Ni kweli kabisa lakini ni vema mkafikiria kwa kina,Mambo ya kusoma kipande cha gazeti na kutoa hukumu si utaratibu wa kiungwana ukifeli mtihani wowote unalaumu polisi ukikamatwa na bhangi unalaumu polisi!Askari Polisi wapo zaidi ya 45,000 aingii akilini hata kwa yule aliye pata division 0 hivi majuzi kuamini kwamba wote hao ni wabaya.Mimi ninaona suala la maadili ni janga la taifa kwa sasa kama ilivyo huko uraiani kuna watu wabaya na wema vivyohivyo hata Polisi kuna Askari wabaya tena ni watoto wenu,kaka zenu,dada zenu n.k ambao hamkuwalea vema na wale wanaobainika wanachukuliwa hatua za kisheria.POLISI IPO NA ITAENDELEA KUWEPO TOA MAONI NI NAMNA GANI TUBORESHE.Haikusaidii kutotoa ushirikiano kwa Polisi kwani wewe ni nani?Nchi ya watu zaidi ya milioni 40 huwezi ukawasemea wote wapo wanaoendelea kuheshimu kazi nzuri za Jeshi la polisi.Ni vizuri wakachukua maoni yako kama changamoto na si kukuingiza kwenye black list yao ...