Shuntuma, limbwata hatari katika mapenzi

Shuntuma, limbwata hatari katika mapenzi

Si kwa mama wa Kihaya? Ni maarufu hapo.
Kwa hiyo nikifika matembele ya pili niulizie kwa mama wa kihaya?nikifika niseme nataka shuntama?
Haya imeisha hiyo 😁
 
Kuna wanawake wanawapa wanaume limbwata kuwafanya wawe wajinga
Ile unakuta mama amejiachia bar anakula bia halafu bwana yupo home analea watoto mama anarudi usiku baba anafungua mlango Wala hamuulizi chochote hata amuone na mchepuko.
Hizi zipo vijijini sana
 
Shuntama sio shuntuma, asili yake uhayani huko,, ila sioni haja ya mwanamke kujiingiza huko maana mwisho huwa Ni mbaya na aibu Sana,, ukishindwa kummudu mwanaume kwa uanamke wa kuzaliwa nao muachie kwa walimwengu,
Mods changia kama hizi mnatakiwa kuzi-bold kwa rangi ya Gold hukohuko bila kutushirikisha. Upande wa pili huu upuuzi wa limbwata wanaume tunajiendekeza wenyewe, binafsi hiyo shuntama(kaa) hata iwe onyame(lala) kabisa haifanyi lolote akizingua nazingua double.
 
Mods changia kama hizi mnatakiwa kuzi-bold kwa rangi ya Gold. Upande wa pili huu upuuzi wa limbwata wanaume tunajiendekeza wenyewe, binafsi hiyo shuntama(kaa) hata iwe onyame(lala) kabisa haifanyi lolote akizingua nazingua double.
Kuna wanaume hawarogeki ila nadhani ni wachache,,

tafuteni wanawake wenye utu ndani yao, kwanza hata kuwaza hii sijui niko niko tu siku akipata mtu akamtengeneza huko nje basi atakuwa ameniweza maana ishu za kwa waganga sizijui kabisa

Haina haja ya kumfanya mjinga mtoto wa watu ni uuaji
 
nakubaliana na wewe Noelia, hizo mambo za shuntama sio kwa kila mwanaume zinafanya kazi, na nyingi zinabuma automatically sema wanagumia tu kimyakimya kama mtu mzima aliyebet akapoteza.
 
nakubaliana na wewe Noelia, hizo mambo za shuntama sio kwa kila mwanaume zinafanya kazi, na nyingi zinabuma automatically sema wanagumia tu kimyakimya kama mtu mzima aliyebet akapoteza.
Yeah, matapeli ni wengi ndo pona yenu,, na wapo ambao kwao wana nguvu za kiroho kiasi hawarogeki,, ila ni aibu sana yani
 
Nadhani sio muda wote ni wa masikhara yako,, sina mood na utani wa kipumbavu
Taratibu member wa jf haya mambo hayataki vurugu.. hiyo mood tutaitengeneza tu.. 😂
 
Back
Top Bottom