Shule yafungwa kwa kukosa walimu

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,963
10,460
Shule yafungwa kwa kukosa walimu

2007-10-26 09:23:56
Na Mohab Dominick, Maswa


Shule ya sekondari ya Binza ya wilayani Maswa Mkoani Shinyanga imefungwa kwa muda kutokana na kukumbwa na upungufu mkubwa wa walimu.

Habari kutoka shuleni hapo zinasema kuwa shule hiyo ya serikali ilijikuta imebaki na walimu watano, hali ambayo ilisababisha? wanafunzi wa shule hiyo kutofundishwa kwa muda wa wiki mbili.

Wakizungumza na waandishi wa habari shuleni hapo? wanafunzi hao walisema shule hiyo imefungwa kwa muda? hadi Oktoba 22? itakapofunguliwa.

Rebeka Kiselya anayesoma kidato cha? pili? katika shule hiyo? alisema tatizo? la kufungwa kwa shule hiyo limewaathiri sana? kwa kuwa wanategemea kufanya mitihani wa taifa mwishoni mwa mwezi huu (Oktoba 31).

`Sasa hivi tuko majumbani tu, lakini ikifika jioni ndipo tunakuja hapa shuleni kujifundisha wenyewe,` alisema akionyesha masikitiko.

Naye mwanafuzi? wa kidato cha tatu, Majura Thomas,? alisema kufungwa kwa shule hiyo? kumewakatisha tamaa ya kuendelea? na masomo katika mtiririko unaotakiwa.?

`Sisi tunaiomba serikali na wizara itusaidie kutupatia walimu wa kutosha ili tupate masomo wakati? wote,` alisema Majura.

Hivi karibuni, wanafunzi? hao waliandaa maandamano? ili kwenda kuonana na Ofisa Elimu wa wilaya hiyo, lakini wakatakiwa kusitisha maandamano yao kwani bodi ya shule ingekutana kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo, lakini walisema hadi sasa hakuna kinachoendelea.

Shule hiyo yenye wanafunzi hadi kidato cha nne, ina mikondo 16. Walimu waliobaki shuleni hapo ni ni? Mkuu wa shule, Bw. Simon Mwombeki,?msaidizi wake Bw. Julius Danga, Bi. Meryciana Mganga na waliotajwa kwa jina moja moja, Mwalimu Kisusi na Mwalimu Jumanne.

Imeelezwa kuwa baadhi ya waalimu wapo masomoni huku wengine wakiwa wamepewa ukuu wa shule za kata.

Hata hivyo, wanafunzi hao walisema dhamira yao ya kuandamana kuonana na viongozi wa wilaya bado iko palepale na kwamba watatekeleza hilo baada ya kukubaliana wote kwa kuwa baadhi yao hawapo shuleni.

Mkuu wa shule hiyo, Bw. Mwombeki alisema kwa kifupi kuwa hawezi kuongelea suala hilo katika vyombo vya habari.

`Matatizo yaliopo yatajadiliwa katika vikao vya bodi ya shule au katika baraza la shule. Nakuomba uende kwa ofisa elimu?ndiye mwenye uwezo wa kuongelea tatizo lolote la shule,` alisema.

Kaimu Ofisa elimu wa wilaya, Bw. Martin Mahinda pamoja na Mratibu wa shule za Sekondari wilayani hapa, Bw. Peter Sinaga, walisema hawana taarifa za kufungwa kwa shule hiyo na kuahidi kulifuatilia suala hilo.

`Tutafuatilia suala ulilotueleza. Ikibainika ni kweli tutachukua hatua stahili,` alisema Bw. Mahinda.

SOURCE: Nipashe

Wana JF wenzangu, tatizo hili la ukosefu wa walimu limekuwa sugu sana hapa nchini, kutokana na kujengwa shule nyingi za sekondari za kata bila kuwa na walimu wakutosha kukidhi mahitaji ya shule hizi.
1. Shida iko wapi?
2. Tuendelee kujenga shule hizi za kata?
3. Tufanyeje kutatua tatizo hili?
4. Kama mwana JF, mchango wako ni upi katika kutatua tatizo hili?
 
Ni kuwa hizi program za MEM na MEMKWA I dont know their names zilitakiwa ziende sababa. wakati unaongeza madarasa primary school unaongeza sekondary school unaongeza na hata vyuo. Wakati huo huo unaandaa miundombinu ya shule. Shule sio majengo tuu hata chini ya mti kama unawalimu na vitabu ni shule. Sasa tunakimbizana na madarsa wakati hamna walimu na vitabu. Tunakimbizana na quantity na sio quality a elimu. Wezetu wa Kenya wanawaalimu wengi kuliko mahitaji, you know what! mwalimu wa kenya anakula kama laki saba wakati wataanzania wanakula elfu 80. Hamna nyumba za waalimu etc etc etc.
 
Mpaka hapo Serikali itakapotambua umuhimu wa Elimu, vinginevyo tutaendelea kushuhudia elimu yetu viwango vikishuka siku hadi siku.................na kwa maana hiyo tutaendelea kuibiwa kila kukicha ktk maliasili zetu
 
i kuwa hizi program za MEM na MEMKWA I dont know their names zilitakiwa ziende sababa. wakati unaongeza madarasa primary school unaongeza sekondary school unaongeza na hata vyuo. Wakati huo huo unaandaa miundombinu ya shule. Shule sio majengo tuu hata chini ya mti kama unawalimu na vitabu ni shule. Sasa tunakimbizana na madarsa wakati hamna walimu na vitabu. Tunakimbizana na quantity na sio quality a elimu. Wezetu wa Kenya wanawaalimu wengi kuliko mahitaji, you know what! mwalimu wa kenya anakula kama laki saba wakati wataanzania wanakula elfu 80. Hamna nyumba za waalimu etc etc etc.

Nashangaa tunaweka vipaumbele katika mambo ambayo si lazima sana, badala ya kutoa vipaumbele kwa elimu na afya. Hali kadhalika ni upuuzi kujali uwingi badala ya ubora. Sijajua sirikali itazinduka lini kutoka katika usingizi huu.
 
Jamani inasikitisha kweli, Mimi nipo tayari kujitolea ktk shule hiyo kufundisha, nipo Dar es salaam, mimi ni mwalimu wa masomo ya chemistry na geography lakini pia nafundisha biology kama kunakua na uhitaji pia, namba zangu za simu ni 0786140534 na 0766326628, naomba jamani niunganisheni na uongozi wa hiyo shule nipate mawasiliano nao ili nikaokoe jahazi, nipo siriasi ndugu zangu, hili ni janga la kitaifa, ahsanteni
 
Jamani inasikitisha kweli, Mimi nipo tayari kujitolea ktk shule hiyo kufundisha, nipo Dar es salaam, mimi ni mwalimu wa masomo ya chemistry na geography lakini pia nafundisha biology kama kunakua na uhitaji pia, namba zangu za simu ni 0786140534 na 0766326628, naomba jamani niunganisheni na uongozi wa hiyo shule nipate mawasiliano nao ili nikaokoe jahazi, nipo siriasi ndugu zangu, hili ni janga la kitaifa, ahsanteni
Mwalimu umezingua huu uzi wa 2007 almost miaka 10 sasa... Hivyo basi hiyo shule ina walimu wa kutosha sasa
 
Back
Top Bottom