Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Anaandika Mwanahabari Huru
Wapo watu waliochoka kusikia habari za mateso kwa viongozi wao wa vyama vya upinzani.
Wapo waliochoka kusikia habari za kubambikia kesi watu maarufu, wenye msimamo kinyume na matakwa ya serikali.
Wapo waumini wa dini waliochoka kuona viongozi wao wananyanyasika ndani ya nchi yao, kisa wana misimamo tofauti.
Wapo waliochoka kufanya biashara katika mazingira magumu.
Wapo waliochoka kusikia fulani amenyimwa fursa ya biashara, au kuandaa shughuli, tamasha la shangwe nk kisa ana 'bifu' na wateule wa Rais. Mfano; #NyamaChoma #Fiesta
Wapo watumishi wa umma waliochoka kuona na kusikia vitendo vya uonevu wanavyofanyiwa, wao au wenzao, chini ya mkono wa wateule wasio na utashi wa kuongoza.
Wapo waliochoka kusikia habari za kutekwa na kuuawa kwa wananchi wengine, huku vyombo vya dola vikionesha kutojali, tena kuwashughulikia wanaohoji mambo hayo.
Wapo waliochoshwa na sera za ukandamizaji, zinazoashiria kifo cha mfumo wa demokrasia; sheria za habari, sheria ya takwimu, muswada wa vyama vya siasa, kikokotoo kipya cha malipo ya pensheni nk.
Ndio maana, ni rahisi sana kwa mtu mwenye ushawishi kiasi, kuonekana kwamba ndio hasa mbadala wa hatamu iliyopo. Vijana, wapinzani na wasio wapinzani watamshabikia na kumpa kura nyingi, mamilioni. Kwasababu wamechoshwa na 'ujuha' wa utawala/watawala wa awamu ya tano. Hii si hadithi mpya, ni marudio tu.
Bora 'mtu' mwenye chembe za dhambi, ni mtu, kuliko shetani mwenye chembe za wema, ni Shetani.