihufanywa kuwa ni ‘siri kubwa'


mkuu nadhani huna uelewa na muundo wa jeshi la Polisi na majukumu yake, jeshi la polisi si la kijambazi limesaidia watu wengi sana mi mwenyewe ni mmoja kati waliosadiwa na jeshi hilo, nimesha wahi kuibiwa vitu vyangu na nikaenda kituo kuripoti na nikashughulikiwa vizuri sana, awali sikujua kama wangeweza kunisaidia kupata vitu vyangu kwa kuwa nilikuwa na mawazo hasi kwa askari lakini walinisaidia mpaka leo ninawashukuru sana, sikatai katika taasisi yenye watu wengi si kila mtu atakuwa mzuri lakini si busara kujeneralize taasisi nzima wakati taasisi hiyohiyo inawasaidia watu wengi.
 
Mbna hamjadili walimu waliofelisha wanafunzi laki mbila na nusu....,kila siku polisi polisi achen majungu na fikra hasi sasa kama unakosa polisi wakuachie,...Nyambafu
 
Mimi siwategemei Polisi kwa lolote hata ikitokea majambazi wamewashinda walinzi wangu sitopiga simu polisi, na nimeapa sitawapa ushirikiano polisi kwa lolote lile

ndugu hawa wat wana visa angalia waskufanyie mauzauza
 
na pia wanapenda kubambikia wat kesi huku wakiwafahamu wahusika halisi
 
mleta mada upo sahihi tatizo umejumuisha wapo polisi wengi watiifu na wachapakazi na kuna wachache washenzi, wazembe, wezi nakadhalika ambao sifa zao mbaya imeathiri mfumo wa upatikanaji haki na nafasi ya polisi kama chombo cha kulinda raia na mali zao
 
Yote uliyosema ni kweli. Ushahidi wa wizi ninao kabisa. Pia polisi wote wana tabia moja. Tabia ya kutetea uovu unaofanywa na wenzao upo kwa wote. Muone kova au mwema anavyotetea polisi wauaji, vitu vyenye ncha kali

Si kweli kaka hawa jamaa mambo yakutetea hayapo huwa wanawachukulia hatua za kisheria hadi kuwafikisha mahakama na hatimaye kufukunzwa kazi . hawa wazee wanapenda maadili na nidhamu ukienda kinyume hawakuachi lazima wakupeperushe
 
wataje japo wa nne.mm police wote kwangu ni wezi na mjambazi
 
Watanzania tumekua waoga ndio maana tunayafumbia macho na kuogopa si kusema bali hata tunaposikia ukweli!!!! Aliyetoa thread anazungumza uhalisia ila wachangiaji wengi wanaonekana kuwa waoga kwamba atafanywa vibaya!. Kwan hii nchi kuna mtu alizaliwa akiwa ameibeba ndio tumwogope? Sisemi kwamba polisi wote sio wema bali hata mm namuunga mkono kwamba polisi WENGI wamesahau maadili ya kazi yao na kuingia kwenye siasa jambo ambalo litaipeleka pabaya nchi yetu na kugeuza wale tuliokua tukiwategemea kama walinzi wetu kuwa adui na wezi wetu!!! Tanzania jeshi la polisi na wananchi turudi katika umoja, tueshimu utu na tujenge tanzania yetu!!! Inawezekana tukichukua hatua!!!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Polisi ni majambazi kama majambazi wengine sema wao wana leseni na uzoefu.
 
Polisi ni wavuta bhang na wanywa gongo rejea tukio la mwangosi na yule mwalimu wa makete.
 
Yaap!! mtwara nimeshuhudia mwenyewe polisi wakimpora mama muuza samaki pesa yake pamoja na mama yule kutembeza sinia la samaki kichwani bila huruma walimpora pesa askari,pia wakati wanalipua mabomu ya machozi wamekuwa wakingia madukani kuiba baada ya wenyewe kukimbia, kwa hiyo vurugu huwapa mianya ya kufanya utapeli, mtwara ni mfano tosha,rafiki yangu mmoja eneo la chuo kikuu cha st.augutine mtwara akiwa dukani kwake wakati wa vurugu polisi wakaenda dukani wakampora simu na shilingi elfu 20 alizokuwa nazo mezani,wengine waliporwa hadi laki mbili mitaani,ndo maaana kwa hasira raia waliamua kuchoma moto hovyo, sababu kuu hawana sehemu ya kusemea,kuna mengi sana kuhusu ujambazi wa polisi, hata ya akina zombe tunaweza kukumbushia.
 
Back
Top Bottom