Si kwamba wananchi wanamshinikiza Rais Samia, bali wanashiriki kufichua uovu waliofanyiwa

sammosses

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,535
2,000
Mamlaka na madaraka ya serikali yatatoka kwa wananchi, na msingi mkuu wa serikali ni ustawi kwa wananchi. Hii ni kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, ambayo ndiyo inayotumika mpaka sasa.

Ukiingia kwenye mitandao ya kijamii utaona maoni ya wananchi,wengi wakimshauri rais hiki na kile lengo kuu ni kutumia haki yao ya kikatiba kushiriki mustakabali wa nchi yao kufikia maendeleo yaliyo kusudiwa.

Uhuru na haki ni funguo unaoweza kuihifadhi haki na wananchi watashiriki kuleta maendeleo kwa Taifa lao.

Lakini si kila jambo lashaurika ndiyo maana ana chuja, na mengine anaendelea kuyafanyia upembuzi yakinifu.

Mamlaka na madaraka ya serikali yanayo toka kwa wananchi ni kwa ajili ya ustawi wa wananchi kama nilivyo kwisha sema hapo juu, maanake yatakuwa na tija kwa serikali pale mlengwa aliyepigiwa kelele kwa utovu wa nidhamu ya utumishi atawajibishwa kwa makosa yake ya utumishi ulio lenga maslahi binafsi kwa kunyang'anya haki za wananchi kwa minajili ya kujinufaisha binafsi.

Ikiwa ni kinyume chake, akalindwa kwa kupewa kitengo kingine bado ule ustawi wa wananchi ambao ndiyo msingi mkuu wa serikali utakuwa ni kazi bure.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano imesisitiza umuhimu wa haki za binadamu, yeyote ataye nyang'anya haki hizo maanake si muumini wa katiba, huyo hatufai.

Jaji Mganga Biswalo katuhumiwa sana kukanyaga haki za binadamu, haikutosha kumtoa kuwa DPP tu na kumficha kwenye mhimili unao tafsiri sheria haki ikiwa ni content ndani yake. Ikiwa alikanyaga haki za binadamu kwa kuwanyanyasa wananchi kwa kesi za kubambikiwa na kuitumia vibaya sheria ya pre bargain kujinufaisha binafsi, iweje leo uteuzi wake kwa nafasi ya kutafsiri sheria na kusimamia haki aliyo ikanyaga kwa makosa aliyoyatengeneza ulete tija kwa maslahi mapana ya Taifa na nchi yetu!

Uko wapi weledi wa chombo kinacho fanya vetting kwa ajili ya mchakato wa kuwapata viongozi.

Ikiwa ametengeneza tuhuma kwa muathirika na yeye ndiye anayekuja kusimamia haki aliyompora mtu huyo, hivi kwa akili nyepesi tu mtuhumiwa huyo atabaki salama.

Hakuna budi kwa rais Samia Suluhu Hassan kulitazama suala hili kwa mapana yake ikiwa kweli ana nia ya dhati kutibu majeraha na vidonda vya wananchi.

Nimsihi japo uteuzi umekwisha fanyika na makosa yamefanyika, iundwe tume huru ya kimahakama kuchunguza mwenendo wa DPP Biswalo alipokuwa akihudumu nafasi hiyo ili kujua ukweli mchungu wa tuhuma anazo tuhumiwa. Tanzania yetu itajengwa na wale wenye moyo Safi.

Pia nitumie fursa hii kukushauri kuachana na kuhamisha hamisha watuhumiwa wa makosa ya kiutumishi,kama mtu amepewa onyo kwa taratibu za kikazi hakubadilika kumhamishia sehemu nyingine ni kuendeleza dhuluma na batili dhidi ya haki. Utaratibu huu ulitumika awamu ya kwanza ndiyo ulio haribu mfumo wa usimamizi wa rasilimali za umma na kuuwa mashirika mengi nchini.

Nafahamu rais ni comforta in chief, comfort yako isitumike kufunika uchafu uliofanywa kwa kuwa una tengeneza dhana ya kuwa, kama sisi ni wachafu kwanini ametuamini tena!

Rais kaza buti, wakizingua wazingue pia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom