Sifa 10 za mwanamke bora wa kuoa

Sifa 10 za mwanamke bora wa kuoa

Askarimtu

JF-Expert Member
Joined
Sep 7, 2019
Posts
277
Reaction score
185
Mwanamke ni utukufu wa mwanaume kwa sababu ametoka kwenye ubavu wake. Mwanamke bora ni huyu hapa:

1. Mwenye heshima kwa wadogo mpaka wakubwa. (USAFI WA MWILI, MATENDO & MDOMO)
-Sio anatukana tu ovyo ovyo halafu we unaenda kuoa, atakuja kutukana wazazi wako.
-Ataharibu watoto, mtoto akikosea anamtukana matusi makubwa makubwa.
-Siku atakutia aibu mbele za watu.


2. Anaekubali kuwa chini ya mme wake. (UKWELI UNAUMA)
-Hapa naongea hasa na wasomi. Mkigombana kidogo tu atasema kila mtu achukue hamsini zake,
hawezi kuwa chini ya mwanaume kwa kisingizio cha kumpanda kichwani.


3. Muelewa wa elimu ya mambo ya MwenyeEnzi Mungu vizuri. (MCHAMUNGU)
-Ukikosea hapa utalogwa wewe na familia yako na wote mtakuwa chini yake.


4. Muwazi na mkweli na mwenye upendo.
-Ataonganisha familia.
-Atakusaidia kufahamu historia yake vizuri. Maana kuna wengine wakisikia kuwa mkeo alikuwaga hivi au vile/ au ukijua kwa uchunguzi wako tu kuwa mkeo alipita hapa na pale, ila yeye hakukuambia inauma sana (ila wengi hujifanya yakale yamepita ila moyoni mwao sivyo).Inauma kwa sababu umegundua mwenyewe ila yeye hakukuambia(unaanza kujiuliza, kwanini hakukumbia kitu muhimu kama hicho, kwanini alificha?). Ni vizuri kufahamu historia ya mwenzio hata kama ni mbaya au inauma.


5. Asiyehangaika na dunia hii kwa lolote lile. (ULEVI,UMBEA, USENGENYAJI,STAREHE)
-Asiyependa starehe, asiyetumia kilevi (Japo wanawake walevi hukataa kuwa ulevi huvunja ndoa au mahusiano)
=(Iko hivi hata kama mwanaume ni muhuni na mlevi wa kutupwa, usidhani kwamba atachagua mtu wa aina hiyo, atakupitia tu na kukuacha).
-Mfano: Unaweza kupata tom-boy(Japo sio vizuri kuwa tom-boy) na hawa huwa wanawake waelewa sana na akija kuamua kuacha utom boy kwa umri fulani hapa 60-70% anakuwaga ni mke wa juu sana, hawa wanawake ni ngumu kudanganywa na hujua nini ampe mumewe na familia kwa ujumla, na maranyingi huwa na mioyo meupe sana isiyohifadhi chuki, ukimchukiza anakwambia hapohapo...wengiwao sio wasengenyaji na huacha tabia zote hasa akishaanza kuwa mke. Achana na wale matom boy wahuni na wavuta bhangi.


6. Asiyependa matumizi ya vipodozi (kujichubua) wala vitu feki (kucha za kubandika na mawigi), na vitu vya kuvaa kama hereni, bangili, vikuku n.k. (NATURAL)
-Ili asikuletee mapepo na ibada za miungu nyumbani, mikosi na mabalaa, hasa majini mahaba.


7.Mwenye quality na quantity unayoitaka wewe ya kimwili, asikulazimishe mtu ili kesi zote uje ujibu mwenyewe kwa Muumba wako kwa habari ya zinaa na kutowajibika.
-Mwanya, lips, kiuno, miguu, shingo, mabega, mgongo, hips, nywele au hata kifua.


8.Asiye lazimisha ndoa ifanyike haraka. (FAHAMIANENI VIZURI KWA MDA/ACHA UKURUPUKAJI & UPELEKESHWAJI)
-Wanawake wanaopenda ndoa, hupenda sifa, hupenda harusi halafu ndoa ikawashinda.
-Inaepusha kuuziwa mbuzi kwenye gunia. Hasa kwa wale wasiopenda wanawake waliozaa.


9.Asiye na tamaa, asiyeyumbishwa na mali au anayekataa kujamiiana kabla ya ndoa.
-Huyu ana msingi mzuri wa maisha na familia yako ya baadae itakuwa bora, huyu ndio yule hasa kifo kitawatenganisha.


10. Wewe mwenyewe mtafutaji mke uwe na kichwa kizuri.
- Sio upoupo tu halafu unatafuta mke, jielewe kwanza, jitambue na amua. Acha kufuata mkumbo.


*********************************************************************************************************************************

MWISHO:
Acha kudharau wanawake, nao wana mioyo na haki kama wewe, usichague quality wakati wewe mwenyewe huna quality, utaleta shida tu duniani. Bahati nzuri au mbaya ni kwamba, msipopatana na mkeo hata ufanyeje maombi yako hayatakubaliwa. Mungu huwasikia sana hao watu usije ukasema kuwa mwanamke huyu ni mikosi, kumbe mikosi umeileta wewe mwenyewe kwa kumuonea mwenzio.

1 PETRO 3:7

Kadhalika ninyi waume, ishini na wake zenu kwa kuwahurumia, mkitambua ya kuwa wao ni dhaifu na hivyo muwape heshima, kwa maana ninyi ni warithi pamoja nao wa neema ya uzima. Fanyeni hivyo ili sala zenu zisizuiliwe.





UPENDO NI WA KWANZA, NA KILA MTU AMHESHIMU MWENZAKE KAMA NAFSI YAKE!!!!!!!!!
 
Ya 4 s sifa tu,
Mm naona n msingi kabsa wa mahusiano yoyote.

Sifa ya 11
Urafiki🌹
 
Hadi hereni ni kitu fake hakitakiwi kuwepo mwilini?
vitu feki (kucha za kubandika na mawigi), na vitu vya kuvaa kama hereni, bangili, vikuku n.k. (NATURAL)
-Ili asikuletee mapepo na ibada za miungu nyumbani, mikosi na mabalaa, hasa majini mahaba.
Amka unawe uso halafu ufikirie tena. By the way Ahsante kwa maneno murua
 
Kwa ulimwengu wa sasa hizo sifa hazipo tutafute njia mbadala ya kuendana na hawa wanawake
 
Back
Top Bottom