''siasa za leo na falsafa ya uhitaji wa rika''

Nyakarungu

JF-Expert Member
May 1, 2011
472
375
''SIASA ZA LEO NA FALSAFA YA UHITAJI WA RIKA''

  • [h=5]
    Napotazama mihemko ya kisiasa kwa vijana kushabikia siasa/wanasiasa kipindi hiki!
    Nakumbuka falsafa ya ''UHITAJI WA RIKA'' niliyoibuni mwaka 2012 na kuiweka kwenye kurasa za KITABU CHANGU kiitwacho ''UTASHI NI MTU''......falsafa inasema ''kuna wakati rika fulani huibuka na mihemko inayofanana kwa muda wa wakati wao kushabikia au kuiga na kufanya kitu/jambo fulani linalofanana, lakini rika la wakati wao likipita kila kitu hupita kisha huja rika jipya na mihemko yao mipya juu ya kitu kipya.
    Karibia 60% ya rika lao hushabikia kitu cha aina moja, rika hili nalo hupita na huja rika jipya lenye mihemko ya uhitaji wake pia.
    Ukomo wa rika huja tu pale tabia zenye kufanana miongoni mwa rika hilo huanza kuhama na kila mmoja kufuata njia yake kimawazo na kifikra, hakuna ukomo wa umri katika tabia za uhitaji wa rika''.
    By Grayson M Nyakarungu UTASHI NI MTU (2013)..........''

    Nijadili falsafa yangu kwa mifano hai,
    Tukumbuke miaka ya 1998 -2006 enzi la Kuibuka kwa makundi ya Muziki wa kizazi kipya hapa Tanzania kundi kama vile:-
    KWANZA UNIT, SAREHE JABIR(Solo Artist na mwanzilishi wa rap ya kiswahili), TWO PROUD (kwa sasa Sugu aliyeufanya muziki huu kupiga hatua ya kuanza kuuzwa), WATEULE,WABABE CRAK, GORILA KILLERS, HBC(Nigga Jay,Terry Fanani na , kundi la DIPLOMAT (saigoni na wenzake) n.k,
    Nimetaja makundi na wasanii wa muda mrefu kidogo waliokuwa na dhamira kubwa ya wazi ya kuona Muziki wa kizazi kipya Tanzania unakuwa imara na wenye tija, baadae kizazi kile cha muziki uliokuwa wa dhamira ya kutengenza mfumo wa muziki kilipita kikaibuka kizazi cha rika la wasanii wa upepo wanaoenda na matukio walioamini si muda wa kuimba matatizo ya jamii bali ni muda wa kuburudika tu na watu wasahau shida zao kwa muda, miaka hii tunakumbuka kulikuwa na mihemko ya vijana wakiibuka na kufanya muziki wa kizazi kipya (kwa sasa bongo fleva).
    Kila mkoa, kila wilaya, kila kata, kijiji na pengine karibia kila kaya usingekosa mtu anaejiita msanii, anaesuka nywele bila kujali jinsia yake, anaevaa jeans kwa mtindo wa KK, anaetembea amekunja bega moja na hata waliovuta bangi sio kwa sababu ya asili yao bali kwa sababu ya mihemko ya kudhania kuwa kuwa msanii lazima uvute bangi.

    Bongo fleva iliwatoa wengi kimaisha, kiumaarufu, hata kimaslahi mengine waliyoyajua wenyewe, mradi tu iliwatoa.
    Wakati ule kila msanii aliyetoa single redioni tulitarajia na baadae tukashuhudia tamasha kubwa la uzinduzi wa album yake, kwa wengi kipindi kile walipoingiza sokoni album waliuza sana, kipindi hicho walisambaziwa na kampuni moja tu ya wahindi (GMC) iliyoko kariakoo inamilikiwa na MMAMU,

    Waliuza sana tapes (kanda) na walitoka kwa kweli, na wengi wao mie nilishiriki harakati zao kimuziki ikiwa ni pamoja na kutengeza beats zao katika studio kadhaa hapo bongo miaka ya 2003 -2005 na wengine kutumia mashairi yangu niliyowapa kwa hiyo nawafahamu na ninaujua muziki wa bongo vilivyo.

    Lakini kizazi cha rika kipoondoka hatukuona tena kitu kinaitwa uzinduzi wa album pale Diamond jublee wala club billcans, wala tour za mikoani za kutangza album hazipo tena, mbaya zaidi hata tapes hazikuzalishwa tena ukiachilia kutonunuliwa kwake,
    Hii ni dhahiri kuwa wafanyabiashara walisoma alama za nyakati kuwa rika lao la biashara halipo tena, hata Mr Nice aliwahi kukiri kuwa nyimbo za TAKEU hazina soko tena kwa sababu waliokuwa wakizipenda ni watoto wa enzi zile na sasa wameshakuwa watu wazima na haoni umuhimu wa kuimba tena nyimbo hizo kwani hazina soko.

    Kilichobaki kwenye huu mziki ni wasanii tu lakini sio wale mashabiki wala wateja wa awali, hivi sasa wasanii kwa kujua kuwa hakuna wateja nao hawana mpango wa kuuza kazi zao bali wanauza show tu, ''nipe pesa nipande jukwaani niimbe, acha watu wakopi nyimbo zangu kwenye flash disc zao wasikilize popote ili wawe oriented na nyimbo zangu nipate show''.

    Katika siasa za sasa za dunia yote wala sio Tanzania tu, mihemko hii ya uhitaji wa rika imetia fora.
    Napenda kuwaomba vijana watambue kuwa kwenye hii mihemko ya uhitaji wa rika ni mizuri endapo tutaitumia vizuri, tukadumu nayo kwa ari tuliyonayo kwa mwelekeo wenye dira na ndoto sahihi kwa Taifa letu.
    Wakati ule wa Bongo sanaa, niliwahi kushudia mashindano ya mfalme wa rymes, wakati Afande Sele the King (moja ya wasanii wanaotumia akili sana kuandika mashairi na kuufanya muziki wao kutokushaka thamani) wa MOROGORO aliibuka kidedea.
    Wakati ule kila kijana alikua akishabikia msanii anaempenda, ilifikia hatua wasanii wakawa na ugomvi baina yao na kuwafanya mashabiki wawe na ugomvi wa kiushabiki kama wale wanaowashabikia.

    Kadhalika kwenye siasa hivi sasa hakuna tofauti na wakati ule vijana wanadhani siasa ni burudani kama ilivyokuwa sanaa.
    Siasa ni mfumo wa kutengenza mbele ya Taifa, tutofautiane kifikra, kimtazamo na kiitikadi lakini tusitofautiane kwenye lengo kuu (kutengenza Taifa imara).
    ''Uwe na malengo yako, yenye utofauti na ya mwingine, lakini yote yalenge kutimiza lengo kuu - ''UTASHI NI MTU'' Ukurasa wa 44.

    Wapo wasiojua tofauti ya vyama vya siasa na Taifa au Serikali, hawa wapo tayari hata kupinga Jakaya Kikwete kuitwa Rais, wapo pia wanaodhani tofauti ya itikadi ndio tofauti ya malengo makuu ya siasa za nchi (wanahitaji shule)
    Wapo wanaodhani kuibadili nchi kimfumo wa utawala ni kuondoa chama tawala na kuweka kingine bila transformation ya fikra na mfumo wa utawala ndani ya jamii na ndani ya vichwa vya watu wanaojiita/wanaojidhania ni viongozi, (hapa shule kubwa sana inahitajika, lakini tukienda kwa lengo la kuitoa ccm tu madarakani kwa aproach ya now and then,tukidhania kuwa lengo letu namba moja ni kuitoa ccm madarakani bila kujali jamii haina wala haijajua tofauti ya taifa na vyama vya siasa, bila jamii kubadilishwa kimtazamo na kiwajibu, bila mifumo ya kiuongozi kubadilishwa, kesho ataibuka mwingine na kuwahadaa kwa style hiyo hiyo na tutajikuta tunajipeleka shimoni)
    Mwisho wa yote tunajikuta tumekusanya watazama show na wacheza show kwenye makundi ya siasa.
    Watazama show wakikosa ladha ya burudani waliyotarajia huondoka bila kujali wamelipia kiingilio getini, huamua kurudi kulala wakitajia kuota ndoto zenye kuwatia moyo, kuliko faraja waliyoitegemea na kuikosa kwenye show,

    Wacheza show wao ni wabaya sana, maana wao hucheza sambamba na msanii anapoimba jukwaani, msanii hujikuta akiendeshwa na wacheza show walio kwenye dancing flow ambao hata hakufanya mazoezi ya show pamoja nao, wacheza show huamua hata kumlazimisha msanii aimbe wimbo fulani ambao hata hakujiandaa nao, (Mtakumbuka 2006 Shaggy alipokuja diamondo jublee kilichotokea)
    Hawa maDisco Bugerz wakikosa kuheshimiwa na msanii kwa kile wakitakacho huamua kupiga fujo na hata kumrushia chupa au matusi...

    Mifumo ya kiutawala ni lengo namba moja, kubadilisha mifumo inayosababisha wizi wa mali za umma, mianya inayosababisha rushwa, mianya inayosababisha uonevu n.k
    Sio kuahidi kuwafunga watu au kuwachukulia hatua wenye tuhuma za wizi huku mifumo ikibaki vilevile, je uhakika wa kupata watu waaminifu kwenye mifumo iliyowapa watangulizi wako mianya ya wizi uko wapi?
    Huwezi kuamini katika mabadiliko ya mtu pasipo mfumo kubadilika kwanza, tunatamani kuona viongozi wanaodhani wanaweza kuwa mbadala wa hawa waiopo wakijipambanua kwa mifano halisi ya nafasi zao walizo nazo katika taasisi zao kwanza.
    Mjue kwa sasa watazama show ni wengi kuliko wacheza show, hawa watzama show huwa makini sana na endapo utaenda nje ya key watajua na hawatapiga kelele, ukirudia tena watajiuliza..je ni makusudi au kajisahau, au katuona tumekuja humu kumshangaa yeye na sio show?
    Wakianza kujiuliza maswali hayo uwezekano wa kuondoka bila kujali muda wao waliopoteza kwako ni mkubwa mno.
    Wacheza show wao watakuzomea na pengine usipojirekebisha watakupiga na kukuabisha.

    Siasa haiko hivyo bali tunasimama leo kwa ajili ya kesho, na sio kusimama mchana wa leo kwa ajili ya jioni ya leo, Mobb politics huvuma kwa wakati wa rika na huisha rika linapokwisha.....!!

    NATAMANI RIKA LA UHITAJI HILI LITAKAPOPITA TUBAKI KWA LENGO MOJA KUU NALO NI KUJADILI NA KUPANGA KWA AJILITAIFA LETU.


    [/h]

 
  • Mifumo ya kiutawala ni lengo namba moja, kubadilisha mifumo inayosababisha wizi wa mali za umma, mianya inayosababisha rushwa, mianya inayosababisha uonevu n.k
    Sio kuahidi kuwafunga watu au kuwachukulia hatua wenye tuhuma za wizi huku mifumo ikibaki vilevile, je uhakika wa kupata watu waaminifu kwenye mifumo iliyowapa watangulizi wako mianya ya wizi uko wapi
 
  • Mifumo ya kiutawala ni lengo namba moja, kubadilisha mifumo inayosababisha wizi wa mali za umma, mianya inayosababisha rushwa, mianya inayosababisha uonevu n.k
    Sio kuahidi kuwafunga watu au kuwachukulia hatua wenye tuhuma za wizi huku mifumo ikibaki vilevile, je uhakika wa kupata watu waaminifu kwenye mifumo iliyowapa watangulizi wako mianya ya wizi uko wapi?
    Huwezi kuamini katika mabadiliko ya mtu pasipo mfumo kubadilika kwanza, tunatamani kuona viongozi wanaodhani wanaweza kuwa mbadala wa hawa waiopo wakijipambanua kwa mifano halisi ya nafasi zao walizo nazo katika taasisi zao kwan
    za.



nitakuja kutoa mchango wangu baadae,,,ila kwasasa nimevutiwa na kipengere hicho,,,,nafikiri hapa ndipo tunapoona umuhimu wa katiba kuweka malengo ya taifa kiuchumi, kisiasa, kitamaduni na kijamii,,,lakini pia katiba kuweka mifumo ya uwazi na uwajibikaji,,lakini kubwa katiba kupewa uwezo wa kutochezewa na kuguswaguswa na wanasiasa,,,yaan,,si kila wanavyojisikia basi wabadalishe baadhi ya vipengere kwaajili ya maslahi yao.....

swali,,hicho kitabu wakizindua lini????
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom