Shule za binafsi zifutwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shule za binafsi zifutwe

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by fikirikwanza, May 21, 2012.

 1. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kwa kuzingatia hali ya mporomoko wa elimu, shule za watu binafsi zifutwe. Shule hizi zimechangia kuua elimu tena bila hata huruma, hawa jamaa wamegeuza elimu ya taifa hili kuwa ni biashara wakti serikali wakiangalia. Waziri wa elimu taifisha shule hizi kwa kuwapa fidia wamiliki.

  Shule zibaki kuwa za mashirika ya dini, taasisi za umma na serikali tu.

  Hebu fikiria wizi wa mithani ni hizi english medium, ada kubwa yaani wizi wa kuaminiwa, elimu duni yaani watoto hawafundishwi kama ambavyo inatengazwa na kuonekana kwa TV, Je mtoto atapata elimu kwa lugha asiyoijua?? as lower as class 1 or 2 at 7&8yrs of age????

  Elimu biashara inamchango mkubwa kwenye kufa kwa elimu TZ, eti mtu anafaulu hajui kusoma wala kuandika haya ni mambo ya elimu biashara. WAZIRI FUTEENI SHULE ZA BINAFSI.

  Nawasilisha
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  mkuu hawajui kusoma wala kuandika ni wanao soma shule za kina kanumba!
   
 3. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,319
  Likes Received: 2,605
  Trophy Points: 280
  Kama jina lako lilivyo mkuu nadhani "ungefikiri" kabla ya kupost hapa jamvini.
  Jaribu kufafanua shule binafsi zinaua vipi elimu na wakati inabidi zifaulishe ili kujitangaza kwa wananchi?
  Wazo la kutaifisha umelifikiria vyema? Huoni kama hili ni gumu kutekelezeka kwa kuwa hizo tu shule chache ambazo serikali ina dhamana nazo inashindwa kuzihudumia ipasavyo!
  Hapa kwenye "...eti mtu anafaulu hajui kusoma wala kuandika..." nimeshindwa kukuelewa maana mitihani yote ya taifa inahusisha kuandika na ili uandike inabidi usome maswali, sasa kweli hata kama kuna uizi wa hiyo mitihani unataka kusema watu huingia na papers ambazo wameshajibiwa! mmh hii sidhani kama inaingia akilini.

  Mkuu mi nadhani ungetoa wazo la serikali kuwa na mamlaka kwa ajili ya kusimamia huduma ya elimu ya msingi na sekondari, kama ilivyo kwa Trca katika mawasiliano au Ewura katika nishati au TCU na NACTE kwa vyuo.
  Hakuna usimamizi yakinifu, zaidi serikali imeweka nguvu kubwa kwenye usimamizi wa mitihani tu kupitia NECTA na kusahau kuwa mitihani ni hitimisho tu la kile mwanafunzi alichoambulia akiwa shuleni.
   
 4. pgasper

  pgasper JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 311
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lowasa anasemaje kuhusu hili
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Zifutwe?? Labda hizo shule hazimilikiwi na watunga sheria!!
   
 6. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2012
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Thubutu!!!!, umetumwa na nani wewe
   
 7. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  ngoja nipite maana ukichangia naweza kujikuta namtukana mleta mada nikaishia kupigwa ban, kwaheri fikirikwanza
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  HAPA penye zinabidi zifaulishe ili kujitangaza kwa wananchi> chanzo kikuu cha wizi wa mtihani maana ni lazima kufaulu ili kupata wateja wengine tena wengi na bei kuwa juu; justification ya kwanza hiyo;

  Ya pili kwa ufupi kabisa, je wewe unaamini elimu inaweza kuwa biashara na bado nchi ikawa na uhakika wa elimu bora??? angalia hata digrii za kibiashara elimu ya juu zilivyo huko india, marekani etc.

  Ni kweli kunauwezekano huo wa kupewa pepa imejazwa; maana siku hizi wala sio watoto wenye jukumu la kuiba mitihani ni shule na mmliki wake; unaona hilo???

  Mkuu fikiria tena, mamlaka harafu niambie ulizotolewa mfano zimefanya nini kwa watz, kula pesa yetu bure; mifano wazi TCRA unatuma sms haiwi delivered hela wanachukua??? kodi mashirika ya simu ndo hayalipi, EWURA wao tena wanataka mgawo kwenye bili zetu maji na tanesco 2%, mafuta ndio yako juu hata hayashuki tangu dola ilipanda hadi 1800 leo imeshuka 1560 bado bei ya mafuta imetoka 1250 iko 2250 bila woga EWURA wanadunda. Kama kila kitu serikali itaunda msimamizi harafu yenyewe ifanye nini??? kama serikali???? tunapotoka na hizi mamlaka. Ukikumbuka skendo la mafuta na EWURA nadhani hutapendekeza uchafu huu, REA wao pia wanapata mgawo kwenye bill niambie wamefanya nini??? mamlaka zipo kibao mzigo kwa WTZ; Kweli unaamini ELIMU inafanyiwa biashara TAALUM itakuwepo?????
   
 9. w

  warea JF-Expert Member

  #9
  May 21, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zifutwe na serikali ipi? ya CCM?
  Kaulize hizo shule zinazoitwa Saint ..... (yaani shule za watakatifu) zinamilikiwa na akina nani! Wabunge wa CC_, wakurugenzi wa serikali ya CC_, mawaziri wa serikali ya CC_, wenyeviti wa taasisi za CC_, wastaafu wa serikali ya CC_, n.k.

  Haziko kwenye orodha ya kampuni za biashara na hawalipi kodi kwa vile ni shule za watakatifu ..... ingawa ada zake ni kuanzia 1m kwa mwaka na kuendelea hata kama ni za chekechea.
   
 10. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #10
  May 21, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Labda nimeiwahisha mada, subirini mtakuja kuniunga mkono muda ukifika. Elimu inafanyiwa biashara leo tunalalamika eti elimu imeshuka??? mfanyabiashara faida mbele ulitegemea afanye nini? shule za kata ni special case; hazina walimu wala sitaki kuziongelea maana ipo siku walimu wakitosha tatizo litakwisha, dwindling return; Sasa Elimu na Biashara tatizo linakua kila siku, kama umaskini wa mtz. HILO NI BOMU; labda kama mnafurahi kuwa na vyeti bila taaluma.
   
 11. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #11
  May 21, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  HII NDO inatutafuna, wakubwa ndo wamiliki wa hizi shule-ZINAUA JAMII KIELIMU harafu hakuna la kufanya. Kama kiingereza ni elimu basi ziendelee; lakni ukweli ni JANGA mtoto anajifunza kwa lugha ngeni eti atakuwa thinker au claimer wa mambo tangu mtoto tunaviona zinakariri, leo hatuoni madhara ya hili; nchi zote zilizoendelea zinafundisha kwa lugha ya mama walau kwetu kiswahili nyerere alikifikisha pazuri tungetumia hadi University.
   
 12. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #12
  May 21, 2012
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Lipo la kufanya.
  Kwanza tusipinge kama kiswahili au kiingereza ndio kitumike kutoa mafunzo, nyuzi nyingi hapa zimesha'discuss hilo swali au tatizo lenyewe ni ACCESS ya hiyo elimu. Bila kutoa judgement kuwa private schools wanatoa elimu nzuri au kuwa wanaiba mitihani na kuwa na pass rate kubwa, inabidi tu ujiulize kweli elimu pale inapatikana? Nadhani utagundua kuwa nyenzo za kutimiza ahadi ya elimu wanayo, walimu, vitendea kazi n.k.

  Lakufanya ni lipi? Hatutoendeleza elimu bila sisi wakereketwa kuwa mstari wa mbele kuishinikiza serikali kufanya kweli kwenye sekta hii, lakini pia, wazazi na walezi inabidi watoe mchango wao katika kuendeleza elimu. Tukumbuke, kuwa sio pesa peke yake itatatua tatizo lenyewe, wazazi/walezi inabidi kujua na kufuatilia kwa umakini elimu watoto wao wanayopata na hapo labda patakuwa na mabadiliko. Tusi'lalamike tu wakati matokeo yanatangazwa kuwa failure rate imepanda, lakini kila siku tujiulize, hawa watoto wanapotoka kwenda shule, je wanaambulia nini?!

  Je elimu ni biashara? Ndio, na maudhui ya biashara sio tu kupata faida, kama mzazi unampeleka mwanao shule X kwani inatumia ST Fulani bila kujua kwa undani kama kweli mwanao atapata elimu, wewe ndio wakulaumiwa, wewe ndie unaharibu hiyo biashara na kuwafanya wamiliki wasiwe na changamoto kuendeleza elimu bali tu kukupa a pass rate ya uongo na kweli, Wazazi wakifuatilia na kujua nini kinacho fundishwa na value yake, basi elimu itolewe na serikali au watu binafsi hapo elimu itakuwa na manufaa.
   
 13. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #13
  May 21, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  st. Kayumba ndo zinazalisha watoto wasiojua kusoma na kuandika
   
 14. w

  warea JF-Expert Member

  #14
  May 21, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Elimu ni haki ya kila mtoto!
  Watoto wote wanapaswa kupewa elimu ya kuwasaidia kujitegemea na kuchangia uchumi wa nchi.
  Tatizo lililopo ni serikali kuacha mamlaka ya kusimamia elimu na kuruhusu wachache kuchukua nafasi hiyo kujinufaisha.
  shule za serikali zimeachwa ili shule za binafsi zipate soko?
  Kinachotakiwa:
  Shule za serikali ziwepo na zitoe elimu inayostahili kumsaidia mtanzania.
  Shule za binafsi ziwepo kwa wenye uwezo na ziendeshwe kibiashara. zilipe kodi kama biashara zingine!
  Huku kujificha kwenye kivuli cha St. english medium wakati ada tunazotozwa ni za kibiashara ni kuliibia taifa kodi.

  Suala la mzazi kumkazania mtoto ili afauli vizuri zaidi sio tatizo la kitaifa, hilo ni la mtu binafsi. Watoto wakifundishwa vizuri shuleni watajua kusoma na kuandika hata bila mzazi. Sasa wewe unayetaka mtoto wako afanye vizuri zaidi ndio ufanye juhudi binafsi.
  kinachotakiwa ni hata yule mtoto ambaye wazazi wake hawakufanikiwa kupata elimu au hawapo nao wapate nafasi ya kusoma kwa vile nao ni watanzania na wana haki.
  Tusisahau kuwa ni asilimia ndogo sana ya watanzania wana elimu zaidi ya sekondari.
   
 15. k

  kotinkarwak JF-Expert Member

  #15
  May 21, 2012
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 386
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inabidi tuanze kuangalia njia mbadala wa kutoa elimu kwani sioni kama kweli nia au uwezo upo kutoka serikalini kuiboresha elimu ipasavyo. Kama ni haki, basi mashitaka yatolewe kwa wote wenye jukumu la kutoa hiyo elimu lakini sioni kama shutumu tu zitasaidia ishu yenweye kwani ni nzito sana.

  Serikali + Mzazi + Mwalimu + Mwanafunzi + Viwanda = Elimu.

  Ndio simaanishi kuwa hizo +'s ndio peke yake zinazohitajika, lakini amini kuwa, bila ya hiyo combination, elimu inayotolewa haitakidhi mahitaji.
  Mzazi na Mwalimu kwani wao ndio wapo karibu na mwanafunzi mwenyewe wanajukumu la kujua kama kweli hayo manufaa yanayotangazwa kuwa ni matunda ya elimu kweli huyo mtoto anayapata. Sidhani kama hili liwe ni "best effort" ya mzazi bali ni "a must effort" kwani bila kujali hili hata serikali ikitoa 100% education, wanafunzi watazidi kufeli...
   
 16. The_Emperor

  The_Emperor JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 884
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mabadiliko ya kweli hayaletwi kwa njia ya mapinduzi,suala hapa ni kuboresha mazingira ya hii sekta muhimu!Una uhakika gani kama shule za serikali zinaweza kuchukua wanafunzi wa nchi nzima!?
   
 17. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Tatizo hapo liko ktk namna mbili, moja wizi wa mitihani hautapungua kama hizi english medium zinashindania wateja na ukweli kwamba ni mpango wa kibiashara ambapo faida kubwa ni mafanikio

  Mbili, iweje serikali ishindwe kutoa haki ya elimu kwa kila mtoto na kuwapa watu binafsi bila kuzingatia madhara tajwa ktka hoja ya kwanza, na kwamba kupitia shule hizo tunajenga taifa lenye matabaka ktu ambacho kitairudisha nyuma tz ktk maendeleo yake na vita dhidi ya matabaka ndani ya jamii. Yaani suala hili linatishia usalama wa taifa hili.

  Nimesema zifutwe na pia nimesema kwa maana ya kutaifishwa ili ziwe za serikali na wenye nazo walipwe fidia wasepe; kwa maana hiyo hakuna shule itakayopungua zote zitabaki na watoto wote watapata nafasi kama ilivyosasa. Cha msingi tu ownership ya shule ibadilike kuwa umma/serikali.
   
 18. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Kumbe hoja ni kuwa viongozi wetu ndo wako mstari wa mbele kuharibu ustawi wa taifa letu, ndo maana ya hoja ya mapinduzi katika sekta ya elimu wala sio mabadiliko na kuongeza usimamizi; tufute elimu biashara tubakize elimu huduma kwa jamii. Wananchi hasa wa chini kama mnaliona hilo kwa moyo wa dhati, lazima tutoke mbele kupigania udhalimu huu wa viongozi; vinginevyo tabaka la watawaliwa ndo saizi ya maisha yetu; tufanye kazi kwa manufaa ya watawala sio nchi
   
 19. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Ukweli ni kwamba lazima matatizo yetu tuyajadili sisi wenyewe; shule za binafsi kweli zinatoa kile kinachohitajika na taifa??? au mwanya mwingine kwa wazazi kuibiwa??? pesa nyingi elimu kidogo wizi wa mitihani unakomaa. Je kunafaida gani kitaifa mtoto kupata div 1 ile hali ni mweupe katika masomo; yaani anapata div 1 kukoleza biashara baada ya mmliki au mwenye dhamana kama headteacher au master wa shule kufanya mambo??? SERIKALI IKO WAPI JAMAANI mbona kodi zetu mnachukua??? Tumwambie nani???
   
 20. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #20
  May 28, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Unashangaa zero na 4 kwa shule za watoto wenye vipaji maalum? hiyo ni kutokana na uchakachuaji ngazi walizotoka, siku hizi kuchakachua na kufaulisha sana ni sifa ya kumuongezea mtu idadi ya wanafunzi na hivyo mapato. Utashangaa mengi na huu utitiri wa shule binafsi za wafanyabiashara ambao hela ni kwanza mengine yote baadaye.
   
Loading...