Siasa zilizokataliwa na Edward Lowassa zimeharibu brand ya CHADEMA

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,390
5,310
Mara baada ya Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kujiunga na kuinunua CHADEMA ili awe mgombea urais mwaka 2015 , kitu cha kwanza kabisa alipokabidhiwa tu chama alipiga marufuku siasa za kiharakati na kushauri siasa hizo hazina tija kwa sasa. Edward Lowassa alionya kuwa CHADEMA lazima igraduate kutoka chama cha kiharakati hadi kuwa chama cha siasa sasa.

Edward Lowassa alifafanua madhara ya chama kubaki cha kiharakati muda wote kuwa ni pamoja na kupinga maendeleo yote ya nchi ,kuombea mabaya nchi, kushirikiana na mabeberu ili kuiibia nchi, pamoja na kushangilia kila lililobaya kwa taifa ili kumfurahisha tu anayefadhili hizo harakati zako.

Matokeo ya harakati hizi ni chama kuchukiwa na wazalendo na kupoteza ushawishi kwa Wananchi.

Hakika Lowassa aliona mbali. Leo brand ya CHADEMA imeharibiwa vibaya, chama kilichojizolea umarufu kwa kutetea wanyonge leo kinataka machinga na mama ntilie wafukuzwe mitaani! Leo ni furaha kubwa kwa CHADEMA ndege kukamatwa na wazungu!!!

Pia tangu tarehe 17 mwezi Machi Tanzania imekumbwa na simanzi isiyo na kifani mara baada ya kutangazwa kwa kifo cha Rais Magufuli.

Mamilioni ya watanzania wameangua kilio kila kona kwamba sasa mwokozi wao ameondoka, cha kushitusha ni kwamba wananchi wa hali ya chini kabisa ndiyo wanaoongoza kwa kilio kinyume na tulivyokuwa tumeaminishwa kwamba Magufuli alikuwa ananyonga wanyonge!

Kitendo cha hayati Rais Magufuli kuagwa na mamilioni ya watanzania huku wakiangua vilio njia nzima na kutandika kanga zao chini ili mwili upite imeenda kinyume kabisa na wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lissu na genge lake.

Kwa jinsi msiba huu unavyoenda naamini utakuwa darasa tosha kwa wasaliti wa nchi hii akina Tundu Lisu ,Godbless Lema, Chahali, Ngurumo, Mange Kimambi na wengine wengi, sasa wataelewa kumbe watanzania siyo vilaza.

Wataelewa kumbe watanzania wanajua yupi anapigania haki zao kwa vitendo na ni yupi ni mpiga makelele nyuma ya keyboard.

Kwa mapenzi haya yanayoonyeshwa na Watanzania kwenye msiba huu ni lofa tu atakayeendelea kuamini kwamba eti Tundu Lisu aliibiwa kura kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Wito wangu kwa wasaliti wa nchi hii wanaoshangilia msiba kwamba sasa Magufuli ameondoka watarudi Tanzania na kuanza tena kutumika kuiba rasilimali za nchi hii kama walivyokuwa wanafanya huko nyuma wajue tu kwamba wanapoteza muda.

Watanzania siyo vilaza ,wanajua fika Tundu Lisu aliwatisha kwamba watashitakiwa MIGA ikiwa watabadili sheria za madini.

Tundu Lisu aelewe kuwa hawezi kuwa rais wa Tanzania kwa kushinda Twitter akikejeli kila lililojema kuhusu nchi yetu.

Tundu Lisu kupitia msiba huu atakuwa ameelewa na kupata darasa kwamba ukitaka kupendwa na Watanzania tumikia watanzania na siyo kutumikia Acacia.
 
Screenshot_20210323-082956_Chrome.jpg

hii kama kiongozi sio sawa. ni bora kupiga kimya ubaki kushangaa tu. unless uandike to a very positive tone
 
Njia mojawapo ya kutotatua tatizo ni kulizunguka. Utajifurahisha umetatua tatizo, lakini unalisukuma mbele ili lije tena. Kwa maneno mengine, umefanya hivyo.
 
Nitawashangaa chadema 2025 kama wataingiza pua kwenye uchaguzi kupambana na IRON LADY. Jana kapigilia msumali wa kimamlaka kwamba; Yeye ndiyo RAIS NA AMIRI JESHI MKUU WA VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA. TII SHERIA BILA SHURUTI, CCM NI ILE YA JANA NA LEO.Hongera sama Mama tuvushe zaidi ya mtangulizi wako

KIMETOKA CHUMA KIMEINGIA CHUMA, a.k.a IRON LADY
 
Back
Top Bottom