Nimesoma katika gazeti la Mwananchi leo, nikajikuta nasistushwa sana na kauli ya Mwigulu Nchemba, kwamba watumishi wengi wa umma wanatumia muda mwingi kazini kushabikia siasa hasa vyama vya upinzani badala ya kufanya kazi, na hivyo kukwamisha utekelezaji wa ilani ya CCM. Na anaonya kuwa watumishi wa namna hiyo wajitoe mapema. Najiuliza: Who is Mwigulu Nchemba? Je, watumishi wa umma wote lazima wawe wana-CCM? Waungwana nisaidieni kuhusu kauli hii.
Kumsuta Mwigulu Nchemba kwa kauli yake ni dalili ya kutojua historia au kuwa na mtazamo finyu. WaTz mnajifanya wajanja sana wa kurukia uongo ili kuficha nyongo zenu na tama zenu. Kwa mfano ikifika kwenye kutaka uRais kila mmoja anataka au yeye mwenyewe au kumpa mtu wa kabila lake au dini yake. Kikwete wetu huyu mpaka kampeni zilimwangusha akazirai, Mchaga usipomtajia CHADEMA au Mbowe wewe ni mpumbavu anaacha hata kuongea na wewe. Mwenendo huu umesababisha WaTz kuishia kuwa watu wa kuganga majeraha yanayokana na ajali za kujiandalia wenyewe.
Anayosema Mwigulu Nchemba ni majeraha tu ya ajali ilikwisha kutokea baada ya Ali Hassan Mwinyi kungoa usukani wa gari lenu na nyie mkampa Mkapa na Kikwete waliendeshe hivyo hivyo. Lazima liende mrama na kutumbukia mikenge na sasa wote mmo ndani ya mkenge mnamlaumu Mwigulu Nchemba kuwa ndiyo kawatokea huko.
Bwana Mkubwa Ali Hassan Mwinyi alikuwa na mahangaiko mengi sana ndani ya Ikulu, moja wapo kuwepo vyama vingi au kuendelea na chama kimoja. Tuakaambiwa kuwa kulipigwa kura ya maoni lakini WaTz wote mkataka kibaki chama kimoja, CCM. Lakini Mheshimiwa sana Mwinyi (alisema) kwa kujali kuwepo kwa demokrasia na kwa kulingana na upepo wa mageuzi uliokuwa ukivuma dunia nzima akaamua (kinyume na kura yenu ya maoni?) kuanziasha mfumo wa vyama vingi. Akaalika watu wenye uwezo wa kifedha kuanzisha vyama vyao ili vishindane na CCM. Hivyo CCM ikiwa imetokea TANU na ikiwa na miaka karibu hamsini mpaka leo bado mnashindana nayo.
Kwenye siasa angalia tu jengo la UVCCM barabara ya Morogoro utaelewa Usalama wa Taifa Wanatengenezwa hapo hapo na viongozi wanaorithi uongozi wa kulinda viongozi walioko madarakani wanatoka hapo hapo. Kwenye ajira ni juzi tu mmekelele watoto wa vigogo Benki Kuu mpaka mkawataja kwa majina, hamjauliza katika mawizara kuna watoto wa akina nani. Mimi binafsi nimebughudhiwa sana na watoto ndani ya Wizara baada ya kuajiriwa na Mama zao. Watoto hawa walikuja kunivuruga kwa kutumwa na mama zao majumbani. Na vurugu katika mawizara ni pamoja na kuchaniana barua na hata kupotezeana majalada mazima. Unaandikiwa barua ya kuitwa kwenye interview mtoto wa jirani anaificha wewe bila kujua hata kama uliandikiwa barua hiyo.
CHADEMA wamebahatika kidogo kuwa na wezi waliokwishaunda umoja wa kujihami mapema. Ukiambiwa Wachaga wanakwenda Xmas kuhesabiwa amini ni kweli kwa sababu si kuhesabiwa tu bali zamani walikuwa wakienda kuunda mikakati ya kuchukua shule zote na ofisi zote , sasa wana mikakati ya kuchukua nchi. CCM inaliona hili kama CCM na wanaCCM Wachaga (ambao bado wana kimfupa cha kuguguna) wanapambana na CHADEMA huku wakijiandaa mara watakapobaini kimfupa hakiana hata juisi ndani yake wanahamia CHADEMA.
Makundi haya ni ya kijasusi na vita ni vya kijasusi kwa hata kufikia viwango vya kurogana na kulishana sumu. Hivyo badala ya kuvunja ukabila, udini na makundi Mwinyi aliimarisha kundi moja la wahuni (CCM) na kukaribisha kuundwe makundi mengine ya wahuni kupambana na CCM. Niwie radhi kuita wahuni kwa sababu makundi haya ndiyo yanazalisha wizi, ufisadi, ukabila na udini. Linalobishaniwa sasa ni matokeo tu tarajiwa kwa sababu Mwigulu Nchemba anasemea kundi lake, na anayemsuta naye anahoji kwa nini kundi lake Mwigulu Nchemba halitambui? Kwa hiyo Mwinyi amewatengenezea mzunguko unaitwa "viscious circle".