kotinkarwak
JF-Expert Member
- Aug 5, 2010
- 376
- 114
Unashangaa zero na 4 kwa shule za watoto wenye vipaji maalum? hiyo ni kutokana na uchakachuaji ngazi walizotoka, siku hizi kuchakachua na kufaulisha sana ni sifa ya kumuongezea mtu idadi ya wanafunzi na hivyo mapato. Utashangaa mengi na huu utitiri wa shule binafsi za wafanyabiashara ambao hela ni kwanza mengine yote baadaye.
Tujiulize, elimu bora gharama yake kiasi gani?
Elimu bora, mwanafunzi anatakiwa kuandaliwa vipi kuimudu ngazi hii ya elimu...
Elimu bora, nani mdhamini wake, mzazi/mlezi, shule (education provider) na Serikali/Mzazi (financial provider), mwanafunzi (Anayeandaliwa kielimu), mwajiri/Ujasiriamali (Mtumiaji)
Je soko linahusishwa kujua ni product ipi inatoka mashuleni (wana-ICT, ma-engineers, Doctors, Nurses etc etc)
Mzazi anafuatilia uelewa wa mwanafunzi?
Mzazi/Serikali inaweka mazingira ya elimu sawa?
Mwanafunzi anachukua fursa zilizopo kujiendeleza mwenyewe?
Mzazi ana'invest hali na mali kumuwezesha mwanae apate elimu bora au ya mkato?
Haya ndiyo kati ya maswali tunahitaji kujiuliza na sio tu kuona uozo uliongia kwenye sekta ya elimu. Wamiliki wa haya mashule watazidi tu kukusanya hayo mapesa kama wahusika hawatajishughulisha kujua nini kunachotolewa pale kielimu.
Mfano, tukubaliane kuwa elimu bora gharama yake ni 500,000 TSH kwa mwaka, shule ina wanafunzi 500, je shule inaweza kuendeshwa kwa mil 20.8 kwa mwezi? Shule za serikali, gharama yao kwa mwanafunzi mmoja kwa mwaka ni kiasi gani?
Je wazazi wenyewe wanaweza kuanzisha shule ambayo uendeshaji wake hautakuwa wa kukimbilia profit bali education profit?
Maswali ni mengi sana jamani...