Watanzania
JF-Expert Member
- Jul 7, 2009
- 727
- 42
Tangu enzi za Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani, Mrema alitangaza kuwa Kambona hakuwa raia wa Tanzania na kuwa atakamatwa uwanja wa ndege akitokea uhamishoni. Salim Ahmed Salim naye alikuwa akipakaziwa katika kampeni za kuwania urais kwa tiketi ya CCM kuwa alikuwa ni raia wa Saud Arabia. Generali ulimwengu aliambiwa siyo raia wa Tanzania baada ya kumkosoa Mkapa. Mtikila naye akazusha ya kwake kuwa Nyerere hakuwa raia wa Tanzania na kuwa ni raia wa nchi jirani na Tanzania. Kuna makamu wa BMT aliwahi kufukuzwa nchini kuwa hakuwa raia wa Tanzania. Bashe na Mkulo nao wanasemekana siyo raia wa Tanzania. Pia Mkapa aliwahi kuandamwa na wanasiasa kuwa ni rais wa Msumbiji. Rostam Aziz naye anasemekana ni raia wa Iran. Unaweza kujaza kurasa kuelezea visa vya wanasiasa au nafasi za uongozi na uraia. Kwa nini idara ya uhamiaji isifanye kazi yake barabara kuanzia huko wanakoishi wananchi. Hivi sasa inaonekana masuala ya uraia yanatiliwa mkazo kwenye suala la kugombea uongozi. Kinachotakiwa ni idara ya uhamiaji isitoe elimu ya uraia ili raia wajue haki zao na kulinda usalama wa nchi kwa kuzuia wahamiaji haramu. Suala hili ni muhimu kwa haki na wajibu wa Watanzania, usalama wa Taifa na ulinzi wa mali za Watanzania. Uhamiaji na serikali tekelezeni sera na sheria za uhamiaji vema vinginevyo uraia unaonekana kutumika kama mtaji katika siasa.
Mkuu unauliza swali hili kama vile wewe si mtanzania. Ni idara gani Tanzania inafanya kazi yake barabara, sasa hivi watu wako busy na kujichumia pesa, hakuna aliyeonesha uzalendo wa kutosha kwa Tanzania. Kama ingekuwa hivyo ujinga wote tunaousikia usingekuwepo. Nafahamu watu wengi tu wasio watanzania, lakini ukienda kusema uhamiaji unaweza kushangaa mwenyewe unaingia jela. Jaribu kusema Rostam Aziz si mtanzania uone kitakachokukuta.
Hapo ndipo shughuli ilipo, usalama wa nchi yetu upo mashakani. Kunatakiwa mabadiliko makubwa sana ili nchi yetu ibaki salama.
Mkuu kuna mambo ya ajabu sana yanatokea siku hizi. Huwezi kuamini, kuna watu wengi sana wanatanua na passport za Tanzania nje ya Tanzania, wahindi kibao wanakuja toka India wanakaa Tanzania mwaka tu wanafanya ujanja na kupata passports za Tanzania wanaenda kuishi Canada, hawajui kiswahili hata siku ya uhuru wa Tanganyika, ajabu wengine hata Nyerere hawamjui. Kuna wengine wengi tu wamesoma shule za serikali, wengine mpaka wanaomba hata mikopo bodi ya mikopo na wengine wengi wanaomba visa hapahapa Tanzania kwenda nchi za nje kwa kutumia passport za Tanzania, nobody cares.
Kuna mambo mengi ambayo miaka 10 iliyopita yalikuwa unthinkable lakini sasa ni common knowledge. Zamani haikuwa rahisi majambazi kwenda kufanya uhalifu at our city centre, lakini sasa wanaweza kufanya hivyo even 500 meters kutoka Ikulu. sasa hivi wezi wanaweza hata kuiibia benki kuu na kuendelea kutesa mjini huku wakiwa na ulinzi juu. Hii inaonesha kuwa sasa hivi watu hawana interest na usalama wa Tanzania na wa watanzania. wanaangalia hela zao tu.
Nani wa kulaumiwa? Sisi Watanzania, idara ya uhamiaji au Serikali? Watanzania tufanyeje sasa?. Tuache mambo yaendelee kama yalivyo? Tukiacha mambo yaendelee hivi wajukuu zetu wataishi mazingira gani?.
tatizo pia ni mfumo mbovu wa kutunza kumbukumbu. rai hawana kitambulisho chochote kuutambua utaifa wao unategemea nini. nenda kenya au hata rwanda uone jinsi wanavyofanya kutambuana.eo ukiambiwa sio raia huna kitambulisho wala baba hana wala babu tabu tupu.
ndio maana watu wanatumia mwanya huo kuharibiana
kujihakiki hakutasaidia chochote, kwani siku ukikaa on the wrong hand ya watawala hawatazitambua hizo document za kujihakiki kwa sababu hivi vyombo utakapaenda kujihakiki havina credibility yoyote mbele ya watawala, hasa pale vitakaposema tofauti na wanavyotaka.
Mkuu this is very interesting. Kuna watanzania wengi tu wana uraia wa nchi mbili lakini kwa kuwa wako upande wa serikali serikali iko kimya kabisa. Kuna wengine wengi tu huwa wanatangazwa na wanasemwa kuwa ni raia wa nchi nyingine, na hata uthibitisho unawekwa hapa lakini hakuna linalofanyika. Kuna wageni mpaka wamekuwa magavana wa Benki Kuu, wengine mpaka wakuu wa wilaya, walipojifanya kusimamia utaratibu wakatimuliwa na kuitwa wageni.
You can ask yourself kwanini mtu kama kinana is always low key, although yeye ni mmoja kati ya outstanding Tanzanians. Ametegeshewa bomu la uraia.
Kwa nakubaliana na unachosema kuna wakati ukiidifu CCM na serikali, au ukikaa kimywa wanapofanya madudu yao basi you are good. Hii ni TZ.
Bongolander, kumbe unaelewa system iliyopo Tanzania....kwa upuuzi kama huu ambao umetawala katika serekali ndio maana nashindwa kufahamu hawa watu wanao itawala Tanzania wana imani kweli na nchi yao? Mimi nimepata bahati ya kuishi nje ya Tanzania kwa miaki mingi sana ,sijawahi kuona mambo kama haya popote pale. wenzetu kila raia anjua haki yake na kila raia anajua umuhimu wa kuilinda nchi yake. Sisi bongo tunaishi kama wadudu tu, viongozi na raia wa kawaida wote tuko kundi moja. Ndio maana naona wanzanzibar wanafanya cha maana kutaka kuwa kivyao... kwasababu huu utawala mbovu unarudisha watu nyuma ...kama wazanzibari watakua na nchi yao basi naamini watapiga hatua haraka sana...na hii labda inaweza kutuokoa sisi... kwasababu hawa viongozi wetu hawatakua na visingizio tena.Mkuu unauliza swali hili kama vile wewe si mtanzania. Ni idara gani Tanzania inafanya kazi yake barabara, sasa hivi watu wako busy na kujichumia pesa, hakuna aliyeonesha uzalendo wa kutosha kwa Tanzania. Kama ingekuwa hivyo ujinga wote tunaousikia usingekuwepo. Nafahamu watu wengi tu wasio watanzania, lakini ukienda kusema uhamiaji unaweza kushangaa mwenyewe unaingia jela. Jaribu kusema Rostam Aziz si mtanzania uone kitakachokukuta.
Bongolander, kumbe unaelewa system iliyopo Tanzania....kwa upuuzi kama huu ambao umetawala katika serekali ndio maana nashindwa kufahamu hawa watu wanao itawala Tanzania wana imani kweli na nchi yao? Mimi nimepata bahati ya kuishi nje ya Tanzania kwa miaki mingi sana ,sijawahi kuona mambo kama haya popote pale. wenzetu kila raia anjua haki yake na kila raia anajua umuhimu wa kuilinda nchi yake. Sisi bongo tunaishi kama wadudu tu, viongozi na raia wa kawaida wote tuko kundi moja. Ndio maana naona wanzanzibar wanafanya cha maana kutaka kuwa kivyao... kwasababu huu utawala mbovu unarudisha watu nyuma ...kama wazanzibari watakua na nchi yao basi naamini watapiga hatua haraka sana...na hii labda inaweza kutuokoa sisi... kwasababu hawa viongozi wetu hawatakua na visingizio tena.
Mkuu kuna mambo ya ajabu sana yanatokea siku hizi. Huwezi kuamini, kuna watu wengi sana wanatanua na passport za Tanzania nje ya Tanzania, wahindi kibao wanakuja toka India wanakaa Tanzania mwaka tu wanafanya ujanja na kupata passports za Tanzania wanaenda kuishi Canada, hawajui kiswahili hata siku ya uhuru wa Tanganyika, ajabu wengine hata Nyerere hawamjui. Kuna wengine wengi tu wamesoma shule za serikali, wengine mpaka wanaomba hata mikopo bodi ya mikopo na wengine wengi wanaomba visa hapahapa Tanzania kwenda nchi za nje kwa kutumia passport za Tanzania, nobody cares.
Kuna mambo mengi ambayo miaka 10 iliyopita yalikuwa unthinkable lakini sasa ni common knowledge. Zamani haikuwa rahisi majambazi kwenda kufanya uhalifu at our city centre, lakini sasa wanaweza kufanya hivyo even 500 meters kutoka Ikulu. sasa hivi wezi wanaweza hata kuiibia benki kuu na kuendelea kutesa mjini huku wakiwa na ulinzi juu. Hii inaonesha kuwa sasa hivi watu hawana interest na usalama wa Tanzania na wa watanzania. wanaangalia hela zao tu.
Duh, Tanzania hii inatisha!Mkuu kuna mambo ya ajabu sana yanatokea siku hizi. Huwezi kuamini, kuna watu wengi sana wanatanua na passport za Tanzania nje ya Tanzania, wahindi kibao wanakuja toka India wanakaa Tanzania mwaka tu wanafanya ujanja na kupata passports za Tanzania wanaenda kuishi Canada, hawajui kiswahili hata siku ya uhuru wa Tanganyika, ajabu wengine hata Nyerere hawamjui. Kuna wengine wengi tu wamesoma shule za serikali, wengine mpaka wanaomba hata mikopo bodi ya mikopo na wengine wengi wanaomba visa hapahapa Tanzania kwenda nchi za nje kwa kutumia passport za Tanzania, nobody cares.