Mkuu, umeeleza vyema lakini kuna point ya msingi umeikosa..
Michango iliyokatazwa ni Ile ya upande mmoja, yaani kutoka shule kwenda kwa wazazi, ile ambayo imetamkwa Na waalimu tu.
Lakini michango ya pamoja, ambayo inatokaa Na majadiliano baina ya waalimu wa wazazi hiyo haijakatazwa..
Wazazi wanatakiwa wachangie kwa hiari kama vile wanavyo changia kwenye maharusi Na sherehe mbali mbali.
Kumbuka, makubaliano baina ya pande mbili yakifikia hitimisho zuri huwa Sheria ambayo imewekwa Na pande hizo mbili.