SIASA OVU KUOGOFYA WAWEKEZAJI.

Mpalakugenda

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
4,321
4,607
Kuafuatia MCC kusitisha kuendeleza miradi yote iliyokuwa inafanya hapa Tanzania hofu inazidi juu
1. Foreign direct investment. Je bado wanaiona tanzania sehemu salama ya wao kufanya uwekezaji? kama ndio,je ni ile ya muda mrefu ama ya kuchuma haraka na kuondoka maana hawajui kesho yao itakuwaje.
2. Fedha yetu kuendelea kukosa thamani kwa wawekezaji waliopo kuhamisha fedha.
3. Tunaingia katika hatari ya kutengeneza ukosefu wa ajira.
4. Tanzania mpya ya viwanda kutokutimia.
5. uwezekano wa kukosa fursa ya kufanya biashara za kimataifa.
6. Inaweza kutupunguzia uaminifu katika jumuia za kimataifa katika masuala mbali mbali.
7. Uharibifu wa mazingira kuendelea
8. Utalii kuwa shakani pia,kwa tabia ya wazungu wakaanza kuiona Tanzania sio sehemu salama pengine kudhani ni kama Somalia,Afghanstan,Iraq ama libya.
Niwaombe watawala watutazame sisi wananchi kwa jicho la Kimungu maana ndio wanaotuomba tuwaombee kwa Mungu. Wasingoje tukione cha moto.
 
Back
Top Bottom