Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 15,322
- 11,192
Shule yafungwa kwa kukosa walimu
2007-10-26 09:23:56
Na Mohab Dominick, Maswa
Shule ya sekondari ya Binza ya wilayani Maswa Mkoani Shinyanga imefungwa kwa muda kutokana na kukumbwa na upungufu mkubwa wa walimu.
Habari kutoka shuleni hapo zinasema kuwa shule hiyo ya serikali ilijikuta imebaki na walimu watano, hali ambayo ilisababisha? wanafunzi wa shule hiyo kutofundishwa kwa muda wa wiki mbili.
Wakizungumza na waandishi wa habari shuleni hapo? wanafunzi hao walisema shule hiyo imefungwa kwa muda? hadi Oktoba 22? itakapofunguliwa.
Rebeka Kiselya anayesoma kidato cha? pili? katika shule hiyo? alisema tatizo? la kufungwa kwa shule hiyo limewaathiri sana? kwa kuwa wanategemea kufanya mitihani wa taifa mwishoni mwa mwezi huu (Oktoba 31).
`Sasa hivi tuko majumbani tu, lakini ikifika jioni ndipo tunakuja hapa shuleni kujifundisha wenyewe,` alisema akionyesha masikitiko.
Naye mwanafuzi? wa kidato cha tatu, Majura Thomas,? alisema kufungwa kwa shule hiyo? kumewakatisha tamaa ya kuendelea? na masomo katika mtiririko unaotakiwa.?
`Sisi tunaiomba serikali na wizara itusaidie kutupatia walimu wa kutosha ili tupate masomo wakati? wote,` alisema Majura.
Hivi karibuni, wanafunzi? hao waliandaa maandamano? ili kwenda kuonana na Ofisa Elimu wa wilaya hiyo, lakini wakatakiwa kusitisha maandamano yao kwani bodi ya shule ingekutana kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo, lakini walisema hadi sasa hakuna kinachoendelea.
Shule hiyo yenye wanafunzi hadi kidato cha nne, ina mikondo 16. Walimu waliobaki shuleni hapo ni ni? Mkuu wa shule, Bw. Simon Mwombeki,?msaidizi wake Bw. Julius Danga, Bi. Meryciana Mganga na waliotajwa kwa jina moja moja, Mwalimu Kisusi na Mwalimu Jumanne.
Imeelezwa kuwa baadhi ya waalimu wapo masomoni huku wengine wakiwa wamepewa ukuu wa shule za kata.
Hata hivyo, wanafunzi hao walisema dhamira yao ya kuandamana kuonana na viongozi wa wilaya bado iko palepale na kwamba watatekeleza hilo baada ya kukubaliana wote kwa kuwa baadhi yao hawapo shuleni.
Mkuu wa shule hiyo, Bw. Mwombeki alisema kwa kifupi kuwa hawezi kuongelea suala hilo katika vyombo vya habari.
`Matatizo yaliopo yatajadiliwa katika vikao vya bodi ya shule au katika baraza la shule. Nakuomba uende kwa ofisa elimu?ndiye mwenye uwezo wa kuongelea tatizo lolote la shule,` alisema.
Kaimu Ofisa elimu wa wilaya, Bw. Martin Mahinda pamoja na Mratibu wa shule za Sekondari wilayani hapa, Bw. Peter Sinaga, walisema hawana taarifa za kufungwa kwa shule hiyo na kuahidi kulifuatilia suala hilo.
`Tutafuatilia suala ulilotueleza. Ikibainika ni kweli tutachukua hatua stahili,` alisema Bw. Mahinda.
SOURCE: Nipashe
Wana JF wenzangu, tatizo hili la ukosefu wa walimu limekuwa sugu sana hapa nchini, kutokana na kujengwa shule nyingi za sekondari za kata bila kuwa na walimu wakutosha kukidhi mahitaji ya shule hizi.
1. Shida iko wapi?
2. Tuendelee kujenga shule hizi za kata?
3. Tufanyeje kutatua tatizo hili?
4. Kama mwana JF, mchango wako ni upi katika kutatua tatizo hili?