Shule za sekondari binafsi na mashirika ya dini kufukuza wanafunzi wasiofikia wastani

mwanamapinduko

Senior Member
Jan 24, 2011
178
41
Serikali ilitoa tamko la kuzuia taratibu za shule za binafsi na za mashirika ya dini kuwarudisha nyumbani kwa kushindwa kufikia wastani ambao shule imejiwekea.
Wizara ya elimu itoe tamko kama agizo la swali lilifutwa? Na kama halijafutwa he maafisa elimu wameshindwa kusimamia maagizo ya Wizara?
 
We jamaa vipi? Shule binafsi zinafanya shughuli zake kisheria kabisa kama wanavyofanya wafanyabiashara wengine katika kada nyingine yoyote. Lengo lao siku zote ni kutengeneza faida. Ili kupata wateja wengi(wanafunzi) lazima wapate maokeo mazuri.Unafahamu vizuri kabisa hakuna anayekulazimisha kupeleka mtoto wako shule ya private. Waache wanaoridhika na utaratibu uliopo wasomeshe watoto wao.
 
Kuchujwa ndio mpango mzima...mwanafunzi akishajua kuna kurudishwa nyumban au kuchujwa lazma asome kwa bidii kwa kuogopa aibu hiyo....iendelee tu cz watoto especially wa sasahivI c wa kuwaendekeza ni shule tu utarudia ht mara 5 ..we fatilia shule za serikali baadhi...watoto hawana hofu wanasoma wakijisikia at the end bad results
 
Wenzetu nchi nyingine zinazofanya vzuri kwenye sekta ya elimu mchujo is there to stay. Ni njia mojawapo ya kuwafanya wafocus kwenye masomo.
 
Kwa hiyo mtihani wa kidato cha pili na kidato cha nne ambayo ndio kigezo cha kitaifa cha kuchuja haina maana?
 
Agizo la serikali ni kuwa wanafunzi wanaruhusiwa kukariri darasa wakiwa darasa la nne na form two basi.... Na hili ni agizo kwa shule zote public na private waraka uko!!
 
Waziri wa elimu awashukie, hao wanaotakiwa kusimamia utekelezwaji wa waraka huo. HAPA KAZI TU. Kutafuta faida kufuate taratibu na sheria.
 
BILA MCHUJO WANAFUNZI HAWASOMI KABISA mfano mzuri ni shule za serikali kama shamba la bibi kila mjukuu,
 
Watu hutofautiana uwezo ... Mpeleke mtoto shule itakayoendana na kasi yake. Utapoteza tu milioni twako. Anyways, hata hizo private zinatofautiana wastani. Ila at least apate 50%.
 
Kwa hiyo mtihani wa kidato cha pili na kidato cha nne ambayo ndio kigezo cha kitaifa cha kuchuja haina maana?

Haaaaa weww huo wastani wa 31 sijui 34 nao ni wastani....ukiangalia hiyo ni division four...yn unamtengeneza mwanafunzi asome ili apate D tu...
 
Hiyo kwa tuliosoma makongo tunaita below,yani wastani chini ya hamsini huvuki kidato lazima urudie tu kama hutaki hama shule.Big up sana
Headmaster Lt.Iddi Omary Kipingu
Saini kwenye ripoti yangu bado ipo.
 
Serikali ilitoa tamko la kuzuia taratibu za shule za binafsi na za mashirika ya dini kuwarudisha nyumbani kwa kushindwa kufikia wastani ambao shule imejiwekea.
Wizara ya elimu itoe tamko kama agizo la swali lilifutwa? Na kama halijafutwa he maafisa elimu wameshindwa kusimamia maagizo ya Wizara?

Halitekelezeki fullstop.
 
Maagizo ya kipuuzi yanapaswa kupuuzwa tu haijalishi kayatoa nani.Kuna shule mchujo ni 60% ya wastani wa hadi surprise test,ukipata below 45% kwenu,hakuna kukariri kidato.Na wanafunzi wako serious na shule hakuna upuuzi pale.Huwa zinaitwa,Weka mbali na vilaza.
 
Back
Top Bottom