Shule ya wasichana Ruvu imekithiri ukabila na ubabaishaji

Shule ya wasichana Ruvu imekithiri ukabila na ubabaishaji

Wabongo bwana mtu anasema ukwel mnamponda dah!

Unatetea ubwegg ? Kwani anaogopa nini kutaja majina tuifanyie taarifa kazim Yeye anajificha wenye sketi ya mashangingi sisi tumtafunie ? acha umtetea bbwwegge
 
Huyu nae kawaza kweli kweli....anaweza kua na hoja nzuri ila uwasilishaji ndo zero,maana ukabila wa kuonekana muda taa zinawaka ni balaa...Au kila taa zinakabila atuambie.
 
Hii ni shule kongwe kwa wanaoifahamu. Ilikuwa na sifa nyingi miaka ya nyuma. Nakumbuka miaka ile ya mwanzoni 1990 wakati natokea mazengo-high school na kufika maeneo hayo muda wa saa mbili sa usiku na kuona taa zikiwaka kutoka katika jengo hilo. Kwa kweli miaka ile ilikuwa ni ruvu kweli. Hapakuwa na chembe ya ukabila wala walimu/wanafuzi kubaguliwa.

Kwa hakika ilikuwa na maendeleo makubwa kitaaluma. Kwa sasa ni tofauti. Kuanzia mkuu wa shule, walimu wa miradi, makamu wake, muhasibu pamoja na mwalimu wa taaluma ni wa kabila fulani. Mwalimu mkuu alitakiwa kustaaafu kwa mujibu wa sheria lakini mpaka sasa bado yupo. Inasikitisha kuona baadhi ya walimu wa kabila fulani wanafika shuleni mara moja kwa wiki na wanaichi mbagala!. Matokeo ni mabovu ukabila umeimaliza kabisa shule kana kwamba hakuna wasimamizi. Ingekuwa miaka ile ya 1980 au 1990 yasingetokea hayo.

Pesa za miradi mpaka ada za shule zinaliwa kiolela inawafanya wanafunzi waishi maisha magumu na kula kijimlo. Masikini Ruvu girls sio ile ya niliyokuwa naifahamu

wewe ni mwalimu mpika majungu first class!! yaani mkuu astaafu kwa mujibu wa sheria? unamfahamu? ni mdogo kwangu na mimi nastaafu 2025, sasa piga mahesabu utajua MAMA MINDE ATASTAAFU BEYOND 2025.Mijitu mingine kwa uongo!!
 
Unasema shule imeshuka kitaaluma,nimeingia kwenye web ya wizara nahaya ndio matokeo yk one22,two40,three 106,four40,zero6.

hapo umemmaliza na umbea wake. kwa hali ilivyo hapo wanafunzi 22+40+106 =168 wanaenda kusoma vyuo vya elimu ya juu. big up kwa uongozi wa hyo shule. mleta mada analeta ukabila tu hapa. OVER!
 
Mtu analeta fact watu wanaanza kutetea ujinga ndo maana wanasiasa wanaiba pesa za nchi nmekaa kimya kisa mbasubiri ushahidi....mtasubir mpaka yesu arudi

unazijua facts wewe au umekurupuka usingizini. kama hizo ni facts na umezielewa embu tuambie ni kabila gani linalozungumziwa hapo. embu rudi kulala
 
wachaga wanawapa stress sana, hamuwapendi mpaka kaburini, mchaga anakupa stress pale Kilimanjaro na bado anakupa stress pwani, dah hii ni hatari, ukiona hivyo ujue una matatizo mpaka kwenye unyayo,wai ngileketya kyo
 
ILA kwa sasa upendeleo wa kikanda, kikabila, kidini, kindugu, kirafikia, kuhujumiana watumishi kwa umma, ni jambo la kawaida. Na wakati mwingine wanawatumia madiwani kuwahujumu watumishi wenzao ili kufanikisha malengo yao.
Nadhani vyombo vinavyofuatilia utendaji kwa watumishi hasa USALAMA WA TAIFA wanatakiwa kuliangalia hili, vinginevyo watu ambao wana sifa na hawana fedha na ni wasomi na wako ktk utumishi wa umma wataendelea kunyanyasika.
 
...Mwalimu mkuu alitakiwa kustaaafu kwa mujibu wa sheria lakini mpaka sasa bado yupo. ...
Mimi nilijuavyo mtumishi wa umma akifikisha umri wa kustaafu basi automatically payroll haisomi jina lake, na wala hakuna sababu ya kumlaumu; pengine anajitolea!
 
nakumbuka miaka hiyo nasoma Ruvu ikiwa mixture kama leo ina mambo hayo ni matatizo ya sector karibia zote nchini hakuna uwajibikaji , rushwa, fitina, uvivu ndio uliojaa
 
Back
Top Bottom