Sababu wewe Akili yako ndio umeweka huko, gunduzi nyingi unazoziona karibuni ni sababu ya mafuta, mafuta ndio yameleta abundant raw material ambayo haikuwepo mwanzo, naweza kukuuliza same thing kwanini wazungu hawajagundua internet 1800s ama 1700s ama 1600s etc, utakuja jibu pale pale. Na gunduzi za Leo zisingekuwepo incase wangeanza from scratch, wameweza kugundua kutokana na kutumia gunduzi za wenzao
Ukiangalia hapo middle East, Dunia yetu ya Leo inaendeshwa na Algorithm kuanzia hizo computer, internet na mambo mengi uliyotaja hakuna Algorithm bila Al khawarizim, Baba wa hisabati ambaye Aneandika formula nyingi,
Hizi ni Tool alizotumia Al zahrawi Baba wa upasuaji, same things ukienda Leo hospitali utazikuta
View attachment 3604092
Suruali unayovaa Leo wapersia ndio wameisambaza Duniani, pengine ungekua umepiga kimini chako sasa hivi unawaiga wazungu
Ukienda China utakuta gunduzi za Karatasi na kuprint, bila Karatasi hakuna vitabu vingi na bila vitabu kusambaa knowledge ingesambaa vipi Dunia nzima?
Wachina pia wamegundua Baruti, Leo hizo bunduki, makombora etc source yake utaipatia hapo hapo.
Wagundua pia vitu kama Compass, Earthquake detector, chai, saa na mambo mengi.
Long story short civilisation haishii kwenye gunduzi Tu Bali ni way of life.
Nimewahi Kutoa mfano mzuri humu, hao watu wa Middle East na Africa ndio wamewafundisha watu wa Ulaya kuoga kila siku, kupiga mswaki, kujiremba etc there was A time Ulaya kutokuoga ilikua ni sifa, Mfalme anajisifia maisha yake yote ameoga mara 3, mwengine anajisifia anaoga mara 1 kwa mwezi etc. hata mabaki ya Crusaders yanaonesha sifa yao ilikua ni Uchafu.
Leo hii kwa siku MTU anaoga mara kadhaa na anapiga mswaki mara kadhaa, akitoka anahakikisha manukato kidogo kajipaka huoni kwamba ni civilisation hio?