ZeMarcopolo
Platinum Member
- May 11, 2008
- 14,279
- 7,685
Wenye virus utawajua kwa upungufu wa sera kichwani.
nilishawahi kusema na narudia....hii vita ya ruge na sugu ni kwa manufaa yao wenyewew!
SUGU NI MAARUFU ZAIDI YA CLOUDS TEAM + REDIO + kiTV. nazani wamekubaliana kusaidia waathirika coz kipato watakao toa ni watu wa mbeya pia sio lazima msanii apate faida wakati wa matatizo ya kijamiii
unaakili nyepesi sana mchumba mbona unaonekana kuingilia makubaliano yao yakuchangia jamiiiiii, umetumwa na ruge nini au huwa unawananihiii
Sasa hapo cha ajabu ni kipi?ulitaka akupe wewe na familia yako?
mwanasiasa, mwanamuziki, mwandishi na mwanaharakati sugu ametangaza rasmi kuwa asilimia 33 ya mapato yote ya tamasha litakalofanywa jijini mbeya na vinega zitatumika kuwasaidia waathirika wa mafuriko hukohuko mbeya.
Mimi, wewe na wengine wote wanajua kuwa mbeya ni strategic area kwa shughuli za kisiasa za sugu. Vilevile sote tulijulishwa kuwa lengo la anti virus movement na vinega ni kuwakomboa wasanii toka kwenye unyonyaji wa "matajiri". Hii ni kumaanisha kuwa wasanii wawekeze kwa kutumia vipaji vyao ili wajikomboe kiuchumi.
Iwapo mgawanyo wa pesa utakuwa kama ulivyotajwa, basi vinega (zaidi ya 20) itabidi wagawane pesa zitakazobaki yaani asilimia 67 toa gharama za investment. Sasa tujiuliye, je huu uwekezaji wa kutoa msaada asilimia 33 ya gross income una tija kwa vinega? Jibu lake ni rahisi, kiuchumi/investment hakuna tija. Kwa vile kiuchumi mgawanyo huo hauna tija, je ni kwanini sugu amesimamia kuhakikisha mgawanyo unakuwa hivyo?
Hapa ndipo tunapokuta kwamba sugu anawatumia vinega kujijengea umaarufu kisiasa. Mkombozi wa kweli wa wasanii wa bongo (iwapo wanadhurumiwa) bado hajapatikana. Sugu is just another mnyonyaji.
Ninawapa ushauri wasanii wote wanaohusika katika vinega kuwa makini na terms za ushirikiano wenu. Msikubali kuyumbishwayumbishwa. Kama kuna haja ya kuchangia maafa basi kila msanii apate pato lake na yeye mwenyewe kwa hiari yake akachangie maafa. Priority yenu number one inapaswa kuwa "kutoka kiuchumi".
Merry christmass...
Kwani haiwezekani kuwa hao vinega wakawa wameamua kujitolea kuwasaidia wahanga?
Show imeenda Mbeya wakati wa maafa so wanawasaidia wenzao, am sure ingekuwa inapigwa Dar now pia wangejitolea kuwachangia wahanga wa mafuriko.
Je Vinega walipotoa wimbo kwa ajili ya wahanga wa Meli ilozama Nungwi pia ilikuwa ni Sugu Na Siasa?
Je wewe kesho utaogopa kumsaidia ndugu yako kidogo kisa unahisi ni umaarufu unatafuta?
Hii inaitwa "giving back to community" rafiki yangu. Utajiri wa hao wasanii unatokana na michango inayopatikana kwenye mauzo ya albums na shows zao, na wateja ni hao wananchi ambao ndio wahanga wenyewe nw kuna ubaya wakirudishiwa japo kidogo wajikwamue na janga kuna ubaya?
Na hiyo ni kama wananchi wa Mbeya wamepata platform ya kuwasaidia wenzao kupitia wawakilishi waaminifu.
Muziki na Maisha ndio hii sasa.
Songa Mbele Sugu, Songa Mbele Vinega.
Nilishazungumza hao vinega wanatumiwa tu na sugu kulipiza kisasi kwa ruge,hao vinega ni kenge waliokwenye msafara wa mamba wawili wenye ugomvi yoo