Si uungwana kubaguana kwa tofauti za dini

rr3

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
3,045
3,820
Kwa ufupi mno

Unajua mtu unaenda ofisi fulani na anayehusika kutoa huduma hapo ni dini fulani, basi akishaona tu jina lako haliendani na dini yake, utazungushwa kupata huduma hadi ukereke.

Na hii dini inafahamika fika kabisa, ni wabaguzi mno. Sijui huko kwenye nyumba za ibada huwa wanafundishwaga nini.

Ni upuuzi wa hali ya juu kumbagua mtu mweusi mwenzio kisa dini ambayo imeletwa na wakoloni sama mojawapo ya tools of colonisation.

Mtu ukimtajia tu jina anaanza kukupiga chenga bila sababu ila palepale akienda wa dini yake na unamjua anahudumiwa fasta.

Tuondoeni hizi mentality zisizo na maana vichwani mwetu. Sisi ni Waafrika weusi na Watanzania before anything else.
 
Angalia Mkuu na wewe usije kwenda huko huko kwenye huo ubaguzi (ingawa wewe nadhani bado upo kwenye stages za mwanzo mwanzo)

In Short ubaguzi wa aina yoyote ile ni upuuzi, na mbaya zaidi watu wanaotangaza upendo (kwenye dini ni upendo) wanapobagua wengine naona ni Unafiki tu.
 
Angalia Mkuu na wewe usije kwenda huko huko kwenye huo ubaguzi (ingawa wewe nadhani bado upo kwenye stages za mwanzo mwanzo)..

In Short ubaguzi wa aina yoyote ile ni upuuzi, na mbaya zaidi watu wanaotangaza upendo (kwenye dini ni upendo) wanapobagua wengine naona ni Unafiki tu...
Mkuu Mimi sio mbaguzi kabisa. Niko flexible mpaka watu wa dini yangu huwa wanashangaa.

Nina uwezo wa kukaa na waamini wa dini yeyote nikasikiliza mahubiri yao na kusali pamoja na bado Niko very strong kwenye dini yangu though nairegard Kama chombo Cha wakoloni tu.

Kinachonisukuma hasa ni amri ya upendo. Ukiwa na upendo vingine vinakuja tu.

Kinachonishangaza Hawa wenzetu wako very rigid, very rigid. Yaani huwa nawashangaa mno.
 
Ubaguzi ni ubaguzi tu unaweza kutumia dini kubagua,kabila, race,viwango vya elimu, hali za maisha. Tusitafute wa kumpa lawama.
Kweli ubaguzi ni ubaguzi hata wa ukabila upo Ila atleast kwenye ukabila unaweza usitaje jina la ukoo na mambo yakaenda fresh.

Ila huku kwingine hata ukitaja majina mawili tu, tayari ameshajua wewe si mwenzie na figisu zinaanza. Very ridiculous.
 
Mkuu Mimi sio mbaguzi kabisa. Niko flexible mpaka watu wa dini yangu huwa wanashangaa.

Nina uwezo wa kukaa na waamini wa dini yeyote nikasikiliza mahubiri yao na kusali pamoja na bado Niko very strong kwenye dini yangu though nairegard Kama chombo Cha wakoloni tu.

Kinachonisukuma hasa ni amri ya upendo. Ukiwa na upendo vingine vinakuja tu.

Kinachonishangaza Hawa wenzetu wako very rigid, very rigid. Yaani huwa nawashangaa mno.
Sehemu yenye vita amani itakujaje kwa kutumia upendo tu?
 
Ubaguzi ni upuuzi na ulevi wa madaraka.

Baadhi ya viongozi ktk utumishi wa umma hujiona kama nafasi walizo pewa kama vile wanaendesha kampuni za baba zao!! wakijasahau kuwa hii ni serikali/nchi ya watanzania wote.

Lakini pia jambo hili limesababishwa na ukosefu wa UWIANO wa imani za dini ktk nafasi mbalimbali za serikali, unakuta imani moja imejazana/imehodhi ktk nafasi za umma. Hii sio sahihi na matokeo yake ubaguzi huanzia hapo. kwani walio hodhi nafasi nyingi hujisahau na kujiona wao ndio wamiliki wa serikali.

Ndio maaana kila mara nashauri kwamba ktk uteuzi wa nafasi mbalimbali za utumishi wa umma ni lazima mamlaka pamoja na mambo mengine zizingatie pia UWIANO wa imani za dini kubwa mbili ktk nafasi za utumishi wa umma.

Tuache tabia ya kuwajaza watu wa aina moja ya imani ktk nafasi za utumishi wa umma eti kwa kisingizio cha "veting" matokeo yake ndio hayo ya tabia ya ubaguzi hujitokeza!

Hii nchi ni ya watanzania wote hivyo ni lazima ijengwe kwa kushirikiana sisi sote bila kubaguana au wengine kubaguliwa.

Ni lazima mamlaka za UTEUZI zizingatie pia suala la kujenga na kuimarisha umoja wa Taifa letu kwa kuzingatia UWIANO ktk nafasi mbalimbali za uteuzi, tuache kujificha ktk kisingizio cha "Veting", tujenge uzalendo wa nchi yetu, tusijifanye hatuoni!! tusijifanye hakuna madhara.

Tuijenge nchi yetu ktk misingi imara kwa miaka 100 ijayo.

Tuache ubaguzi lkn pia tuzibe myanya ya kibaguzi kwa kuweka Uwiano.
 
Well said
 
Nchi yetu ni nchi huru isiyo na ubaguzi wa kidini. Ila ubaguzi upo ndani yetu hauepukiki hadi siku ya mwisho.

Tuwe wakweli tu tunaubaguzi huo japo hatusemi wala hatuonyeshi.

Kwenye mahusiano unaweza kujisemea siwezi toka na mtu flani kwa sababu ya imani japo hutasema.

Kwenye kazi unaweza kuwekewa au kumwekea mtu ugumu pasipo wewe au yeye kugundua ni kwa sababu ya utofauti wa dini.

Kwa ufupi tutaendelea kubaguana kiaina japo hutotambua kuwa kigezo cha dini kimeusika.
 
Wakati mwingine unaweza hisi umebaguliwa kumbe ndio umeanza kujibagua mwenyewe😃😃😃
Hapana haiwezekani ukajibagua mwenyewe.

Hivi umeona jamaa yako ameingia ofisi flani na amefanikiwa Jambo lake kwa haraka mno.

Wewe unafika pale unaongea na secretary anakuambia hii inawezekana kabisa ngoja bosi akuite. Unaitwa na bosi unaanza kupigwa danadana. Hapo umejibaguaje?
 
Kitu gani kimekufanya uamini dini yako ndio inakukwamisha?
 
Back
Top Bottom