Sifa kuu ya JK | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sifa kuu ya JK

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Geza Ulole, Mar 13, 2012.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,083
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  Mara nyingi hainiingii akilini pale huyu Mh wetu anapowaalika watu kwa mazungumzo na majadiliano ya mwafaka wenye Mstakabali wa Kitaifa halafu pale wahusika (yaani wawakilishi wa wenye kilio) wanapogeuka huyu Mh hufanya yasiyotarajiwa! Tumeona mchakato wa katiba ulipoanza huyu Bwana aliwaita viongozi wa CHADEMA kujadiliana nao baada ya kususia mchakato Bungeni kwa kutoka nje! Na pale wahusika walipotoa pua yao nje ya lango Kuu la Ikulu, huyu Bw. akasaini mabadiliko yale ya katiba yaendelee mpaka na mpaka leo hamna anayejua linaloendelea hata kama kuna kuchukua maoni hamna mtu anayejua wapi yanachukuliwa na hao wachukua maoni watakuja lini! na hii ikiwa haki yetu Kikatiba kama wananchi wa nchi hii!

  Hapa juzi baada ya wauguzi na madaktari wetu kulalama bila wafanikio, waliamua kugoma mara 2 bila ya mafanikio
  wakipewa ahadi na longolongo nyingi waliamua kugoma tena! Huyu Mh kawa kawaida yake aliwaalika wawakilishi wa MAT na mbali na viongozi hawa kuitikia mwito wake kwenda Ikulu na kujadiliana naye, walienda mbali zaidi na kukubali kusimamisha mgomo kwa nia safi! Huyu Bwana siku mbili baadaye alikutana na Wazee wa Dar na utumbo aliomwaga pale hausemeki na kwa kiufupi ni kuruka kimanga madai muhimu ya madaktari na wauguzi wetu katika shughuli zao za kila siku kwa kuyaweka kiporo bila kutoa dira ni vipi atayashughulikia! Kama vile kutafuta mchawi, Mh huyu wa fitna zilizozidi maelezo alienda mbali zaidi kuwaparamia wanaharakati walioandamana kushinikiza serikali yake ishughulikie swala la madaktari na wauguzi kwa kuwaita waliokosa ubinadamu kwa kushinika serikali yake ichukue hatua zipasavyo na kuunga mkono madaktari na wauguzi katika mgomo wao wa kuendelea kuua!

  Bwana huyu maarufu kwa uzabazabina alienda mbali na kuwa mkalimani na mtetezi mkuu wa haki za Kibinadamu kwa kuanza kutafsiri haki ya kuishi kama haki ya kwanza ya msingi inayotambulika kwa nchi zoote wanachama wa Umoja wa Mataifa! Katika hali ya kawaida katika kufikiri na kutenda kizembe Bw huyu alienda mbali na kuwasafisha viongozi wawili waliokataliwa na umati wa wafanyakazi walio chini ya wizara wanazoziongoza yaani Waziri na naibu Waziri na pia kutoa dalili ya uwezekano mkubwa wa hata yule Katibu Mkuu aliyesimamishwa kwa tuhuma kibao kurudishwa kazini! Haya yoote yanafanyika kweupe bila kutuambia ni kivipi serikali yake imesimamia haki hii ya wananchi wake kuishi kwa amani na utulivu huku tukijua kwa kipindi choote cha utawala wake kuna maalbino wanaendelea kuishi kwa kuhofia maisha yao na watuhumiwa wapo wametajwa lakini hakuna kilichofanyika kuhusu utendaji wa haki kwa wote! Pili Kizabazabina huyu mpaka leo hajatoa tamko lolote juu ya ukandamizaji na matumizi ya nguvu zilizopitiliza kwa wananchi pale askari wake huko Songea pale walipoamua kutumia bunduki na kusambaratisha maandamano ya amani ya kuishinikiza polisi isimamie ulinzi wa roho za Raia wema waliokuwa wakiuawa kwa sababu za kishirikina! Roho za marehemu wanne zilipotea huko...! Mbali ya hayo suala la utawala bora limeendelea kubaki la kufikirika kwa Mh huyu wa Wazee wa Dar!

  katika hali ya kawaida Mh huyu anakosa uhalali wa kuongelea haki ya kuishi kama anashindwa hata kutoa pole kwa waliopoteza uhai uko Songea kwa kupitia kwa wauaji wake walio chini ya uongozi wake! Ila Bw. huyu asiye na soni hakuona hilo ila lile la Madaktari na Wauguzi wetu waliojaribu kutumia kila mbinu ya ustaarabu kudai haki yao ya kuweza kujikimu na kufanya kazi katika mazingira s
  tahili kwa kazi zao hatarishi! Hivi kweli huyu Mh anategemea makubaliano na MAT yaendelee kwa jinsi alivyojirahisisha na kudhihirisha ahadi zake hewa ambazo wakati woote huzitoa na kuzigeuka ndani ya masaa 24 baada ya kuzitoa! Hivi yeye kama kiongozi mkuu wa nchi anategemea nani kuwa msuluhishi kama makubaliano yakivunjika? BTW hii jeuri anaitoa wapi ya kudharau matakwa ya wengi? Tutegemee makubwa haswa pale hulka ya ustahimilivu wa Watanzania itakaposhindwa!
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Huna zaidi ya majungu.

  Ukweli unabaki kuwa ukweli. JMK kiongozi wa uhakika.
   
 3. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,401
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Madaktari ndio wanaowawezesha wananchi kupata haki yao ya kuishi kwa kuwatibu wanapougua. Ukiwatengenezea madaktari mazingira mazuri ya kazi maana yake umewapatia wananchi mazingira mazuri ya kupata haki yao ya kuishi. Ukiwakwaza madaktari na kazi zao maana yake umewakwaza wananchi na haki yao ya kuishi. Sehemu kubwa ya haki ya kuishi ya mwananchi inapatikana kwa daktari. Sifikirii na siamini kuwa, kwa kuwazomea madaktari ndio njia nzuri ya kuwapa wananchi haki yao ya kuishi.
   
 4. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,401
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  Usiwe mwepesi wa kutoa majibu rahisi kwa hoja nzito. Kama ukweli ndio huo unaouamini toa basi hoja zako na wewe ku criticise hoja zilizotolewa moja baada ya nyingine.
   
 5. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Kiukweli hata mimi sikutegemea baada ya mazungumzo yale na madaktari ikulu, angeongea yale ya jana. Jana alikuwa na kazi ya kuwashambulia wanaharakati na madaktari. Hivi, vifo vya viongozi vinavyotokea na kuendelea kutokea sio haki zao za msingi za kuishi? Asijifanye ana machozi ya mamba. Aongelee kwanza utata wa vifo na maradhi na malalamiko ya viongozi wa chama na serikali ndio aje huku chini.
   
 6. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 689
  Trophy Points: 280
  Hii ni Mwanaasha original.
  Haijachanganyika kabisa hii!!
   
 7. MNAMBOWA

  MNAMBOWA JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 17, 2011
  Messages: 1,984
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  mlitaka aongee nn? Watz kwa ushamba wa siasa bwana, kama kulikuwa na matukio ya mgomo wa madaktari mnategemea aongelee ki2 gani? Mnaponzwa na uhuru wa kuongea, atakuja atakaye wafunga midomo.
   
 8. M

  Makupa JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Duniani kote ni watu wachache sana wenye tabia ya usikivu na mmoja wao ni Dr Jakaya Mrisho Kikwete ee mungu mmjalie maisha marefu
   
 9. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2012
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  sawa yeye majungu wewe weka masufuria yako hapa tuone uhakika wake na sijui kama tuliwahi au tutakuja kupata kiongozi dhaifu namna hii Mungu atuepushie mbali
   
 10. T

  Topical JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Madrs walio over do..walitakiwa kuambiwa ukweli kuwa resources zilizopo na madai yao ni vitu viwili tofauti mkuu..

  kwanza, Kwakuwa tumeamua kuwa katika soko huru serikali si muajiri pekee wa madrs wanaweza kwenda kwenye sekta binafsi bila kubughudhiwa na serikali..

  Pili, wanaweza kujenga hospitali zao wakalipana na kuweka mazingira ya kazi zao bora kama peponi..wenye uwezo watakwenda huko na watakuwa na hela kama kakobe..

  tatu, mdrs walitakiwa kuingilia wajibu wa kikatiba wa rais, katika kumchagulia nani afanye naye kazi, badala ya kufuata kanuni bora ya majadiliano na kujikita kwenye madai yao ya msingi..

  Madrs chapeni kazi nchi hii ina matatizo lukuki tangu enzi za st. nyerere kuyamaliza inahitaji muda na mikakati ya muda mrefu..
   
 11. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Ng'ombe akipelekwa machinjioni huwa hajui, kimsingi hautofautiani naye!!!!!!!
   
 12. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #12
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Sikumbuki kama jk aliwaita chadema ikulu.
   
 13. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #13
  Mar 13, 2012
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Tupo kwenye season one Episode ya pili...Siasa zinaingilia utaalam na wataalamu wanachukulia advantage ya madhaifu ya siasa kuumiza wasiojua ABC za siasa...Naichukia serikali ya CCM,nawachukia viongozi wa MAT kwa kujua udhaifu wa viongozi wetu na kuwawekea mtego of which waliuvagaa na matokeo yake tumewapoteza ndugu zetu...let em go to hell muda wao wa kuishi utakapofikia kikomo!
   
 14. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #14
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Your chosen name is not represented by the strength of your mind....
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Hivi Jk hana zuri?
   
 16. B

  Burebure Member

  #16
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kwa hakika tunashindwa kumuelewa kabisa mtu huyu!@Anatetea haki ya kuishi kwa binadamu na Je,hao waliopigwa risasi na polisi huku Songea hawakuwa na haki ya Kuishi??
   
 17. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #17
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Usijidanganye ngugu yangu! Binaadamu sote tunategemeana na kwa kuanzia fahamu kuwa hakuna anaezaliwa kuwa Daktari bali hupitia sehemu nyingi hadi kufikia hapo. Hivyo kufikiri kuwa mtu fulani awe bora zaidi ya wengine si sawa!
   
 18. NdasheneMbandu

  NdasheneMbandu JF-Expert Member

  #18
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 940
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Amewahi kuongoza familia yako nini!!
   
 19. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #19
  Mar 13, 2012
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Kwa nn asizungumze na vijana wa DSM? Maana wazee wenyewe sidhani hata kama wanaelewa wanachohubiriwa ni kama wamekusanywa tu kwa lengo maalum la kufanya kundi fulani lionekane baya kwa jamii,
   
Loading...