kuna mvuvi mmoja alioa mwanamke ambae hakubahatika kusoma, jamaa baadae mambo yakawa super akaamua kuwapeleka watoto english medium school. Kuna cku yule mama alienda kusalimia kwao akamkuta mama yake ni mgonjwa aliporudi akawakuta watoto wamerudi likizo, kesho yake watoto wakaenda matembezini, baadae rafiki yao akawaletea kadi ya birthday yule mama akaipokea na kuuliza ni barua ya nini hii' kale katoto kakajibu ni birthday invitations card na kisha kakatimua. Yule mama aliangua kilio cha kifo mtu hadi majirani wakaitika' kumuuliza kulikoni? Kilichofuata ni kuwatolea ile kadi huku anadai ni barua ya taarifa ya kifo cha mama yake alietoka kumuuguza huko kijijini! Majirani Kufungua, ni kadi ya birthday watu hoi kwa kicheko!!!!