Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tanzania Pharmaceutical Industries (TPI) Ltd, Ramadhani Madabida, amepandishwa kizimbani akidaiwa kusambaza dawa bandia za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi (ARV). Ramadhan Madabida, Ofisa mtendaji TPI Madabida na wenzake watano, wakiwemo watumishi wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD), walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.Mmiliki huyo wa TPI, ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam na wenzake wanadaiwa kuisababishia MSD hasara ya sh. milioni 148.Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi...