Siasa za Lowassa, Sumaye na Membe - upinzani

Siasa za Lowassa, Sumaye na Membe - upinzani

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,776
Reaction score
46,050
Ninaandika uzi huu kuangazia siasa za Tanzania kuwazungukia wazee hawa:

Lowassa, Sumaye na Membe.

Ni wazi kuwa panapokuwa na ukweli, uchungu huwa ni sehemu ya maisha.

Kwamba ujio wa Lowassa au Sumaye ulikuwa ni mkakati wa CCM kuuwa upinzani? Thubutu! Si mdadisi makini tokea CCM wala upinzani anayeweza kuwa na ujasiri wa kuyasema hayo faraghani (yaani wakiwa wenyewe kwa wenyewe).

Hadithi hiyo ya kuwa walikuja kwa nia ya kuvuruga mbona ni janja ya nyani tu kuitoa hadharani yaani "meant for public consumption?" Si jiwe, pole pole, Mbowe, Lema, Slaa, Lipumba nk anaweza sema hayo indoors.

Siyo siri kuwa ujio wa wazee hawa upinzani ulikuwa unakwenda kuigharimu CCM Dola waziwazi. Laiti kama kuwekwa kwa maslahi ya taifa mbele dhidi ya maslahi binafsi kungekuwa kumetamalaki vilivyo (kunako upinzani) angalau kwa hawa mabwana: Dr. Slaa na Prof. Lipumba, kwa hakika 2015 jiwe na CCM wangeisoma namba.

Kwamba 2015 upinzani ulishindwa? Hiyo itakuwa ni kuukimbia ukweli. 2015 upinzani ulipata kura nyingi na majimbo zaidi kuliko wakati wowote ule. Laiti wangali kuwa na subira kidogo tu walikuwa wachukue nchi.

Kubeza mchango wa wazee hawa kwa mafanikio ya 2015 itakuwa ni kujaribu kuukimbia ukweli wa wazi mithili ya mtu kukikimbia kivuli chake mwenyewe.

Upinzani unapaswa kujilaumu kwa kutoweka mazingira wezeshi na hasa kutowekeza katika kupambana na ubinafsi. Kutokuwapo kwa mazingira wezeshi kupambana na ubinafsi kutaendelea kuugharimu upinzani kwa hasara yao na manufaa kwa CCM hadi upofu huu utakapofahamika bayana.

Bila ya ubinafsi, miungano thabiti dhidi ya CCM ingalikuwapo katika chaguzi zingine zilizowahi kuwapo.

Kwa hakika kama huko Kenya, Malawi, Zambia nk vyama hivi vya ukombozi vingeendelea kuwapo madarakani peke yao miaka nenda rudi, bila ya kuungana.

Kwamba upinzani umeshindwa kujizatiti kuepusha mitafaruku inayopelekea wanachama wao kuondoka? Kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi upinzani wenyewe hauwezi kukwepa lawama kwenye hilo.

Kwamba yalitokea? Yaliyopita mbona si ndwele? Ni wazi kuwa si Sumaye, Lowassa, Slaa, Lipumba nk wangeandoka kwa namna ile kama jitihada za kuziba nyufa vilivyo zingekuwapo. Kukiri upungufu ni kitendo cha maendeleo.

Consolidation ya waliopo na wanaokuja kutoondoka, kutambua kinachopatikana hata kama ni kidogo nk ni uelekeo mzuri. Roma haikujengwa siku moja.

Kama ilivyokuwa kwa hao wengine, ujio wa Membe upinzani hauwezi kuwa na maslahi yoyote kwa CCM kwa lolote. Hasa hasa kama upinzani watautumia vyema na kuweka maslahi binafsi pembeni.

Kwamba kina Lowassa, Sumaye na leo Membe ati kuwa wametumwa kuvuruga upinzani na wasemao hivyo ni akina Pole pole na ndugu zao? Huruma hiyo na dua njema hizo kwa upinzani wameanza lini kuwa nazo? Ni mafanikio makubwa kwao kutusikia tunaicheza ngoma yao hiyo kwa niaba yao.

Alipenda kusema Rev. Mtikila (rip), "saa ya ukombozi ni sasa!"
 
Ukweli hauwezi kuwa mtamu.

Umoja ni nguvu combination ya wote wakiwamo kina Lissu, Membe, Maalim Seif, Zitto, na wote ambao hawawezi kuwapigia wao kura wanahitajika mno kwenye huu mchakato.

Walipotea walioondoka, wasipotee wengine.

Tupige vita maslahi binafsi. Tuweke maslahi ya taifa mbele.

Membe yuko right - kijani wanapigika.
 
Back
Top Bottom