Sielewi dhamira ya huyu dada kwangu

Sielewi dhamira ya huyu dada kwangu

Dogo G

JF-Expert Member
Joined
Jul 6, 2018
Posts
1,052
Reaction score
440
Wakuu,mimi kuna nyumba moja nimepanga huku kitaani kwetu ni nyumba quality sana miongoni mwa nyumba za namna hii chache hapa mtaani kiasi kwamba mandhari yake yapo safi sana pametulia wapangaji tupo wawili tuu na hawo wenye nyumba kwa upande wao wanasehemu yao kulingana na mtindo wa nyumba hii ulivyo,sasa lengo langu si kueleza nyumba hii ila ni haya yanayonikuta.

Nimehamia nyumba hii,huu ni mwezi wa pili sasa tokea nihamie mwezi wa tano mwishoni,hapa kuna mama mwenye nyumba anayejiweza kiuchumi kwan anamiliki maduka ya nguo na ana hospitali yake ndogo hivi.Huyu mama huwa hashindi sana nyumbani kutokana na hizo shughuli zake anazosimamia kwahivyo unaweza ukaonana naye mara mbili au tatu kwa wiki na smtmz huwa anasafiri kabisa,sasa hapa nyumbani kuna binti yake wa kwanza yupo na mdogo wake anayesoma sekondari moja hivi japokuwa mara nyingi anayeshinda nyumbani ni huyu dada na housegirl tuu.Huyu dada anafanyia kazi kwenye hospital ile ya mamaake kwahivyo kapewa kitengo pale.

Shida iliyopo huyu dada simuelewi kabisa ndugu zanguni vijana wa siku hizi huwa wanasema HASOMEKI,yaani nimeshindwa kumsoma kabisa.kuna vituko na mambo ambayo huwa nayaona hata sipati picha mantiki yake.Huyu dada huwa ananichukia chukia tuu,akiniona nimetoka kazini tu punde ataanza kujifanya anaanzisha stori na yule housegirl wataanza kuongea majungu kwa sauti na ukitafsiri utagundua yanakulenga moja kwa moja.Utakuta wanasema tabia za kabila langu huku wakicheka,mara idara nayofanyia kazi wanaikashfu kwa vicheko japo hawanitaji mimi.Sometimes tukionana hivi anapenda nianze kumsalimia na mara nyingi mimi huwa namuanza na nikimsalimia anaitikia sauti kama yupo shimoni tena kwa madoido hivi.

Kuna siku nimetoka kazini niko ubao nawaza kuanza kukiwasha kigae nifanye harakati za chakula akamtuma housegirl msosi kwenye hot pot kukiwa ni ndizi na samaki tena inaonyesha viliandaliwa special to somebody,mimi kwasababu nilkrahisishiwa process nikakila huku nikifikiria mara mbili mbili hivi.Baada ya kula,nikaenda kumgongea mlango hakufungua yeye akamtuma yule housegirl kwa niaba yake zaidi nikamwambia yule housegirl nashukuruni baasi.Jana umeme uliisha sasa huwa kuna uraratibu wa kulipa ilibidi nilipe mimi sasa sikuwepo nikakuta amelipa kwa niaba yangu tena akazidisha kiwango ambacho huwa kila mpangaji anatakiwa kununua na akanunua umeme,Nilishangas sana kwani sielewi.Lakini kinachonishangaza ni kila tunapoonana yaani ananiangalia kwa chuki flani hivi anachange sura(kama anataka kusonya) na hajawahipiga stori na mimi hata siku moja

Hivi kwa namna hii huyu mtu mnamkadiriaje.sijui dhamira yake kwangu nashindwa kutabiri malengo yake kwangu wakuu(huyu dada kanizidi miaka 2 tuu).

Ni hilo tuu,mawazo yenu wataalamu wa saikolojia za wanadamu.
 
Inaonekana aura zenu haziendani.


Ila kwa kichekesho tu, subiri housegirl wao akiondoka mvizie uingie jikoni kwao kamata kopo la chumvi kaza kabisa alafu rudi chumbani kwako kulala
Nakuhakikishia lazima atakuja mwenyewe kukuonba ukamfungulie
 
Inaonekana aura zenu haziendani.


Ila kwa kichekesho tu, subiri housegirl wao akiondoka mvizie uingie jikoni kwao kamata kopo la chumvi kaza kabisa alafu rudi chumbani kwako kulala
Nakuhakikishia lazima atakuja mwenyewe kukuonba ukamfungulie
Umenichekesha sana mkuu hadi stress za mfalme jiwe nimezisahau kwa muda
 
jaribu kufuata kanuni na taratibu za uandishi, umeandika hovyo hovyo mno, haivutii kusoma, fanya editing then rudi tukupe ushauri.

NB; kwani upo kidato cha ngapi?
 
sijaimaliza hii story yote kuisoma Hajar njoo unambie kimejir nin huku
Hahahaa. Subiri nitafute miwani mdogo wangu. Naja naja sasa hivi kusoma kisha nikwambie kilichojiri.

zeshchriss mkombozi wenu nipo ngoja nivae miwani kisha nipitie mstari kwa mstari niwaambie nini mleta uzi anataka saidiwa sababu na weye najua umeisha katikati. Hahahaaa.
 
Pamoja na watu kukuponda ulivyoandika ila nmekuelewa japo hueleweki sana kwa jinsi ulivyomfafanua hyu demu,ila ngoja nikupe ushauri kidgo halaf utapata jib ni aina gan ya huyu dada alivyo na nia yake kwako,,nenda katafute demu mkali mara kumi ya yeye,ambae anavutia kuanzia juu mpk chini,hakikisha anavutia kweli kweli zaid yake,halaf nenda nae nyumban na uhakikishe hyo dada yupo,kaeni ndan kama unapika piken kula halaf usimfanye cchte wakat unatoka kumsindikiza hakikisha hyo dada na house gal wake wapo nje ita uber mpe huyu dem uliekuja nae mle laki mbili au tatu mbele yao halaf muagane vzr baada ya hapo utajua nia haswa ya huyo mwanamke ni nn.[emoji112] [emoji112] [emoji112] [emoji112]
 
Back
Top Bottom