Siasa za Bongo nizakukomoana zisizo na manufaa kwa taifa.

singojr

JF-Expert Member
Oct 28, 2014
5,308
6,884
Ukiangalia trend ya siasa za Bongo ni kuchomana ili flani aonekane mbaya hafanyi kazi atumbuliwe watu wafurahi ilhali hata tatizo la msingi halijatatuliwa.
Watanzania wengi wanafurahia kutumbuliwa kwa watu kuliko mabadiliko yatakayoletwa kwa kutumbuliwa kwa watu husika.
Vyama vya upinzani ni kama havina agenda ya msingi kazi ni kutafuta nani tumsagie kunguni tutafute matatizo kwenye eneo lake( watu sio malaika lazima watapata) then tumchomeshe, tushikilie bango mpaka apigwe chini, tushangilie kutumbuliwa kwake halafu tuhamie kwa mwingine.
Kashikiwa bango January Makamba na Maharage Chande kila kitu alionekana wamekula hela kila walichosema kilinukuliwa kuwa uongo kabadilishwa wizara mwenzake kabidilishwa Taasis, umeme bado si unakatika kuliko hata mwanzo? Tatizo lilikuwa January Makamba na Maharage?
Sasa hivi wamekuja na gia ya Ummy Mwalimu, kifo chochote cha wajawazito anabebeshwa yeye kana kwamba ndo yupo labor. Lakini hivi vifo si vipo miaka na miaka tena kwa sasa jitihada zimefanyika vimepungua. Bango ni kubwa kwamba atumbuliwe lakini je tatizo ni yeye au tutashangilia akitumbuliwa halafu tutasahau kwamba vifo vinaendelea na kuhamia kwa mwiingine?
 
Back
Top Bottom