Siasa za Kunguru zinakarahisha mno!

Siasa za Kunguru zinakarahisha mno!

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,323
Reaction score
79,954
SIASA ZA KUNGURU ZINAKARAHISHA MNO!

Anaandika, Robert Heriel.

Inaelezwa kwamba kiumbe wa pili kujiingiza kwenye Siasa baada ya Nyoka alikuwa Kunguru. Na inatajwa kuwa ili uwe mbobevu katika Siasa lazima uzimudu mbinu za viumbe hao. Sijamtaja Panya na Siasa zake za kung'ata na kupuliza, Leo nitatumia muda wangu mdogo kuelezea Siasa za Kunguru katika harakati zake Duniani.

Kunguru ni jamii ya mwewe aishiye nyumbani kwenye makazi ya watu. Sijajua lini tabia hiyo aliianza lakini nakumbuka kuna mtu mmoja niliwahi msikia akisema kuwa sababu ya Kunguru kukimbia porini na kujiunga na maisha ya mwanadamu ni tabia Yake ya kujifanya Njiwa. Ati Kunguru Naye alivutiwa na tabia ya Njiwa ya upole, na upendo WA dhati achilia mbali Usafi.

Huo ndio ulikuwa mwanzo wa Siasa za Kunguru katika maisha ya mwanadamu, sifa moja ya Kunguru ni ujanja, unafiki na ulafi uliopitiliza.

Taikon nikaambiwa kuwa hata kwenye misahafu kuna mahala Kunguru ametajwa na Siasa zake. Nikafungua Biblia kuona jinsi kiumbe huyu afanyavyo Siasa zake. Huko nikaona kuwa ati, kulikuwa na harakati za kipekee za kukiokoa kizazi cha Utu wa binadamu ambacho kilisalia kwenye Safina.

Nikamsoma Mtu mmoja aitwaye Nuhu, huyu jamaa baada ya Gharika kukoma alitaka kuwatoa viumbe wote ndani ya Safina, lakini ni wazi wasingetoka wote bila ya kumtuma kiumbe mmoja akapeleleza hali ya uko nje Kama ni shwari au bado ni Shari.

Nuhu Kama Mtawala katika Siasa zake, akafikiri wakumtuma ni Nani, ili utumwe nje kupeleleza itakupasa uwe na sifa Fulani za Kisiasa, ambazo ni Ujanja, werevu, Upendo, na uaminifu.

Akamchagua Kunguru!!! Ndio ni Kunguru huyuhuyu unayemuona akiruka Hapo nje akiiba vitu na kuwapokonya watoto wako chapati au kalmati.

Nilisema CV ya Kunguru miaka hiyo ilikuwa ni Safi, alipokuja kwenye maisha ya mwanadamu alijitambulisha Kama kiumbe mwenye sifa za njiwa, ati alijita PACHA WA NJIWA, hahaha! Kunguru bhana!
Licha ya kuwa yeye ni mweusi tii Kama mkaa lakini hakuona haya kujifananisha na Njiwa.

Kama sitasahau, sifa nyingine ya Kunguru kwenye Siasa ni kutokuwa na Aibu wala Haya, anaweza kuongea uongo macho yake yakiwa makavu Kabisa. Huyo ndio Kunguru.

Lakini tabia zake mbofu mbofu, ndio ni mbovu alizificha hivyo Nuhu hakuweza kuzitambua. Alitumia kiherehere chake na kujipendekeza mpaka alipoubwaga moyo wa Nuhu.
Siasa za Kunguru ni za kujipendekeza na ukiherehere mpaka wenye nguvu wamuamini kabla hajawageuka na kuwapiga Mlio.

Nilisema sitaandika Sana, Acha nimalize,

Kunguru akaaminiwa Kati ya viumbe wengine, wote wakamtumainia, sasa jina la Kunguru likawa kubwa Kati Yao mule Safinani, Nani ambaye hakumjua Kunguru, ikiwa wote walichoshwa na kukaa mule ndani, gharika na machafuko yalikuwa yamekoma sasa Safina haiwafai tena isipokuwa imegeuka Gereza la hiyari. Anyway!

Kunguru akatanua mbawa zake, kisha akazipiga na kuranda randa mule ndani ya safina kutafuta tension/Kiki ili kila aliyeko ndani anyone, kisha akatoka shaap! Nje!

Kunguru anasiasa za Kiki, hupenda akifanya Jambo kila mtu alione na Ajue, sio ajabu ukiwa ndani ukamsikia Kunguru wakipiga piga kelele nje huko au kusumbua sumbua, hii ni tofauti na Njiwa, ambaye ni mtulivu na mpole asiye na makuu!

Kunguru huko alipofika hakuona pakutua, bado maji yalikuwa yamefurika usoni pa nchi hata pasionekane pakutua. Kunguru akarudi, akiwa anasubiriwa Kwa hamu zote.

Akawaambia hakuna mahala pakutua. Tusubiri Kama siku kadhaa hivi! Zilipopita hizo siku kadhaa, Kunguru akawaambia akiwa Kama mtaalam sasa, ngoja niende tena, Nuhu na waliomo wakamruhusu.

Akaondoka, siku ya kwanza hakurudi, yapili, yatatu, yanne, ya Saba wakasema Eeeh! Yakhee! Huyu mwenzetu kipi kimempata mbona harudi?

Nuhu akamtuma Njiwa, huyu Siasa zake ni zakiadilifu, mwaminifu asiye na makuu. Akatoka huku waliomo safinani wakiwa na hofu na wakimsihi asije akatokomea Kama Kunguru. Njiwa akawaahidi kuwa atarudi. Akaondoka akiwaachia tumaini la kuondoka kwenye jela ya hiyari ambayo ni jukumu Lao ima kubaki au kutoka ndani yake.

Njiwa huko nje akakutana na Kunguru akila minofu ya Vibudu(wanyama waliokufa Kwa gharika) taikon akili yangu inaniambia kuwa Njiwa alimkuta Kunguru akiwa amenona kutokana na Kula mizoga, hivyo ndivyo Siasa za Kunguru akipewa nafasi, hata hivi leo unakakuta kamwanasiasa kipindi kanaomba uongozi kalikuwa kamedhoofu Kama Taikon lakini siku kakipewa tuu uongozi utashangaa tambi Hilo, ubonge huo, ni kawaida ya walafi kwani ni tabia ya Kunguru.

Kunguru akamuambia Njiwa, Usirudi huko, kaa nami huku ule unenepe na kunawiri Kama Mimi. Njiwa akakataa, basi ukawa ugomvi mkubwa Sana. Naambiwa Kunguru alitaka kumuua Njiwa ili asirudishe ujumbe Kwa waliomo safinani ili waendelee kukaa gereza la hiyari. Lakini Njiwa alijihami na kutoroka.

Taikon akili yangu inaniambia sababu ya Kunguru kutaka kumuua Njiwa ni kuhofia kuwa atapeleka taarifa Kwa waliomo safinani kuwa Kunguru kawa Msaliti na amemkuta akila Mema ya nchi mwenyewe.

Hata sasa wanasiasa wenye tabia za Kunguru ukitaka watake kukuua jifanye unatoa taarifa zao Kwa Waliomo Jela ya hiyari kuwa wao wanatafuna Nchi. Anyway! Tuendelee

Njiwa akarudi jioni akiwa kabeba Jani, lakini akawaambia kuwa maji yamekauka lakini bado nchi inatope jingi Sana, ardhi bado ni tepetepe hivyo wasubiri Kwa siku kadhaa.

Wakafurahia Sana.
Siku kadhaa alizosema Njiwa zikapita, Nuhu akamwambia Njiwa, sio wewe uliosema siku kadhaa tuzisubiri zipite! Tazama zimepita, ondoka ukaiangalie nchi.

Njiwa akatii lakini akiwa dirishani ili atoke akasema, Kama nisiporudi mjue nchi imekauka, na nikirudi mjue bado tunahitaji subira,
Nuhu akamuuliza Njiwa, je tusubiri Kwa siku ngapi ili tujue kuwa hautarudi au utarudi. Njiwa akajibu zikipita siku tatu Kama sijarudi basi tujueni mambo ni Shwari. Wakaagana.

Zikapita siku tatu njiwa hajatokea, nuhu akaona awatoe watu Safinani ambalo liligeuka Gereza la hiyari.

Njiwa Siasa zake ni kuwa ataleta taarifa endapo utamtuma. Ni muaminifu, na huleta taarifa za matumaini.

Lakini Kunguru Siasa zake, ukimuona amerudi ujue huko nje hapajakauka, ujue anashida ndio maana karudi mbele zako, lakini kama Hana shida kamwe huwezi kumuona.

Hii ipo katika Siasa za nchi yetu, wanasiasa wenye Siasa za Kunguru huwezi waona wakati nje pamekauka wakati usio wa kampeni, lakini nje pakiwa pamefurika maji wasipate pakukanyaga ambapo ni wakati WA kuomba Kura hujikuta wakirudi kujifanya wanakuja kutoa taarifa kuwa huko nje hakuna pakutua, muwatume mara nyingine wakaangalie Kama maji yamekauka au Lah!

Kunguru wewe Kunguru!
Kwa nini Watowesha Uhuru!
Umezima taa watu sipate Nuru!
Kazi yako Kula na kufaidi Ushuru!
Wanaokusema wasema Wanakukufuru!
Wawaka sweka na kuwarusha kwenye Tanuru!
Kunguru wee Kunguru!

Taikon anawaambia kila siku Kunguru sio Njiwa, siku hizo ugomvi wa Kunguru ukakua na mpaka leo Hawaivi, Kunguru akachonga Fitina kisha akaisambaza sumu mbaya Kwa jamii ya mwewe, kipanga na Tai ambayo ndio jamii yake ili wamchukie Njiwa, fitna yake ikafanikiwa, njiwa akawa adui wa wahuni hao.

Akaona haitoshi, Kunguru akamchongea Njiwa Kwa Nyoka Kwa Aina zake, mpaka hivi leo nyoka na Njiwa ni maadui.

Siasa za nyoka
Siasa za Kunguru
Siasa za panya Buku!

Nipumzike sasa!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Binafsi naona chanzo cha siasa za kunguru kwenye siasa zetu kwa kiasi kikubwa zinachangiwa na jamii tuliyotoka, kama mwanasiasa ametoka kwenye familia masikini akaingia siasani kwa kigezo cha "kuwatumikia" wananchi, huyu hawezi kukosa tabia za kunguru.

Siasa baadae itageuzwa kuwa ajira na bahati mbaya au nzuri kwasababu ina maslahi mazuri, basi inakuwa msaada mkubwa wa kukidhi mahitaji ya wategemezi waliomzunguka huyu "kunguru"

Sasa tufanyeje ili tutoke hapo, kwanza lazima pawepo na ajira za kutosha, ili hawa "kunguru" wetu wasijikute wana mzigo mzito wa kuubeba kwa jamii waliyotoka, hili likiwezekana, hawa "kunguru" watabadilika na kuwa viumbe wengine wenye kukisimamia wanachokiamini mpaka mwisho bila kutetereka.
 
Binafsi naona chanzo cha siasa za kunguru kwenye siasa zetu kwa kiasi kikubwa zinachangiwa na jamii tuliyotoka, kama mwanasiasa ametoka kwenye familia masikini akaingia siasani kwa kigezo cha "kuwatumikia" wananchi, huyu hawezi kukosa tabia za kunguru...
Umeongea Hoja nzuri.

Lakini Kunguru falsafa Yao inayowaongoza ni Kula mizoga, yaani lazima wengi wafe na wataabike Ile Kunguru apate mlo!

Kunguru hapendelei mlo kutoka windo lenye damu mbichi. Anasema sio chakula kitamu
 
Wewe upo kundi lipi kati ya hayo?? Usijekuwa kundi uliloliita la "wapumbavu na walalamishi".
 
Back
Top Bottom