Siasa inaiua nchi, Serikali fanyeni kazi acheni siasa


Mahweso

Mahweso

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2014
Messages
1,071
Points
2,000
Mahweso

Mahweso

JF-Expert Member
Joined Jan 10, 2014
1,071 2,000
Kama Serikali iliopo madarakani ni ya CCM, inakuwaje badara ya kuyanya kazi bado inapiga Siasa?
Kwa sasa hivi nijuavyo mimi, Serikali ya CCM ina maamuzi ya kila kitu, sasa kama Mtu una maamuzi kwanini usifanye kazi unabaki kutoa matamko?

Kuanzia leo sitaki hiki
Kuanzia leo sitaki Shisha, Sheria hujaitunga ya kuzuia hicho kitu
Kuanzia leo sitaki Machinga Barabarani, Maeneo ya Biashara Ndogondogo huna,

Miradi ikianzishwa wa wenzenu mnaikwamisha , kisa watapata sifa, tena hii ndio mbaya sana maana wanao pata madhara na hila hizo ni wananchi sio mwanzishaji wa miradi hiyo.

Mfano mzururi, Tetemeko la Kagera, UKAWA walienda kuwasaidia wananchi kwa kuwafungia Mahema yenye nembo ya UKAWA mliwafukuza, pale aliyepata madhara ni nani? matokeo yake Serikali haijatoa huduma ya aina hiyo mpaka leo, na michango ndio imelekezwa kwenye ujenzi wa miundombinu ya Serikali.

Tuliona Kinondoni Chini ya Meya wa UKAWA walivyofanyiwa figisu kuhusu kufunga mtambo wa kuchakata Taka kuwa Mbolea, umezuiliwa kisa UKAWA watapata sifa, Magomeni kota, Jiji liliwalipa watu pale ilikupisha ujenzi ambao ulikuwa umeshachorewa mpaka Ramani,

kilichotokea mnajua, Kuna ujenzi unaendelea eti kuwajengea wapangaji walikuwepo kukaa kiaka kadhaa bure wakati hao hao watu alishalipwa sijui ile hasara inakuwaje, sababu ni Mpango wa UKAWA hawajari hasara wao mpango uferi basi.

Arusha kwenye Hospitali ya Mama na Mtoto, Tuliona ule mradi Lema aliusaini kabla ya Uchaguzi 2015 lakini Gambo anaenda pale anapotosha, Lema angekuwa hajasaini, ule mradi ungefelishwa vilevile,

Kazi nyingi kufanyika Kisiasa, Wakuu wa Mikoa na Wilaya kufukuza wafanyazi hovyo na kuwaweka ndani wengine, hizi ni Siasa kutaka kujionyesha mnafanya kazi, kwani msiweke utaratibu na sheria Mtu akienda kinyume awe anajua adhabu yake?

Hivi tuamini mawazo ya hao watu ndio Sheria?
Hospitali hazina Dawa unataka mtumishi wa pale afanye nini?
Mnatudanganya kila kitu, Huyu anasema Dawa zipo, huyu kunaupungufu wa dawa,

Ooo sijui dangote hivi, Mara Waziri wa Viwanda analipuka ooooo Serikali tulificha ukweli, Dangote anataka Gesi bure, sasa ukweli unamwagika aibu ya nani? hasara kwa nani? hizo Siasa zenu mnazozileta Serikalini hamuoni zinatufukuzia Wawekezaji na kuwaogofya waliokuwa na Marengo ya kuja kuwekeza?

Hujaomba bajeti ya kununua Ndege wala Tolori, unanunua , Bajeti zinapitishwa za nini, hizo Bajezi za kununua Ndege imepitishwa na nani? au Sifa binafsi nilinunua Ndege Chini ya uongozi wangu huku ukiumiza watu kwa Kukosa Elimu, Tiba, Njaa na Msongo wa Mawazo.

CCM jitafakarini sana , Mnaongoza Nchi fanyeni kazi acheni Siasa za kujionyesha manafanya nini,
 
gbefa

gbefa

JF-Expert Member
Joined
Jun 1, 2016
Messages
3,468
Points
2,000
Age
24
gbefa

gbefa

JF-Expert Member
Joined Jun 1, 2016
3,468 2,000
Sema wote tuache siasa tufanye kazi serikali ni watu ni sisi, acha porojo mkuu Fanya kazi
 
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
38,878
Points
2,000
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
38,878 2,000
Kama waziri mkuu hiyo ziara yake sijaona anachokifanya zaidi ya kutoa ahadi juu ya ahadi
 
Y

Yaleyale

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2011
Messages
1,340
Points
2,000
Y

Yaleyale

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2011
1,340 2,000
Nawe unafanya siasa badala ya kufanya kazi. Serikali ni watu kama wewe hivyo badala ya kuja na ukurasa mrefu ungekuwa unafanya kazi sasa.
 
kivava

kivava

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2013
Messages
5,797
Points
2,000
kivava

kivava

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2013
5,797 2,000
Nawe unafanya siasa badala ya kufanya kazi. Serikali ni watu kama wewe hivyo badala ya kuja na ukurasa mrefu ungekuwa unafanya kazi sasa.
Nawe upo kazini siyo?
 
Kiroboto one

Kiroboto one

Member
Joined
Sep 25, 2017
Messages
71
Points
125
Kiroboto one

Kiroboto one

Member
Joined Sep 25, 2017
71 125
Hakuna mtu ambaye atakataa hayo nisenayo.
 

Forum statistics

Threads 1,283,909
Members 493,869
Posts 30,805,755
Top