Siasa VS Uchumi: Sakata la Bandari zetu

Siasa VS Uchumi: Sakata la Bandari zetu

Sasa kwa wewe ambaye unajiona ni mchambuzi wa uchumi, una tija gani kwenye hii nchi kupitia huo uchumi wako? Mbona miaka zaidi ya 60 sasa nchi bado ni masikini?

Au usomi wenu nyinyi ni wa kujitutumua tu kama wa ndugu yenu mwigulu! Watu wanataka ufafanuzi. Kwq sababu wamechoka kuendelea kuona watawala wakiliingizia Taifa hasara kupitia mikataba ya kimangungo.
Masikini ukicompare na nani? Tanzania ni kati ya nchi 10 Tajiri Afrika yetu hii. Umetembea nje Tanzania au unasikiliza Porojo za Malisa?
Ukabila + Ukanda + Udini utawaua nyie.
 
Kwa watu wanaotazama Uchumi zaidi, tunaona ni Bora shughuli za uendeshaji wa Bandari ziwe kwa kampuni binafsi huku Serikali ikihusika na ukusanyaji wa mapato tu, na uendeshaji wa gati za mafuta nk.
Sijajua wewe unanena haya ukiwa mlengo upi?
Mipango mingi liyopangwa chini ya mzee wa Msoga haijawahi kuwa ya maslah ya Taifa, nina mfano mingi tuuuuuu:
1 DEGE eco village --- huu ulikuwa upigaji uliokithiri kwa kuwa walisahau hata kunawa mikono. Sasa mradi haufai hata kufugia njiwa.
2. Daraja la Kigamboni ------- utakubaliana na mi kuwa hii ni white elephant na sasa ndipo wavhimnguzi wa mambo wanabaini kuwa daraja ni kipingamizi cha uendelezaji wa bandari:
3. Nyumba za makazi ya wanajeshi--------- uliza taarifa jinsi hizo nyumba zilivyo sub standard na zisizofaa kwa makazi.

Vipi usakama wetu tunampompa mwarabu kuwa msimaamizi wa lango kuu la kuingia nchini?
 
-Je vipi mkataba na Sheria zake umejikita kutetea rasilimali za nchi yetu?
Mkataba umejikita zaidi katika kuhakikisha kuwa Familia ile maaarufu na hodari kwa kuanzisha miradi ya upigaji inapata fedha kwa ajili ya kugharamia uchaguzi 2025 na kuhakikisha kuwa familia inaendelea kutawala nchi
 
Ni dhahiri wa shahiri kuwa watanzania wengi hawana uelewa wa mambo mengi, na kwamba wako tayari kuchukua upande mmoja pindi itokeapo hoja yoyote ya nchi, haijalishi ina maslahi au haina maslahi kwa Taifa letu.

Suala la Bandari, limekuwa hyped sana kwa siku 2 hizi, upande mmoja ukisema Bandari inauzwa, na upande mwingine wanapinga kuwa hakuna makubaliano hayo.

Watu wengi hapa wamejigawa kichama yaani CHADEMA VS CCM na sio kujenga hoja kwa mustakabali wa nchi na kuujua ukweli wenyewe wa mkataba, sambamba na faida na hasara zake.

CHADEMA wameichukua hii hoja kisiasa zaidi, na wakiamini watagain kwenye siasa, wakati CCM wameichukua hii hoja kiuchumi zaidi na hawana uhakika wa kugain kisiasa.

Matamko karibu yote yanalenga zaidi kujikuza kisiasa zaidi ya kiuchumi.

Kwa watu wanaotazama Uchumi zaidi, tunaona ni Bora shughuli za uendeshaji wa Bandari ziwe kwa kampuni binafsi huku Serikali ikihusika na ukusanyaji wa mapato tu, na uendeshaji wa gati za mafuta nk.

Tumekuwa tukilalamika hapa, Bandari haina ufanisi, ukiagiza gari hadi kulipata ni shida, makontena yanakaa hadi mwezi pale Bandarini, lkn wizi uliokithiri kwa wafanyakazi wasio waaminifu, hali hii imepelekea Bandari kuwa na ufanisi mdogo zaidi licha ya uwekezaji mkubwa unaofanywa.

Kwanini naona watu wanachanganya SIASA na UCHUMI? Wengi wanaotoa matamko hawana elimu yoyote ya uchumi wala fedha, wala biashara. Wengi ni waliosomea ualimu wa Kiswahili, wanasheria, wasiosoma kabisa nk.

Tunapojenga hoja za Kuwekeza katika Bandari zetu, tuelekeze nguvu kwenye namna ya kuboresha ufanisi wa hizi Bandari, nini kifanyike, wapi parekebishwe na wapi paachwe kama ilivyokuwa.

Ni hatari kwa nchi kutegemea watu kama Yericko Nyerere, Ex Meya, Malisa, Mbowe nk kuwa eti ndio wanauchungu na nchi hii kuliko watu wengine wowote. Ni lazima tutenganishe Siasa na Uchumi. Tujenge hoja kwa muktadha wa kiuchumi na sio Siasa. Bandari nyingi Duniani zinaendeshwa kwa mfumo huu, wa kwamba Operesheni hufanywa na Private sector na umiliki ni wa Government, yapo makampuni makubwa sana hufanya kazi hizi mfano, Bollore, PSA, nk.

Shida ni nini?
1. Hapa kuna kundi la watu wao ishu sio Bandari kupewa wageni kufanya kazi la hasha, hawa hawataki tu uwekezaji wa WAARABU, kundi hili hata uliambie nini wao wataweka hoja za Uarabu na si Kiuchumi zaidi. Kundi hili wako tayari Bandari wapewe wazungu. Kundi hili limejaa zaidi UDINI.

2. Kuna kundi wao ni CHADEMA, yaano hakuna kitu, au program ya Serikali itawekwa na wao wakakubaliana nayo, upotoshaji hapa ndio umelala zaidi. Matamko, hashtag nk, kundi hili halijawahi kupongeza kwa lolote na kwamba wao ndio wanaweza kuongoza nchi hii, ingawa wameshaprove kufeli hata ndani ya chama tu.

3. Hapa kuna kundi, linataka kujenga hoja, ila kwakuwa hawajasoma au kufatilia mkataba wenyewe basi wapo kujichagulia upande wanaoona wao unafaa.

Ni hivi wadau, hii nchi yetu sote, hakuna kiongozi mwenye lengo la Kuongoza nchi masikini Duniani. Nchi hii ina wanasheria wengi sana, Majaji wengi sana, wanaojua mikataba wengi sana nk, haiwezekani Mkataba uletwe hauna maelezo ya kueleweka.

Watu wengi wako na kipengele cga ukomo wa mkataba, wengine wanasema hauna mwisho ma wengine Miaka 100, mradi kuvuga hoja tu.

Sio kila mkataba una time frame jamani, kuna mikataba inamalizika pindi kazi ikiisha. Mfano kazi ya uongezaji wa Kina, itafanyika Milele?, Ujenzi wa Gati unafanyika milele? Sijaona kipengele chochote cha Miaka 100 wala waliposema watafanya milele na hakuna kuvunjwa. Kama mtapitia Article 23 basi mtajaribu kuona utaratibu gani wa kufanya ikitokea kuna shida.

Binafsi naona ni hatua nzuri kwa Serikali kiachia shughuli za Bandari ziendeshwe na Private sector ili kuleta ushindani dhidi ya Mombasa.

Tutenganishe SIASA na UCHUMI.
wewe jamaa ni mpuuzi mkubwa.
 
Sijajua wewe unanena haya ukiwa mlengo upi?
Mipango mingi liyopangwa chini ya mzee wa Msoga haijawahi kuwa ya maslah ya Taifa, nina mfano mingi tuuuuuu:
1 DEGE eco village --- huu ulikuwa upigaji uliokithiri kwa kuwa walisahau hata kunawa mikono. Sasa mradi haufai hata kufugia njiwa.
2. Daraja la Kigamboni ------- utakubaliana na mi kuwa hii ni white elephant na sasa ndipo wavhimnguzi wa mambo wanabaini kuwa daraja ni kipingamizi cha uendelezaji wa bandari:
3. Nyumba za makazi ya wanajeshi--------- uliza taarifa jinsi hizo nyumba zilivyo sub standard na zisizofaa kwa makazi.

Vipi usakama wetu tunampompa mwarabu kuwa msimaamizi wa lango kuu la kuingia nchini?
Mbona umeweka miradi michache? Kigamboni kuna shida gani? Kuna Rais nchi ameleta maendeleo kumshinda Kikwete?
 
Miaka 62 ya Uhuru lakini bado watanzania Hawaelewi na hawajui ni namna gani ya kujiongoza wenyewe..

Kila kukicha ni mijadala isiyo na mwisho.

Hii inadhihirisha wazi kwamba HATUWEZI kujitawala na kujiongoza wenyewe.

Wakoloni walikosea sana kutupa UHURU.ndio maana Viwanda vingi vya enzi ya wakoloni vilikufa baada ya wao kuondoka.

Uafrika ni LAANA.
 
kabla sijamalizia kusoma kundi la CCM Sijaliona hapo linasemaje.
 
Kwa hiyo kwa akili yako kidogo uliyonayo ni wananchi wangapi watafunga safari kwenda bungeni kutoa maoni yao!? Hivi unawaza kwa kutumia nini?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata kwenye wizara ya afya walitaka maoni kuhusu toto afya, watu wengi walikataa isiondolewe. je kipi kilibadilika?
Hakuna kitu kinaitwa maoni ya wananchi hapa Tz.
 
Daaah, kuyaelewa haya mambo yanataka akili sana.
 
Maana ya kupeleka Bungeni si ni uwazi? Lini uliwahi kuona Serikali inapeleka mikataba Bungeni?
Ualimu wa Histori unawezaje kuchambua uchumi kama sio kufuata mkumbo wa kisiasa?

Uliwahi kuona wapi mwekezaji anapewa Muda wa kuwekeza? Utengenezaji au utoaji wa Huduma fulani bila kuweka mitambo nk huwa na muda.

Lini mwekezaji alipewa muda unaotaka wewe kuuona?
Ticts hakupewa!?
 
Sasa kwa wewe ambaye unajiona ni mchambuzi wa uchumi, una tija gani kwenye hii nchi kupitia huo uchumi wako? Mbona miaka zaidi ya 60 sasa nchi bado ni masikini?

Au usomi wenu nyinyi ni wa kujitutumua tu kama wa ndugu yenu mwigulu! Watu wanataka ufafanuzi. Kwq sababu wamechoka kuendelea kuona watawala wakiliingizia Taifa hasara kupitia mikataba ya kimangungo.
Mburura huyo hajui kitu
 
Ticts hakupewa!?
TICTS hakuwa mwekezaji, alikuwa mtoa huduma tu, Mwekezaji hana Tenda. Mwekezaji anakuja na mtaji wake kuwekeza, Ticts walikuwa watoa huduma tu ili kurahisha hawakuwa kama wawekezaji.
 
Mbona umeweka miradi michache? Kigamboni kuna shida gani? Kuna Rais nchi ameleta maendeleo kumshinda Kikwete?
Mimi nikuombe ukanushe mifano niliyotoa kwa hayo manufaa ya miradi hiyo. Ni veama pia ujikumbushe nini kilikwamisha utekelezaaji wa mradi wa uzalishaji sukari wa mkulazi - FYI- wayu wenye nia njema waligundua kuwa gharama ya mitambo iliyokuwa imeombewa fedha ilikuwa mara 6 ya uhalisia ndiyo maana hadi leo kiwanda hakija jengwa: Sasa kama ni maendeleo - basi ni maendeleo ya mfukoni kwa huyo uliyemteja
 
Back
Top Bottom