Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,353
- 38,586
Hii picha iliyopigwa Mwaka 1910 inaonesha ni jinsi gani Ushawishi wa siasa Zanzibar ulikuwa ni jambo la kimataifa na wala si jambo la makabila enyeji ya Zanzibar pekee!! Ukiagalia hapo katikati mwenye kofia nyeupe na amevaa suti ni Muingereza na "waswahili" wanaonekana wakiwa wamevaa nguo zenye kusawiri asili ya Irani na arabuni.
Kama kuna watu wanadhani heka heka za siasa Zanzibar zinahusu watwana na mabwana anajidanganya. Siasa za Zanzibar tangu huko mwanzo mpaka sasa zinahusu maslahi ya kiuchumi na mbinyano na malumbano yanahusu ni nani ashike njia (channel) za kuudhibiti uchumi wa Zanzibar na vyanzo vya chumi za nchi nyingine Tanganyika ikiwemo!!
Asalaam aleykhum Zanzibar!!