Shule za selikali za bweni zaanza kufungwa

Shule za selikali za bweni zaanza kufungwa

Mkuu, umeeleza vyema lakini kuna point ya msingi umeikosa..

Michango iliyokatazwa ni Ile ya upande mmoja, yaani kutoka shule kwenda kwa wazazi, ile ambayo imetamkwa Na waalimu tu.

Lakini michango ya pamoja, ambayo inatokaa Na majadiliano baina ya waalimu wa wazazi hiyo haijakatazwa..

Wazazi wanatakiwa wachangie kwa hiari kama vile wanavyo changia kwenye maharusi Na sherehe mbali mbali.

Kumbuka, makubaliano baina ya pande mbili yakifikia hitimisho zuri huwa Sheria ambayo imewekwa Na pande hizo mbili.
Hakuna hiari,wazazi wenyewe ili kuhimizana wanawekeana sheria kuwa ikifikia muda fulani mzazi hajachangia basi mtoto wake hatapata huduma iliyochangiwa na wengine au akamatwe.N.b msimamizi wa sheria ndogondogo za kijiji au kitongoji ni maafisa watendaji
 
Wanasisitiza elimu bure kwa shule za kata lakini wanasomesha watoto wao Tanganyika International kwa mamilioni ya shillingi.
Kweli ujinga wa wengi ndio mtaji wa watawala
Lengo lao watuharibie wanetu,mimi nilikataa kufanya ujinga wa kumpeleka mwanangu shule ya kata,kwani viongozi wetu wamezigeuza uwanja wa siasa
 
Kausheni basi wadau, binafsi nimenufaika sana sana na hii kauli, wanafunz kwenye twition center niliyopo wanafunz wameongezeka kutoka 72 mpk 216 ndan ya nusu wiki, hk ni kiwanda tosha, mapato yamesababisha mshahara kuongezeka mara tatu zaidi. Kutesa kwa zamu mkuu ngoja na wengne wafaid. Sio kila sehem utampinga mkulu, hapa nipo nae 100%
Nimeipenda hii. Kufa kufaana.
Nipe maelezo hao wametokea wapi na tamko lile limesababishaje hao waje tuition centre.
 
Tusitumie mbinu za makinikia kwa kila jambo! Cha kushangaza wao watoto wao wako feza na wanalipa mamilioni
 
Kuna shule ina matundu 6 ya choo kwa watoto 800+ . Wakipata nusu saa ya mapumziko foleni ya watoto kwenye matundu hayo 6 haiishi hadi baada ya saa 1 wakati mapumziko ni dakika 30 na hii inapelekea wengine kukosa vipindi. Je mwalimu mkuu akishauri wazazi wachangie ujenzi wa vyoo kwa manufaa ya watoto wao kuna dhambi gani hapo?
 
Wameelewa vibaya, michango waliyokubaliana wazazi wenyewe wakaweka mpango wa kuchangia haina shida.
 
Mkuu titicombi, wameongezeka kwa sbb walimu wamezuiwa kuchangsha hela za twition nikiwa na maana masomo ya jioni, weekend practicals pamoja na mitihani/tests , this means no twition tena after normal classes ya saa 9 wakitoka, na wazazi wanahtaj watoto waende twition , kwaio inawalazmu watumie twition za nje ikiwemo hii ambayo wameikubali sana. Kumbuka mimi si mmiliki, ila kwa kupitia mmiliki nikaongezewa mshahara zaid ya mara tatu na nusu ya ule wa mwanzo hii ni baada ya yeye kupata wanafunz mara tatu zaid ya mwanzo, na kwa kupitia mimi kuna wengne watafaidika, Hope umeelewa mzunguko wa maisha na mgawano wa riziki usivyo na ubaguzi.
 
Mwalimu kwann hamtaki ubongo wenu kukubali mabadikiko? Huu sio wakati wa wapiga diri kupitia kwa michango ili kuongezea kaposho ka mwezi

Toshekekeni na mishahara yenu sasa maana hapa ni kazi tu, ukija na mambo ya Jakaya utatumbuliwa siku si nyingi.

Sera ya chama tawala ni elimu bure fuateni maelekezo vinginevyo hamtasaidiwa na vipost vyenu vya mitandaoni lazima mkwame tu!

Kama unaona mshahara hautoshi piga chini kazi njoo kitaa uone Mziki wake, we unaona watu tuko bize na shamba mchezo! Serikali imeshasema Elimu bure mengine ni mbwembwe tu.
Mi sio mwalimi nimsomea fani tofauti kabisa lakini pia sio muajiliwa vyeti nimeweka kando
 
Nani kasema hajaelewa? Nimesema aina ya uwasilishaji wa hoja ni mbovu ingawa mleta mada alikuwa na point ya kuifikisha.

Afu isitoshe yeye mwenyewe kakiri kwamba sio mwandishi mzuri. Wkati mwingine bange si mzuri.
Mimi huwa sio wa kubishana manake kama ungekuwa unajua ungeleta uzi kwa kujenga uwezavyo kuliko kuwa mkosoaji zaid
 
MIMI NILICHOELEWA RAIS KAKATAZA MICHANGO KAMA ADA NA ILE ISYO YA LAZMA. MICHANGO ILE ILIYOKUBALIWA KWA RIDHAA YA WAZAZ KAMA CHAKULA NI RUKSA.

ILA MICHANGO KAMA SJUI TUITION, MITIHANI, KARATASI SIJUI, MLINZI, HII IMEPGWA STOP
Kusema michango,michango ni michango haina ufafanuzi, cha msingi shule zingepeleka mahitaji yote ya Jumla ikiwemo na uliyoitaja kwa mamlaka husika ili ishughulikie,
 
Tamko la Rais limepokelewa kwa kasi sana.. Kuna baadhi ya shule zimesimamisha mpaka masuala ya t-shirts kwa wanafunzi.
 
Mbona mnamlisha maneno yenu rais? Kakataa kuwabebesha mizigo wazazi wasitaka kwa kisingizio cha kuchangia, na kama ni hiari yao wapeleke kwa Mkurugenzi wa halmashauri
 
Mleta mada huna lolote!Inaelekea wewe ni kati ya walimu mliokuwa mnanufaika na michango ya wanafunzi.
Mmepewa ushauri wazazi ndio wenye wajibu wa kuji organise na kukusanya michango huku wakiisimamia wenyewe.Ninyi walimu mnataka nini?
Hujui ulisemalo au huna mtoto anayesoma
 
TUKUBALIANE KUTOKUBALIANA,,rais kasema michango shuleni ni MARUFUKU na anayetaka kuchangia aende kwa mkurugenzi,wala hajasema eti wazazi wajioganaizi wenyewe,,,na hiyo ni SERA YA CCM ELIMU BURE,sasa umeipenda,umeichukia,imefanikiwa,au imefeli ni juu yako 2020 utaamua.
 
Ni matokeo ya kudandia hoja za watu bila kuwa na mipango kamili namna ya kutekeleza!!!!!!

Acha tuisome namba......


Biashara ya watu ikiisha ndo tutashughukia hilo!!!!
 
Back
Top Bottom