Wanabodi,
Hakuna kitu kizuri kama Maisha ya Amani na Furaha hasa katika ngazi ya familia mpaka ukoo. Neno VITISHO visikie kwa jirani lakini sio nyumbani kwako, Vitisho husababisha msongo wa mawazo, hupelekea maisha ya kutangatanga, Hupelekea mtu kuuza utu wake, Vitisho husababisha familia ikutenge ili kuokoa nafsi binafsi
Hii hama hama kuna mambo mengi nyuma ya pazia wengine wanasema wananunuliwa kwa pesa lakini kuna siku hawa wanaohama watakuja kusema ukweli Vitisho wanavyopata na walivyopata mpaka kuamua kuhama
Chezea kila kitu kwa mwanadamu sio uhai wake, hakuna spare ya uhai unapoambiwa umepewa week moja uchague uhai au kuunga mkono hoja, utaunga mkono hoja ndio maisha ya mwanadamu
Ukweli utabaki ukweli unaweza ukachelewa lakini utabaki ukweli tusiwalaumu hawa watu wanaohama kuwa wamenunuliwa kuna mengi kwa sasa hawataongea, haya yatapita lakini kuna siku ukweli utaacha watu na mshangao mkubwa,