Siasa zetu na lawama kwa raisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa zetu na lawama kwa raisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Apr 22, 2010.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Nime kaa na kutafakari hivi ni kwa nini kiongozi mkuu wa nchi ana beba lawama zote? Tuangalie mifano michache. Marekani mzigo wote sasa hivi ana bebeshwa lawama Obama, Uingereza sasa hivi Gordon Brown ana bebeshwa lawama za serikali aliyo rithishwa na tusipo enda mbali hata haa nyumbani K ndiye anaye bebeshwa lawama nyingi kama si zote. Swali langu ni je hiyo ni haki? Kweli mtu mmoja anaweza kubebeshwa mzigo wote wa makosa ya kiutendaji na sera?

  Kwa hiyo nika jaribu kuangalia kwa Tanzania yetu ni sababu zipi zinazo weza kufanya raisi asifanye vyote alivyo kusudia kufanya. Raisi Tanzania ana nguvu nyingi theoretically lakini nime gundua practically sivyo ilivyo.

  a)Chama: Kama unavyo jua raisi anabidi kwanza apate idhini ya chama ili kugombea na kisha kupata uraisi. Chama ndicho kinacho kuja na ilani na si mgombea binafsi. Kwa maana hiyo kuna vitu vitaingizwa kwenye ilani ambavyo mgombea ana weza asi kubaliane navyo lakini inabidi acompromise. Pia kwenye chama kuna watu wengi tu wenye ushawishi ambao raisi hawezi kuwa chunia.

  b)Wana siasa wengine: Kila mwanasiasa ana linda maslahi ya watu au mtu fulani. Maslahi haya yanaweza yakawa binafsi, ya wapiga kura wake au kundi fulani. Kwa hiyo basi pale sera au mpango za raisi zita kapo gusa interest za watu fulani lazima kutakuwa na backlash. Na kama tunavyo jua hauwezi kuridhisha makundi yote. Lazima kuna makundi yata kayo ona yame punjwa.

  c)Balance of power: Japo hii siyo very strong Tanzania lakini kama unavyo jua serikali lazima ifane kazi pamoja na bunge. Hii inafanya maamuzi mengine yachelewe au yasifanyike kabisa.

  Kwa kifupi nilicho gundua ni kwamba politics is a game of compromise. Siyo raisi kupata au kufanya kila kitu unacho kusudia. Kuna maraisi kama Nyerere walio kuwa na bahati ya kuwa na ushawishi mkubwa kwa hiyo ikawa raisi zaidi kwao kufanya wanacho kusudia ila kwa sasa hivi ni ngumu. Nakubali raisi ni kiongozi na kama kiongozi lazima kubali kukwepa lawama. Nakubali pia kwamba kuna vitu raisi anafanya ni uzembe wake mwenyewe. Lakini pia inabidi tuangalie factors zinazo weza sababisha mambo mengi yasifanyike na mara zote si makosa ya raisi. Na simuongelei JK tu. Naongelea maraisi waliopita na hata maraisi wajao wawe wa CCM au chama kingine lazima wata deal na hii kitu.
   
 2. m

  magee Senior Member

  #2
  Apr 22, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nijuacho mimi kwa uelewa wangu mdogo ni hiki.......
  Kiongozi yeyote anapokaa kwenye kiti ni wananchi ndo wanaokuwa wamemuweka pale.Ni kura yako ndo imemuweka pale na yy ndo anakuwa ameaminiawa kubeba dhamana ya wananchi wakitegemea afanye vitu vinavowahusu wananchi kwa ujumla wao na sio kwa mtu mmoja mmoja.LAWAMA ZINATOKA PALE KIONGOZI HUYO ANAPOSHINDWA KUTAMBUA MATAKWA YA WALIOMUWEKA KWENYE KITI(WANANCHI) AMA KUYATEKELEZA,AMA KUENDA KINYUME NA MATAKWA YA ANAOWAONGOZA AMA KUTEKELEZA MATAKWA YA TABAKA FULANI TU.UONGOZI NI DHAMANA KUBWA MNO,NI UJUMLA WA WATU KUKUAMINI NA KUTARAJIA UNAWEZA KUWAFIKISHA WANAPOTAKA.TATIZO LA MARAISI WENGI HAWAJUI DHAMANA WALIZOBEBA WANASHINDWA KUKEMEA MAOVU,MBONI ZAO ZIMEFUNGA HAWAONI NA MAADILI KWAO NI SOMO GUMU MNO.SISI WANANCHI TWAWEZAONDOA HILI KWA KUHAKIKISHA TUNAFANYA LIBERIZATION MARAISI WABAKI TU KAMA PICHA.
   
 3. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #3
  Apr 22, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Katiba ya Tanzania inampa Rais wake madaraka makubwa sana ya kuteua watu wa kumsaidia kazi zake (Waziri Mkuu, Mawaziri, manaibu mawaziri, makatibu wakuu, manaibu katibu wakuu, wakurugenzi mbalimbali, makamishna mbalimbali, Wakuu wa mikoa, Wakuu wa wilaya, mabalozi, maofisa wa Ikulu, wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama na kadhalika), kuwabadilisha kazi hao viongozi wenzake mara nyingi kadri anavyotaka, kuunda Wizara, kuzipanguapangua atakavyo, na kuunda Taasisi nyingine za kuendesha nchi kwa kadri ya utashi wake.

  Rais wa Tz ana hadi madaraka ya kuteua wabunge kumi kuingia kwenye Bunge la Muungano. Hii inapoteza dhana ya kuwa wabunge wote ni wawakilishi wa wananchi. Hawa wanamuwakilisha yeye Rais aliyewateua. Na Rais ni Dola. hao kumi wanawakilisha Dola.

  Kali kuliko zote, Rais wa Tz ana mamlaka ya kulivunja Bunge lililochaguliwa na wananchi na kuitisha Uchaguzi Mkuu...

  Kwa mamlaka aliyonayo, Rais wa Tz kama akitaka ana uwezo wa kuamuru vyombo vya Dola kuwakamata na kuwashtaki watuhumiwa wakuu wa ufisadi...

  Rais aliyepo kwa sasa pia ni Mwenyekiti wa Chama kinachotawala. Akitaka/angetaka pia anaweza kutumia Chama chake kuwashughulikia mafisadi walio ndani ya Chama hicho...

  The bottom line is that the President of Tanzania has almost absolute power. If he(she?) want, he/she can make peoples' lives better. If...
   
 4. M

  Mchili JF-Expert Member

  #4
  Apr 23, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nakubaliana na wachingiaji hapo juu kwa 100%. Raisi ana haki na anasthili kulaumia kwa matatizo mengi yanayowapata wananchi hasa Tanzania. Kama raisi anataka kubalance power ili awafurahishe rafiki zake, huyo sie tunaemtaka wala watanzania hawakumtuma kwenda kutafuta maswaiba. Kama ni masuala y ailani ya uchaguzi, kuna mambo mengi sana yanafanyika sasa hivi kinyume na ilani ya uchaguzi ya ccm. Kwa hiyo hata wana ccm wenyewe hawafurahishwi na utendaji wa JK.

  Raisi akiamua kufanya kwa maslahi ya umma hata kama chama chake watampinga umma utamtetea na atashinda. Mfano mzuri Obama na sera yake ya afya ilipingwa na wanasiasa matajiri lakini amelazimisha pamoja na democrsia iliyopo America. Kwa hiyo raisi akishindwa kufanya to expectation of his/her people anastahili kulaumiwa. Sisemi awajaze watu mahela ila atengeneza smooth play ground, socially, economically and politically.
   
 5. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #5
  Apr 23, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mwanafalasafa huyu Rais unayejaribu kum-define wala si Rais chochote ni mzigo tu. Rais wa maana hayo yote hayawezi kumshinda. Kwa mfano Rais wa Serikali ya Tanzania ndiye pia Mwenyekiti wa vikao vyote vya juu vya Chama tawala CCM. Hata kama wenziwe wanaweza wakawa na mawazo ama msimamo tofauti yeye ndiye mwenye rungu na 'veto' kumuwezesha kuamua kile anachoona ama anachoamini kwamba kinalifaa. Yeye ndiye anayepaswa kuwa na mawazo mazuri na kuyauza kwa walio chini yake ili yakubaliwe. Kama hana convincing power aliutaka uongozi kwa ajili gani? Ataongozaje bila kuwa na convincing power?

  The crap about yeye kutotayarisha ilani is another lie. Hata kama ilani hiyo inatayarishwa na maafisa wa Chama ama Kamati za Chama or whatever, lazima huyo/hao wanaotarajiwa kuwa Wagombea urais watakuwepo kwenye final vikao vya kupitisha Ilani hiyo na kuweza kutoa mawazo na msimamo wao individually. Pia, inawezekanaje Chama kitayarishe na kupitisha ilani isiyotekelezeka? Kupitisha ilani isiyotekelezeka ni collective responsibility na uzembe wa wote including huyo mgombea urais ama Rais/Mwenyekiti aliye madarakani. Kutoa sababu ya aina hiyo ni kujitetea kusiko na tija.

  Hakuna suala la kuchuniana kwenye mambo mazito yanayohusu uongozi wa nchi. Wala si lazima awepo mtu kama Nyerere. Nyerere was a human being just like you and me lakini alikuwa anaelewa uongozi maana yake nini. Uongozi si lelemama. Na mtu anapojitokeza kutaka kugombea uongozi wa nchi lazima aelewe na kuzingatia hilo. Mgombea uongozi wa aina yoyote ile yabidi ajue kwamba anataka uongozi kwenda kutumikia atakaowaongoza na si vinginevyo. Hapaswi kugombea kuridhisha nafsi yake, ya mkewe ama marafiri zake. Kama kiongozi anakubali na kuwaachia watu walinde maslahi yao kwa kuogopa backlash basi huyo si kiongozi! Naam huwezi kuridhisha makundi yote lakini at least utafanya yale unayoamini kwamba yana manufaa kwa Taifa, regardless.

  Hiyo balance of power gani wakati kila mhimili una shughuli zake maalum na kiongozi wa nchi ndiye overseer wa shughuli zote nchini? Bunge linatunga sheria, Mahakama inahukumu wavunjaji wa Sheria, Rais anaongoza nchi. Rais hawezi kushindwa kuongoza nchi ama kutoa maamuzi kwa kisingizio cha kutaka kufanya kazi pamoja na Bunge. Rais anayo majukumu yake ambayo wala hayawezi kuzuiwa na Bunge unless Bunge linaamua kupiga kura ya kutokuwa na imani na Rais kutokana na uovyo na ulegelege wake.

  Hakuna chochote wala factors zozote zinazoweza kusababisha mambo yasifanyike kama Rais anayo dhamira ya dhati ya kutaka mambo hayo yafanyike kwa manufaa ya Umma uliomuweka madarakani. Tatizo la viongozi ama marais unaowazungumzia ni kule kuweka mbele maslahi yao binafsi na kulinda maslahi ya marafiki zao badala ya kuangalia na kuchukua hatua zinazostahili kulinda maslahi ya Umma na Taifa kwa ujumla.
   
 6. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #6
  Apr 23, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Mkuu umeandika sana ila kwa hoja yako, nini maana ya kuwa rais? Nani kamnyima kikwete influence? Kisa cha nguvu zake kuwa za nadharia bado hujanishawishi. Urais ni taasisi lakini hiyo si sababu ya kumpoka nguvu za kimaamuzi na kiutendaji. Kwa ufupi rais wetu ni dhaifu na si rais mtendaji. Kwa utendaji wake huu, tungehitaji waziri mkuu mwenye nguvu kisiasa ili jakaya abakie rais wa hafla mpenda ndege
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Apr 23, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  After all come election day, ni raisi anayezunguka nchi nzima kuomba kura.
   
 8. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #8
  Apr 23, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Rais wetu hawezi kuzikwepa hizi lawama - hata anavyokuja tena kuomba kura zetu ajue hajatimiza kazi aliyoiomba mwaka 2005. Sisi ndo tuliomwajiri na yeye anatutumika sisi na si vinginevyo.
  Amepewa Mamlaka makubwa na Katiba yetu ya nchi ili imuwezeshe yeye kuunda timu ya wasaidizi wake anayoamini kumsaidia kutimiza yale aliyotumwa na wananchi wake, sasa linapotokea suala la uzembe au udhaifu fulani, sisi hatuwezi kuwalaumu wasaidizi wake maana yeye ndiye aliyewaamini - lawama zetu zote zinamwishia yeye. Simple as that.
   
 9. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #9
  Apr 23, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Kama aliweza kukili kuwa hajui kwa nini TZ ni maskini, hata akihojiwa kazi zake atataja kusafiri kwenye nchi zilizo endelea ili akinge kikapu cha kusaidiwa
   
 10. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #10
  Apr 23, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kwani nyie mna shida gani hasa ambayo rais wenu mnataka awafanyie??

  Umaskini ondoa mwenyewe usitegemea rais? kulalamika na kulaumu bila kufanya kazi ni ujinga!

  Sera zipo, sheria zipo, katiba ipo na ameilinda na kusimamia..

  hebu tajani mambo kumi ambayo unataka rais akufanyie..fanya assesment za kutosha

  wengi walalamishi ni jamii ile iliyozoe "kupendelewa"
   
 11. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #11
  Apr 23, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Umenikosha..Jamaa hana jipya wala sio presidential material
   
Loading...