Si ajabu, Hawa Nao ni Mafisadi Papa, Kama Sio Nyangumi!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Si ajabu, Hawa Nao ni Mafisadi Papa, Kama Sio Nyangumi!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by NasDaz, May 25, 2009.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280

  Mwana JF, je wewe ni mfanyakazi wa kawaida ambae shughuli zako zinahusu kutoa huduma?! Je wewe ni Dokta(tabibu)? Kuna wagonjwa wangapi ambao baada ya kuwahudumia walikuachia bakshishi kama “ahsante” kwako”!? Je, mgonjwa huyu akija siku nyingine na kukuta foleni, kisha akaingia ofisini kwako bila kukaa foleni; je, utamwambia arudi akapange foleni hata baada ya kukumbusha kwamba yeye ni yule ambae majuzi alikupatia elfu 50? Je, wewe ni Mwalimu Mkuu pale Bunge Pr.?Kuna wazazi wangapi walikuachia ahsante baada ya kuwaandikisha watoto wao katika kipindi ambacho walihisi wasingepata nafasi?! Je, mmoja wa wazazi hawa akija mwaka ujao wakati nafasi zimeshajaa, na kukumbusha yeye ni yule ambae alikupatia elfu 70, bado utakuwa na jeuri ya kumwamabia akamwandikishe mtoto wake hukohuko Mbezi anakoishi?Je, wewe ni Customer Service Personel pale NMB, CRDB au NBC(Kwa mtizamo wangu, hizo ndizo benki zinazoongoza kwa foleni TZ)? Kama ndio, je umeshawahi kukutana na mteja ambae baada ya kumuhudumia akakupa elfu 30 kama ahsante ya kumuhudumia vizuri?! Je, mteja huyo akija siku nyingine akataka ukamchukulie pesa kwenye akaunti yake wakati kuna wateja wengine kwenye foleni, je utamwelekeza nae akapange foleni kama walivyofanya wenzake? (yashawahi kunikuta haya!)! Generally speaking, wengi wa watu wanaotoa “ahsante” wanalenga kutengeneza mazingira ya kupewa upendeleo wa kuhudumiwa kwa siku zijazo! But, all in all; je mnazani mlistahili kupewa hiyo “ahsante?” wakati ulikuwa ni wajibu wenu kutoa huduma (with zero monetary cost)? Umeshawahi kujiuliza uhuru wako wa utendaji unakuwaje pale anapokuja mteja mwenye silika/tabia ya kukuachiachia visenti vya mboga?! Kwa upande mwingine, tuseme (bila shaka ndio ukweli wenyewe) hamna hata mmoja kati yetu aliyestahili kupokea ahsante hiyo, hii haimaanishi tulipokea takrima ambayo tafsiri yake ni kama rushwa tu!!! Endapo ulipokea ile elfu 20 wakati ukiwa daktari, unataka kuniambia utakataa laki 5 kama “ahsante” utakapokuwa daktari wa mkoa? Utakataa milioni 10 kama ahsante kutoka kwenye kampuni iliyoshinda zabuni(kwa njia halali) ya kujenga wodi kwenye hospitali za mkoa wako? Na je, utakapokuwa waziri wa ujenzi, utakataa ahsante ya milioni 50 kutoka kwenye kampuni iliyoshinda zabuni ya ujenzi wa madaraja mahala fulani!! Kumbuka, ulishaona suala la kupewa ahsante ni la kawaida, kiasi cha kuona ni kama haki yako! Je, wewe ni waziri ama naibu kutoka (sema) wizara ya jinsia(kwa upofu wangu nahisi kule hamna ulaji sana!) ambae unakuwa mstari wa mbele kupiga vita mafisadi? Je, wewe ni mbunge ambae hujapata nafasi ya kuwa waziri au mkurugenzi, na kwamba ni mpiga vita mkubwa wa ufisadi? Kama ndiyo, je, mmeshawahi kujiuliza endapo ungepata nafasi kama ya Mramba na Yona wakati ule wa zama za wenye kuhoji kuitwa wana wivu wa kimaendeleo, ungefanya mambo kinyume na alivyofanya Mramba au Yona?! Je, ungekuwa waziri wa nishati wakati uleee wa akina karamagi, je mkataba wa Buzwagi ungegoma kwenda kuusaini ughaibuni?!
  Sina hakika kama nimeeleweka kutokana na huo utangulizi!! Kwa kifupi ni kwamba isije tukajifanya nasi ni wapiga vita wakubwa wa ufisadi kumbe ni kwavile tu hatujapata nafasi ya kufanya deals na mafisadi wa upande wa pili!!! Fisadi wa upande pili, ni yule aliye tayari kuinunua haki isiyo yake (under grand corruption, most likely, these are business people!)! Hofu yangu ni kwamba, si ajabu huyuhuyu aliye mbele leo hii kupiga vita ufisadi kesho akawa ndie fisadi nyangumi ++ endapo atapata nafasi ya kuwa kwenye anga zenye harufu ya mavumba!!! Kama umeshawahi kupokea “ahsante” isiyo stahiki yako wala hautashindwa kupokea ahsante za aina hiyo pale utakapokuwa kwenye level ya decision makers wakubwa nchini! Ongea na nafsi yako kwa kujiuliza, nini ungefanya endapo ungepata nafasi kama ile aliyoipata Mzee wa Vijisenti (kwenye kashfa ya rada)!! Jiulize, je zile dola milioni kadhaa zilizoenda kwa Mzee wa Vijisenti ungeziacha, au ungepata taabu kidogo kufanya maamuzi ya kuzipokea au kutozipokea!! Ukiona unapata kigugumizi kuijibu nafsi yako, basi ninakuomba usiudanganye umma kwa kujifanya nawe unaichukia rushwa!! Iwe siri yako moyoni mwako, kwavile ukipiga kelele kwamba nawe ni mpinga ufisadi tunaweza kukuamini na kukupatia madaraka bila sisi kujuwa kwamba ulikuwa unapinga ufisadi kwavile tu ulikuwa hujapata nafasi itakayoku-expose kwenye grand corruptions!
   
 2. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,086
  Likes Received: 1,733
  Trophy Points: 280  My worry shall always be the capacity of Tanzanians to analyse issues of governance. The submission above is pale although, seemingly, the composer has spent a fortune (time) sribling. Essentially one has to note:

  1. that Tanzania is lacking knowledgeable political leadership (we are governed by civil servants, not leaders);
  2. that Tanzania is lacking a common purpose (state ideology) to shape and guide our national maintream policy (we are empty, refer to Kikwete's addresses to the nation speaking about descrete functions progress status instead of national collective vision achievement/challenges);
  3. that Tanzania is lacking strong governance structures and institutions;
  4. that the above cause grand corruption to flourish;
  5. that grand corruption causes pety corruption (NasDaz discussion above)to flourish; and
  6. that the above have greatly undermined Tanzanians political culture.
  TM
   
Loading...