Siasa katika taaluma: Vyuo vikuu vinaelekea wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Siasa katika taaluma: Vyuo vikuu vinaelekea wapi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by miradibubu, Aug 27, 2011.

 1. m

  miradibubu JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 313
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ninaomba nianze kwa kukiri kwamba mimi ni miongoni mwa wadau katika taaluma!

  Ninachukulia maana ya neno siasa kwa namna isiyo rasmi hususani kama ambavyo watu wa kawaida wanavyoweza kuichukulia kuwa ni kitu cha masikhara, kupoteza muda,ambatana na matendo yasiyofaa, maamuzi ya ajabu na yasiyona yanayoambatana kutenda kwanza na baadaye ndio unafikiria na si kinyume chake.

  Kabla sijaendelea ninaomba niwashirikishe mtazamo wangu juu ya vyuo vyetu vikuu hapo awali kabla sijapata mtazamo sahihi nilionao sasa. Niliamini kwa dhati kabisa kwamba chuo kikuu ni mahali salama sana ukilinganisha na wanaokimbilia katika siasa.

  Ukweli ni kwamba katika eneo hili ninahisi ni baya zaidi kuliko hata katika siasa. Hii ni kutokana na hoja kwamba vitendo vya zaidi ya siasa ndio vimetawala na hakuna uhuru wa kitaaluma nilioutarajia bali mambo yanaenda hovyo kama nchi yenyewe inavyokwenda.

  Huenda hii hali kuyumbayumba ni kielelezo tu cha namna ambavyo taifa linapoteza mwelekeo.

  Kunamambo mengi yanayodhihirisha usiasa katika vyuo vikuu ikiwa ni pamoja na ubabe, kujipendekeza, rushwa za ngono, kujuana, udini uliokubuhu(uislamu dhidi ya ukristo), kuoneana, uzembe katika kutimiza wajibu, na kuchelesha wanafunzi wa masters kumaliza kwa wakati.

  Kwa leo hii, ninapenda tu kuwashirikisha "usiasa" wa jambo moja tu ambalo ni kero kubwa sana katika vyuo vyetu vikuu ambalo ni kuwachelewesha wanafunzi wa masters kumaliza masomo yao kwa wakati.

  Ninapenda nitolee mfano tu katika chuo kikuu cha Dar es salaam kutokana na ukweli kwamba hiki ndio chuo chetu kikongwe na kimeathiri kwa namna nyingi hata vyuo vingine vilivyopo hapa nchini.

  Athari hizi zinajitokeza kupitia hata kwa wahadhiri wengine walioajiriwa katika vyuo vingine kwani huenda walisoma katika chuo hiki au walihama kutoka mlimani na kujiunga na vyuo vingine.

  Tatizo hili la kuchelewesha wanafunzi wa masters kumaliza limeota mizizi katika baadhi ya idara za chuo kikuu cha Dar es salaam.

  Idara hizi ni pamoja na SHERIA, HISTORIA, LUGHA ZA KIGENI NA ISIMU(fOREIGN LANGUAGES AND LINGUISTICS),SOSHOLOJIA NA SAYANSI YA SIASA. Niwe muwazi kabisa kwamba kuanzia mwaka jana lugha za kigeni na isimu wamejitahidi sana kwani ni wanafunzi wengi wamemaliza.

  Ninashindwa kuelewa kama uongozi wa chuo husika kama wanalifahamu hili, huenda wasilifahamu kutokana na uoga wa wanafunzi wa nchi hii katika kudai haki zao na matokeo yake siku zote wamebaki kupata haki zao kwa huruma kabisa.

  Tabia ya kuwajengea woga wanafunzi wetu ime;leta matatizo makubwa sana kwa wanafunzi kwani wanakosa kujiamini hata wanapoitwa katika usaili wa kazi.
  Kwa upande mwingine huenda uongozi wa chuo unafahamu lakini yanakuwa yaleyale ya kesi ya nyani unampelekea ngedere.

  Kwa kila mmoja inabidi afahamu kwamba kuna tatizo tena kubwa sana ambalo ninahisi litakuwa na madhara kwa taifa kwani mtu anapoipata masters yake kwa shida anakuwa ameondolewa utu wake na kilichopo mbele yake ni kuifurahisha nafsi yake mwenyewe.
  Ninafahamu hao wanazuoni watajitahidi kujitetea kwamba hii hutokana na uzembe wa mwanafunzi mwenyewe.

  Ili kuufanya utetezi huo usiwe na nguvu ni kujaribu kuangalia muda unaotumiwa na maprofesa hawa kusoma kazi, wanatumia muda mrefu mno kuipitia kazi kwani unashahidi wa wazi hata wengine mnaosoma kichokoo hiki mtathibitisha hili kwamba unaweza ukampa kazi yako mwalimu(profesa) akakuambia wewe nenda na usipige simu mpaka nitakapokuita.

  Utakapoondoka unaweza ukakaa miezi mitatu bila kuiona hata kuinusa hiyo simu, ukipiga moyo konde ukaenda ofisini kwake ni ajabu na kweli atakapokuambia hata ile kazi(utafiti) uliyompa hajui alipoiweka labda umpe nyingine ndio aanze kuisoma.
  Kumbuka katika hali hii huyu mwananafunzi amepoteza muda na pesa yake, wakati mwingine labda amesafiri kutoka bukoba hadi DSM.

  Hali hii imekwamisha mafanikio ya watu wengi na wakati huohuo tumelifanya taifa kutumia pesa nyingi kwa muda mrefu likisomesha wakati mwingine mtu mmoja tu.
  Uzembe huu unaojitokeza, sikusudii kusema kwamba huwa ni njia ya kudai rushwa ya pesa na ngono hapana huu ni utamaduni tu wa muda mrefu wa vyuo vyetu.

  Ninamkumbuka mwalimu wangu mmoja wa hapo mlimani( siku hizi amekaribia kuwa Prof.) alitushauri kwamba tusitamani kusoma tenahapa mlimani kwani mtatumia muda mrefu sana kuliko kawaida.

  Alijitolea mfano yeye kwamba Phd yake ameisomea nje ya nchi miaka mitatu wakati wenzake wanaojaribu kuisomea mlimani wakijitahidi sana ni miaka saba lakini wengi ni miaka kumi( isipokuwa mwaka jana kuna dada mmoja wa Kiswahili amesoma phd kwa miaka mitatu- Hongera Kiswahili kuonesha njia).

  Hebu tujiulize, je ni kweli kwamba kwa kuwachelewesha sana wanafunzi kumaliza inawafanya wawe bora? Inakuwaje mtu huyuhuyu akienda nje ya nchi katika vyuo bora kabisa kuliko UDSM anamaliza kwa wakati.

  Mimi ninadhani hali hii haimfanyimwanafunzi kuwa bora bali anafanywa kutojiamini na hata anapokuwa kazini akikumbuka namna ambavyo ameisumbukia masters jeuri yote ya kujiamini katika kazi inaisha.

  Huwa ninajiuliza je huu ni mkakati wa wazee ili waendelee kukaaa ofisini napo ninakosa majibu kwani kuna baadhi ya wazee wanaoendelea na kazi kwa makata wanafanya kazi vizuri zaidi.

  Baadhi ya walimu wamejawa na kasumba ya kwamba hakuna mtu mwingine anyeweza isipokuwa wao peke yao. Hali hii imesababisha upungufu mkubwa wa raslimali watu hata katika hivyohivyo vyuo vikuu.

  Si ajabu ukamkuta profesa hadi anastaafu katika eneo lake alilojiimarisha(area of specialization)hajawahi hata kutoa mwanafunzi hata mmoja wa masters. HIVI KUNASABABU YA KUENDELEA NA WATU WA NAMNA HII?

  Nimalizie kwa kutoa rai kwa wanafunzi wa masters wote wnaotaabika katika baadhi ya vyuo nchini: Jamani acheni uoga kumaliza ni haki yenu usisubiri hisani tafuteni namna yoyote ya kumaliza huu ukoloni ili tuongeze idadi ya wasomi.
  Ninawasilisaha!
   
 2. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Tatizo hapa, utakuta mwalmu mmoja anafundisha vyuo vitatu. Anafundisha Mliman, SUA, UDOM, St. August.
  Kuna mwl mmoja hapo namfaham anafundsha vyuo v3 anakosa muda wa kuwahudumia wanafunz. Pia waalimu wa vyuo wamepewa madaraka makubwa sana. Wao ndio waamuz wa mwsho.
   
 3. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  Wanafunz wa kibongo wanaomba hak zao badala ya kuchukua.
   
 4. only83

  only83 JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  ..............UDOM ndio uozo kabisa,wanaleta na UDINI kabisa.............
   
 5. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2011
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  I congratulate you for the analysis. I believe the trend has changed in other institutes. However, remember that "YOU ONLY GET WHAT YOU PAY FOR" I believe the instructors are putting in the amount of time and effort equivalent to the salary and fringe benefits they are getting.

  This is the country that have chosen to pay hefty sums to those who do not deserve (MPs, Politicians, Ministry officials through masurufus and poshos) and neglect those deserves (Doctors, Nurses, Teachers, Engineers, Magistrates, etc).
  • RESULTS: They spend time and work just equivalent to the money they receives.
  • WAATHIRIKA: Jamii nzima, halafu haitambui kuwa wanaathirika.
  • USHAURI: Jitahidi kusambaza injili na misahafu nchi nzima kuwa SASA BASI!!!!
  Come 2015 (Kama tutafika) mabadiliko ya nguvu.
   
 6. m

  miradibubu JF-Expert Member

  #6
  Aug 27, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 313
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Ninajua wahadhiri wana matatizo yao ya kimaslahi lakini je hasira zao ndio ziende kwa wanafunzi?
   
 7. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #7
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
  kila mmoja anaangalia line of weakness
   
 8. c

  chama JF-Expert Member

  #8
  Aug 28, 2011
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ikiwa sifa ya mhadhiri ni kefelisha wanafunzi, ipo haja watafute kazi nyingine, sifa ya mwalimu yeyote yule ni kuwa na wahitimu wengi.
   
 9. menyidyo

  menyidyo JF-Expert Member

  #9
  Aug 28, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 1,339
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  hapa sasa title inaendana na content. bravo.
   
 10. T

  Tata JF-Expert Member

  #10
  Aug 28, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  If an correct Nyerere once said "if you think education is expensive try ignorance". Unfortunately as a country we thought education was expensive and tried ignorance and now we are reaping the fruits. Ujinga emeenea toka kwa wananchi, viongozi wa siasa na serikali mpaka kwa wahadhari wenye vyeo vya madokta na maprofesa kwenye vyuo vikuu. Ni ujinga tu wa wahadhiri unaowasababisha kuweka vikwazo kwa wanafunzi kumaliza kozi zao kwa wakati. Kusema siasa unapunguza makali ya tatizo. Kwa ufupi tu sababu SIYO SIASA NI UJINGA WA WAHADHIRI. Kuna ushahidi mwingi wa hili janga la UJINGA nchini linavyotutafuna.
   
 11. k

  kiloni JF-Expert Member

  #11
  Aug 28, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Pole sana ndugu. Miye nimehangaikia mchakato wa kunisaidia kuthibitisha kwamba niliwahi kupitia chuo kikuu kimoja hapa nchini baada ya kuunguliwa vyeti vyangu kwa miaka sita sasa na bado.
  Hao wakubwa ni zao la ufisadi wa nchi hii. Ukiona mtu anajiita professor lakini anakimbilia vihongo vidogo na rushwa za ngono huyo ni ZUZU kama wendawazimu wengine tu wa mitaani. Elimu kama kweli ni utaalamu wa kumwezesha mwanadamu kupambana na mazingira yake kimaisha, basi tuwaiteje hao maprofessor waliobobea kwenye ULEVI wa kupindukia na ngono ovyo ovyo? hao ni mazuzu tu.
  Wala usilaumu siasa!! Kumbuka kuna miaka ya kabla ya 1970s -1980s ambao hapo mlimani palijulikana kama "BURNING HILL" jinsi palipoweza kupika wazalendo wataalamu wazuri ajabu. Kwa manufaa yako marais wanaotuzunguka na wapigania uhuru wenye uzalendo wamezalishwa hapo mlimani.
  Hayo MAZUZU kama yametengenezwa na mfumo wa nchi au kwa utashi wao basi sielewi ila panahitaji OVERHAULING kama hayajamaliza kizazi cha nchi hii.
   
 12. m

  miradibubu JF-Expert Member

  #12
  Aug 29, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 313
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Licha ya hayo yote wanafunzi ninawashauri wasikate tamaa bali waamke ili kutetea haki zao
   
Loading...