Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.


Sikuungi mkono kwa kauli zako za kichochezi.Paschal hakukituhumu Chama Cha Mapinduzi wala kuonesha chuki dhidi yake.Paschal ameonesha kukerwa na matukio ya kuhama vyama yanayofanywa na baadhi ya wabunge na madiwani pia suala la kutokuwepo na Mgombea Binafsi wakati kila mtanzania ana haki sawa na uhuru wa kuwa Kiongozi.Suala la hamahama ameliongelea kwa viongozi wote tu akiwemo Lazaro Nyarandu na wengineo.
 
Nimeyaelewa mengi, lakini kaka Pascal Mayala nimekufahamu toka enzi zile upo pale mbezi beach kwenye nyumba yako na Honda lako kubwa...hahaha ila sasa kusema hapa kuwa wewe ni mtanzania mzalendo na hauna chama chochote mh yani kikutokacho mdomoni tofauti na fikra, falsafa na maandiko yako mimi hata nikiamshwa usingizini nikiulizwa Pascal Mayala ana mlengo wa chama gani? NITAJIBU KWA KUJIAMINI your not NEUTRAL.
Cha pili bwana Pascal Mayala hivi unavyosema taifa hili ni masikini UNAMAANISHA NINI?
 
umesahau moja mkuu domokaya .....
.....kama mbunge anajihudhuru kwa kumuunga mkono kiongozi na unaitishwa uchaguzi anagombea tena!

Tu wajinga sana, na tuna ujinga mwingi. Anhalau Nyerere alituwekea misingi ya kuhifadhi Ka utu ketu japo nayo tunaibomoa.

Kama wanazuoni wa fani mbalimbali waliopo timu Simba, Timu yenye karibu nusu ya watanzania wote wanakubali kuwa eti klabu ile thamani ya bilioni arobaini tu. Japo siyafahamu mambo ya mpira, lakini historian tu na jina la klabu ile INA thamani sio tu maradufu Bali Mara elfu ya bilioni arobaini.

Tu wajinga sana sisi, ujinga was kutufanya tuuze nyumba tununue pangaboi.

Wajinga kiasi kila MTU akipendacho in kizuri, wajinga kiasi mhalifu yeyote akituunga mkono anageuka malaika.

Akiwa A, basi wa B kwao atakuwa fisadi na mwizi.
Akienda B basi A kwao atakuwa fisadi na mwizi. Akirudi A anakuwa shujaa, B wanamwita msaliti.

Wajinga sana sisi, na huo ujinga wetu ndio unaotupa haya tuluyonayo.

Wote sisi wajinga, hakuna mwenye afadhali.
 
Hili la kutoruhusu mgombea binafsi linawanufaisha sana CCM na ni moja ya nguzo yao kuu. Ukiruhusu hilo chama kitakufa kesho yake asubuhi.
Nasema walaaniwe majaji waliopitisha maamuzi kwa manufaa yao bila kuangalia maslahi ya taifa huku wakijua ni kinyume cha sheria za kimataifa.
Ila mkuu hongera kwa uzi ulioandika kitaalamu sana.
 
Hitimisho.
Tanzania is too poor spend billions on by elections for foolish and nonsense reasons, nikimaanisha nchi yetu Tanzania ni masikini wa kutupwa, kuhalalisha matumizi ya mabilioni haya ya fedha kuendesha chaguzi ndogo kwa sababu za kuhama vyama. Ili Taifa letu lipate maendeleo ya kweli, ni lazima sisi Watanzania tukubali kuwa wakweli toka ndani ya nafsi zetu, kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa na kufanya siasa za ukweli, tusiukubali huu ujinga wa kuhama vyama, uendelee kutugharimisha sisi masikini wa kutupwa, tunaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, halafu kuendelea kugharimishwa.

Nawatakia Ijumaa Njema.


Paskali
Rejea.
Rev. Mtikila ashida kesi ya kuruhusu mgombea binafsi mahakama ya ...
Mtikila: Shujaa wa Demokrasia, Mwanamapinduzi halisi na Shujaa ...
Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini? | Page 9 | JamiiForums ...

Swali kwa Wana UKAWA: Is UKAWA for Real or Just A Marriage of ...

Pascal Mayalla
pascomayalla@gmail.com[/QUOTE]
Kula like za kutosha mkuu
 
CCM ilishakufa kitambo kilichobaki ni polisi na tume
 

Sheria za kimataifa? Tuone haya kuyazungumzia tusiyoyafahamu. Kujifanya tunajua ndiko kunakotufanya tuwe hivi.

Kama una internet si usome ujiridhishe na upate ufahamu?

Tusilaumu watu wengine, tuko katika hali hii kwa kuwa sisi ndivyo tulivyo!
 
hivi ndiyo vitu vya msingi kabisa ambavyo wanajamvi tunapashwa kuvijadili kila iitwapo leo kwani kwa kurudia uchaguzi sio tu wana siha na kinondoni wanaolipa hizi gharama.
kuna sehemu mpaka leo watanzania hawana maji
kuna sehemu mpaka leo watanzania hawana shule
kuna sehemu mpaka leo watanzania hawana hospital
kuna sehemu mpaka leo watanzania hawana barabara
 

Kuna muda niliwahi kuhoji kama sisi tumefikia kiwango cha kufuata demokrasia ya magharibi. Katika ule mkutano uliofanyika hapa Dar es salaam pale mlimani city. Salim Ahmed Salim alihoji demokrasia ya magharibi mbona haileti maendeleo. Akazitolea mfano nchi zilizoachana na demokrasia ya magharibi na hatua zilizopiga. Watu hawakumtilia maanani.

Demokrasia ya magharibi in ukolini tu kama alivyosema Trump, in mchezo was kijinga sana usio na faida hats punje kwetu.

MTU aingie bungeni kwa gharama, alipwe hela nyingi kama mshahara, aache ubunge, ufanywe uchaguzi was bilioni moja halafu arejee tens bungeni. Huu so uwendawazimu?

Demokrasia ya magharibi haiendani na uwezo wetu was kufikiri, tutafute mfumo utakaotupa maendeleo kwanza demokrasia baadae. Matekani yenyewe kama taifa halikuanza na demokrasia. Iliwachukua kipindi kirefu cha kutumia damu na jasho kupata maendeleo na baadae kufuata misingi ya demokrasia.

Haya maigizo tunayoyafanya hayana tofauti na kuchukua mabunda ya manoti ya mabilioni, kuyamwagia petrol na kuyapiga kiberiti.
 
wanasiasa wa Tanzania hovyo sana ndio maana namshangaa kiongozi wa upinzani akipata nafasi ya kumwuli maswali papo kwa papo waziri mkuu anashindwa kuulia maswali ya maana na pia bado tunaona upuuzi unaojitokeza wa kuingia hasara kwa kurudia chaguzi za ubunge ikiwa tutakazania kuondoa utaratibu wa sasa wa mgombea kudhaminiwa na vyama vya siasa ndio hapo tutakapopata demokrasia ya kweli badala ya demokrasia ya sasa
 
Sheria za kimataifa? Tuone haya kuyazungumzia tusiyoyafahamu. Kujifanya tunajua ndiko kunakotufanya tuwe hivi.

Kama una internet si usome ujiridhishe na upate ufahamu?

Tusilaumu watu wengine, tuko katika hali hii kwa kuwa sisi ndivyo tulivyo!
Hujaona kifungu kilichonukuliwa hapo juu? Au hukuelewa?
 
Akili yako haina tofauti na ya Prof Bana aliesema, katiba mpya haina maana wala sio tiba ya matatizo yetu kwani watawala wanaweza kuivunja wala hatuna la kuwafanya! Nilimsamehe bure kwani najua alikuwa amepanda kuwa profesa hivi majuzi kwa hisani ya CCM.
 
Mahakama ya Afrika Mashariki ilitengua uamuzi wa mahakama ya rufaa na serikali iliahidi kurekebisha katiba kabla ya uchaguzi 2015 na baadae wakasema wataliweka kwenye katiba mpya.
 
paschal

Pascal Mayalla Hivi Katiba inaposema "... kwa kufuata utaratibu uliwekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria" ina maana ngani?? Usitufanye wote humu JF ni nyumbu??!!
 
Ufisadi wa kutisha mlikuwa hampigi kelele
 
Hahaha zamani walikuwa wakituambia pelekeni maoni yenu tume ya katiba. Tume ya katiba ilisheheni maoni ya marekebisho, hahaha wakaweka mpira kwapani kwa hoja kwamba tunataka kuiondoa ccm madarakani na hilo halikubariki.
Waka chagua maoni wayatakayo wao na wakapitisha mapendekezo yao, lakini bado wakakataa kuileta katiba waliyoipendekeza eti siyo kipaumbele chao.
Walitaka mapendekezo ya wananchi hapo hapo wakayakataa.
Paskali hizi kwao ni kelele,fujo na uchochezi. Wanatuhimiza tumuunge mkono mtu wao kwa lazima vinginevyo wewe paskali huo uzalendo unaojivika wanakuvua unaitwa mchochezi.
Wanasema wanatekeleza ILANI ya chama hicho ndio kipaumbele chao, sio kufuata katiba na sheria.
Kinachonifurahisha hadi nicheke ni hiki, wabunge wa upinzani wote na mgombea wa urais wa ukawa wanachukiwa na ccm, lakini wakinunulika eti wanafaa kugombea kwa ticketi ya ccm. Wakiwa wabunge kwa chadema na cuf hawafai bali wakiwa ccm eti vifaa.
Wamshauri Magufuli ajiuzulu alafu lowassa arejee ccm kisha wampitishe agombee urais na wamtangaze awe rais wa Tanzania.
Hahaha wanaufahamu wakutosha mtu wao hafai na wabunge wao hawafai lakini hawataki kukubali kila kukicha wanataka chadema ihamie ccm. Kama wanachadema na chadema nzuri kwanini ccm wote wasijiunge chadema au waunganishe vyama kurahisisha na kupunguza gharama za kuchagua kila siku, what difference will it make?!
Jingine wanalochekesha wanadhani wananchi walichagua watu na sio vyama, hivyo kudhani wakiiba kura na kupitisha aliyekuwa wa chadema au cuf eti hilo wananchi watalikubali,kisa yule yule waliyemchagua akiwa chadema au cuf sasa yuko ccm.
Hahaha no wonder wanatuita wanyonge.
 
Kipimo kiimoja wapo cha Demokrasia ni Uchaguzi Huru na wa Haki 'Independent and Fair Elections'
......Wewe lofa kwa nini unanakili uzi wote kwa hiyo mistari yako mitatu iliyojaa pumba?? Kwani ukimtaja Pasco kwenye new page na kuweka comments huko Lumumba hawatakuewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…