Kada wa CHADEMA
JF-Expert Member
- Feb 27, 2016
- 289
- 615
Peter Kibatala, John Mallya, Tundu Lissu na wengineo hakika ni vyombo tunavyojivunia CHADEMA. Tuliambiwa kuwa vyombo hivi vikisimamia kesi kwa hakika lazima ushindi upatikane. Nakumbuka Tundu Lissu alivyomuita Rais Magufuli Dikteta Uchwara aliwekwa rumande kwa masaa kadhaa. Hata hivyo, baada tu ya kufikishwa Mahakamani hakika ushindi ulikuwa upande wetu.
Najiuliza, nini kimetokea kwa Godbless Lema? Najiuliza pia, ni sababu gani CHADEMA tumeshindwa kuwapeleka nguli wa Mawakili kumtetea Lema? Kwa nini tumepeleka watu dhaifu ukimuoneoa John Mallya kiasi ambacho si tu wameshindwa kupambana na hoja za Serikali lakini pia wanaonesha kukata tamaa mapema? Hawa mawakili wametoka wapi?
Niwaombe sana ndugu zangu wa CHADEMA. Hatumtendei haki Godbless Lema. Hakika akitoka Jela inabidi ajiulize mara mbili. Yaani tunajisikia faraja sana kutumia nguvu zetu na uwezo wetu kisheria kuwatetea akina Denis Wilson, yule aliyemtusi Rais Magufuli? Kwa nini tumemtelekeza Lema? Nini nyuma ya pazia? Au lile andiko lake la kulaani kitendo cha CHADEMA kuwachangia fedha za dhamana wale wanaomtukana Rais? Ndo maana tumeamua kumuacha aozee Selo?
Au tumeamua kukaa kimya baada ya kuamini kuwa Lema anajikaanga mwenyewe kwa maruta yake?
Si sahihi hata kidogo