Shule za Rwanda kutumia internet ya Starlink

Shule za Rwanda kutumia internet ya Starlink

Hakuna mwenye tatizo na DP world ila tuna tatizo na vipengere vya mkataba wenyewe hasa kwenye suala la ukomo
Weshaelezea vizuri vipengele na hata cha ukomo

Shida mnasikiliza walioamua kupinga kila kitu

Tell me ni Kipi lissu aliwahi kuunga mkono

Kuna kundi la waja
 
Wakija hapa mtasema mama kauza nchi

Hebu tuwe wakweli… DP world walipoenda Rwanda tulipongeza Rwanda , kaja bongo tunalalama
Hii nchi ina mijinga mijinga mingi sana jnayojifanya inajua kila kitu kumbe ni bendera fuata upepo tu......iko myeupeeee! Inakera kuikuta mingine ipo humu imeng'ang'ania kujiita great thinkers!
 
Ikiruhusiwa ndani ya miaka hii miwili mje mniite mbwa.
 
Mnataka kitonga cha intaneti kwani mna matumizi nayo.?
 
#SUPATECH: Taasisi ya TonyBlair imetangaza kufanya kazi na serikali ya Rwanda kwa ajili ya kuunganisha huduma ya Internet kutoka katika kampuni ya SpaceX ''StarLink'' iliyopo chini ya Elon Musk.

Mapema mwezi March mwaka huu, Wizara ya Elimu kutokea nchini Rwanda ilianza kwa kuunganisha huduma hiyo kwa shule takribani 50, huku shahuku na nia ya serikali ya nchini Rwanda ni kuzifikia shule 500 ili kuhakikisha kila shule inapata huduma ya Internet.

Kufanikiwa kwa mchakato huu wa ufungaji wa vifaa vya internet kutokea StarLink unategemewa kuleta matokeo chanya kwa uzalishaji wa wabunifu na wavumbuzi alisema waziri wa mawasiliano, teknolojia na uvumbuzi Paulo Ingabire wa nchini Rwanda.

Sasa unaweza kuwa na maswali hii STARLINK ni nini? Kwa ufupi ni huu ni ni mkusanyiko wa mtandao wa setilaiti unaoendeshwa na SpaceX

Faida ambazo zinatofautisha upatikanaji wa Internet wa kawaida ukilinganisha na StarLink

⦁ Inakasi mara tatu zaidi ya mfumo wa kawaida wa Internet, mfumo wa kawaida ni Mbps 100 Lakini StarLink inazidi mpaka kufikia Mbps 300 na hii Mbps ni kifupi cha ''Megabits per second'' ambapo kipimo kidogo zaidi cha kasi ya data ni bits lakini ikiwa kwenye kiwango cha kuhamisha bit Milioni moja ndio huitwa Megabit.

⦁ Urahisi wa gharama ukilinganisha na watoa huduma wengine, kwenye StarLink mtu hulipa kiasi cha Dollar 60 ambayo ni 144,000 kwa pesa ya Tanzania kwa kasi ya MB's 100/10 na kwa mujibu wa wisevoter.com speed ya Internet kwa nchi ya Tanzania ni 22.05 Mbps na kuifanya kuwa nchi ya 150 Duniani kwa kasi ya Internet.

⦁ Upatikanaji wake, Huduma ya StarLink haijalishi wewe unaishi wapi inapatikana popote duniani bila ya uwepo wa changamoto ya upatikanaji wake.

Hasara/ changamoto za StarLink

⦁ Kasi ya Internet kuwa ya kiwango cha chini kwenye miji kwa sababu ya idadi kubwa ya watu kutumia ''bandwidth'' moja kwa pamoja, na kuhusu bandwidth hiki ni Kiwango cha juu zaidi cha data inayotumwa kwenye muunganisho wa internet kwa muda fulani.

⦁ Matawi kwa ajili ya usambazaji wa Bidhaa/Vifaa, Mfano waya wa kisimbuzi ukiharibika ni rahisi kwenda kununua kwa wauzaji madukani lakini StarLink hawana maduka kwa baadhi ya maeneo ikiwa kifaa kimeharibika.

⦁ Changamoto nyinginezo kwenye ukubwa wa kifaa ambao unaleta ulazima wa mtu kuwa sehemu husika ili awezeshwe na huduma tofauti na Internet ya SImu ambayo unakuwa nayo mahali popote.

Chanzo: wisevoter.com, provscons.com, testmanian.com, Techtarget.comView attachment 2664646
Airtel vodacom na tigo wakisikia lazima waomgeze dau kwa nape ahaakikisha iwe jua inyeshe mvua jamaa hakanyagi hapa tz
 
Wakija hapa mtasema mama kauza nchi

Hebu tuwe wakweli… DP world walipoenda Rwanda tulipongeza Rwanda , kaja bongo tunalalama
Shida ni mkataba .DP sio shida mboba unajitoa ufahamu?
Unadhani mkataba wa Rwanda n8 sawa na wa kwetu?
 
Wakija hapa mtasema mama kauza nchi

Hebu tuwe wakweli… DP world walipoenda Rwanda tulipongeza Rwanda , kaja bongo tunalalama
Tofautisha Kati ya Rwanda landlocked country na Tz inchi yenye access ya bahari usikurupuke!. Tz na Rwanda hazilingani
 
Mkuu wacha tumalizie kujenga matundu ya vyoo, madarasa na madawati kwanza. haya ma SpaceX ni anasa.
 
Tofautisha Kati ya Rwanda landlocked country na Tz inchi yenye access ya bahari usikurupuke!. Tz na Rwanda hazilingani
Hii ndiyo akili fupi kabisa… kiko cha Sungura

You didn’t even understand my sentence
 
Kwa kuwa awamu hii ni vilaza hawawezi kuendesha bandari basi wanadhani na viongozi watakaokuja baada ya miaka 30 nao watakuwa vilaza ndiyo maana wanasaini mkataba wa milele!
Nilimuuliza afisa mmoja wa wizara ya habari na mawasiliano kwanini tunasuasua akasema tunataka tujiridhishe kama ni mfumo salama, nikasema kwani hii teknolojia tunayotumia tunauhakika tupo salama kiasi gani akabaki macho wazi
 
Back
Top Bottom