Pununkila
JF-Expert Member
- Jan 7, 2021
- 689
- 1,692
Kipindi Niko shule ya msingi ,sekondari ,na chuo karibia wanafunzi na waalimu walikuwa na majina ya utani
Nakumbuka mm wakati Niko shule ya msingi walikuwa wananiita mtambo kutokana na kukarua hesabu Sana.
O-level ,likaja jina jingine la mr.president hii ni kutokana na siku moja kuwatetea wanafunzi wenzangu ambao walipewa adhabu ya kufyatua tofali na kung'oa visiki kwa kosa ambalo hawakulitenda. Hili jina lilivuma Sana mpaka walimu wakawa wananiita hivyo kwa hiyo shule ikawa na president na head prefect.
Advance ,nikaitwa katekista hii ni ni kutokana na kusoma shule ya seminary ya wakatoliki huko nikabadilika kabisa muda wote mikono iko kifuani.
Chuo, huko nikaitwa mgiriki Hilo jina lilitokana na kuongoza maandamano ya kudai pesa za kujikimu.
TUELEZE WW WALIKUPA JINA GANI NA KWA SABABU GANI..