and 300
JF-Expert Member
- Jun 27, 2012
- 26,325
- 36,257
Vyuo vikuu ulimwenguni ni chanzo cha kuzalisha nguvu kazi ya kuendesha uchumi na maendeleo kwa ujumla sehemu husika na duniani kwa ujumla.
Lakini hapa Tanzania baadhi ya vyuo kwa makusudi wameamua kuja na vigezo "pekee/unique" katika kudahili wanafunzi, kikiwemo chuo kikuu binafsi cha Muslim University of Morogoro
1. Kujumuisha somo la dini katika vigezo vya kufuzu kudahiliwa hapo tofauti na miongozo ya TCU. La kushangaza zaidi wahitimu hawa/walimu hawa wenye ujuzi wa somo la dini wameajiriwa shule za umma.
2. Sifa za kitaaluma za wahadhiri chuoni hapo ni kitu cha kutilia shaka.
Tafadhali TCU mliangalie hili suala kwa jicho la 3 kama kweli mmelenga kuboresha elimu ya vyuo vikuu Tanzania.
** NASISITIZA: Nia ni kujenga wala si kubomoa tafadhali tusichafue hali ya hewa kwa mrengo wa kidini.