Si kila kifo ni mpango wa MUNGU

Si kila kifo ni mpango wa MUNGU

Avatar

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2012
Posts
11,128
Reaction score
11,938
58E62433-1968-4A92-90AF-1759C5AA7934.jpeg

SI kila kifo ni mpango wa Mungu.
Ni sahihi Mungu anajua siku ya kufa kwako lakini kamwe hapangi namna ya wewe kufa.

Ukweli ni kwamba tunakosea kusema “kifo cha fulani ni mpango wa Mungu” kama inavosikika mara nyingi katika misiba mbali mbali.
Hii ni njia tu ya kujifariji isiyokuwa na ukweli ndani yake, kwanini.. chukulia mfano wa mabinti/wanawake wanao waua viumbe kwa kutoa mimba, chukulia vifo vya wafungwa wanaohukumiwa kunyongwa hadi kufa ama kwa kiti cha umeme nenda hata kwenye biblia katika kitabu cha mwanzo kaini alimuua abeli, mahospitalini vifo vinavyo sababishwa na wauguzi wazembe hiyo yote inaonyesha ni dhairi kuwa vifo vyote ni mipango na matakwa ya binadamu wenyewe.

Haya ni matokeo ya Mapenzi ya Mungu kwa binadamu kwa zawadi ya uhuru.

Naomba tuache kumsingizia Mungu, tuishi kwa adabu juu ya huu uhuru tulio zawadiwa na aliyeko juu.

“MUNGU HAPANGI JUU NAMNA YA KIFO CHAKO, LAKINI NI UKWELI KWAMBA ANAFAHAMU SIKU YAKO YA KUFA”

Karibu kwa maoni huru 😉
 
Radio je?
Yule ni ujana wake ulimponza mkuu, we hujasikia kuwa walikuwa night club walikuwa wakizinguana ndipo mlizi akambeba juu na kumtupa chini.
Ingekuaje kama angekuwa kwake !?
 
Alitaka kujiua, je angekufa Mpangaji angekuwa ni Mungu?
Hakuna kifo anacho panga Mungu, Mungu ujua ni lini fulani atakufa,
Nabii tito haikuwa siku yake hiyo, na kama ingekuwa ni siku yake basi style ya kifo chake muhasiusishwe
 
Mhh mtu mwovu!! Kwanini??
Mi najua kifo ni kifo tu haijalishi muovu au mwema
Ezekieli : Mlango 33

11 Waambie, Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi nyumba ya Israeli?
 
Ezekieli : Mlango 18

23 Je! Mimi ninafurahia kufa kwake mtu mwovu? Asema Bwana MUNGU; si afadhali kwamba aghairi, na kuiacha njia yake, akaishi?

Ezekieli : Mlango 33

11 Waambie, Kama mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya; mbona mnataka kufa, Enyi nyumba ya Israeli?
Asante kwa references, tito sio nabii ni mhuni flani
 
Kwa hiyo kuna tofauti kati ya siku ya kufa na aina ya kifo ?
 
Back
Top Bottom