Siasa ni KILIMO 1982

Siasa ni KILIMO 1982

Malick M. Malick

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2013
Posts
658
Reaction score
314
SIASA ni KILIMO

"Tangu Mwaka 1967 tumekua tukisema kuwa "Kilimo ndicho Uti wa mgongo wa maendeleo yetu". Mwaka 1972 tukatoa mwongozo wa "Siasa ni Kilimo".Mwongozo huo una mambo yote muhimu yanayohitajiwa ili kubadili na kuendeleza Kilimo chetu. Hatuachi kuzungumzia umuhimu wa suala hili. Viongozi wote wa Chama na Serikali, pamoja na mimi mwenyewe, tumeendelea kuwahimiza wakulima kuongeza juhudi. Tumeweka" maelezo "kwa mazao mbalimbali, kwa kawaida kuanzia katika ngazi ya serikali kuu na kwenda chini.

Tumepanga" mazao ya biashara "katika sehemu ambazo toka zamani hazina mazao ya kudumu. Tumeanzisha miradi ya mahindi na ya tumbaku kushirikiana na mashirika ya kimataifa. Nakadharika. Lakini pamoja na yote hayo nasema Leo kwamba tumekipuuza Kilimo.

Kwa sababu ya umuhimu wa Kilimo katika maendeleo yetu, ungetazamia kwamba kilimo na mahitaji ya wakulima, ndiyo kingekua mwanzo na msingi wa mipango yetu yote ya Uchumi. Tuliutambua ukweli huu tangu 1967, tulipokiri katika azimio la Arusha kua "Maendeleo msingi wake ni WANANCHI na juhudi yao na hasa katika KILIMO".

Na Mwaka 1972 tulizidi kuukiri ukweli huu katika kijitabu chetu, siasa ni Kilimo, tuliposema "kwa miaka ijayo wananchi walio wengi wataendelea kuishi Vijijini na kujipatia riziki yao kwa njia ya kilimo" Lakini tumekifanya kilimo ama ni Kitu cha pembezoni ama ni shughuli ya kawaida, inayopewa uzito sawa na shughuli nyingine zote na inayozihudumia sekta nyingine Bila kudai kuhudumiwa na sekta hizo. Viwanda vyetu vinatumia mazao ya kilimo, lakini huduma ya Viwanda kwa Kilimo kwa kawaida si ya moja kwa moja na tena ni kidogo sana.

Mipango yetu ya Elimu inategemea mazao ya kilimo lakini kwa wasomi na Vyuo vyetu vya kila aina, kilimo hakina Heshima :sana heshima yake kumpatia msomi diploma au shahada, Lakin baada ya hapo kilimo chenyewe hakimshughulishi. Vijana wetu wengi wanaacha Vijiji na kwenda mijini kutafuta kazi za kuajiriwa, kwa sababu wanadharau kilimo na kilimo chenyewe tumekiacha katika hali ya kudharaulika.

Tunakipuuza kilimo. Tungekuwa hatupuuzi kilimo kila wizara moja moja, kila Shirika la Umma, na kila kiongozi Chama, angekua anajishughulisha na mahitaji ya Mkulima, ya moja kwa moja na mengineyo. Tunakitegemea kilimo. Sababu moja ya kutumbukia katika matatizo yetu ya sasa ni kwamba kilimo Bila kusaidiwa sana hakiwezi kubeba mzigo wa maendeleo yetu. Hata kama Wizara ya kilimo ikiwa mbovu kiasi gani, matatizo ya kilimo si matatizo ya Wizara moja peke yake.

Kilimo chetu cha asili ndicho kimetulisha na kutupa maendeleo haya tunayo jivunia. Lakini ni dhahiri kwamba kilimo hiki cha asili, Bila mabadiliko, hakiwezi kutupatia ongezeko la mazao tunalohitaji kwa maendeleo yetu ya kisasa. Miji yetu inapanuka kwa haraka, watu wetu wanaongezeka kwa kiasi kikubwa kwa Mwaka, vijiji vyetu vinadai maendeleo ya kisiasa.

Mzigo unaobebwa na kilimo hiki cha asili sasa ni mzito mno. Wakulima wetu wanaofahamu hivyo, na sisi tunafahamu pia. Wao wanataka mabadiliko. Na lazima tufanye mabadiliko katika kilimo chetu. Lakini mabadiliko yenyewe hayana budi yaeleweke kwa wakulima wetu. Na kueleweka huko kunataka vielelezo. Ni vijiji vingapi ambavyo vina mashamba mazuri ya vielelezo? Ni mabwana shamba wangapi Vijijini ambao wanalima au kusimamia mashamba kama hayo? "

" Baba wa Taifa Mwl J. K.NYERERE. mkutano mkuu CCM 1982. Dar Es Salaam
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom