Shule ya msingi ulienda kwa style ipi?

Shule ya msingi ulienda kwa style ipi?

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,069
Reaction score
34,839
11953061_1309913752356373_3983563914328452439_n.jpg



Shule ya msingi ulienda kwa style ipi?

(1) Baiskeli
(2) Daladala
(3) UDA
(4) Miguu
(5) Skul bus
(6) Gari la baba
 

Attachments

  • Usafiri wa shule.jpg
    Usafiri wa shule.jpg
    45.8 KB · Views: 977
school bus niliionja kama miaka 2 hivi, mzee alipofirisika nikatupwa kijijini nikawa naenda kwa miguu miaka 5.
maisha yanabadilika muda wowote.
 
Nilikuwa napiga mguu aisee...tena zile shule za kubeba msosi wako..maana kutoka ni saa kumi na nusu jioni....iyo ilikuwa ni Butundwe geita huko...shule ya msingi Luhua
 
mbona hujaweka ya sisi watoto wa kishua. Tumesoma boarding London, sasa wewe unafikiri kutoka bongo tuliendaje shule London ( sio mimi lakini)
 
daah nilianza shule na daladala toka manzese mpaka magomeni mikumi mpaka namaliza la saba, nilikuwa napewa 150 tu ya cku nzima, nauli 100, hamsin kwenda hamsin kurudi, hamsin ya kutumia mpaka namaliza la saba....
 
Namba 6 na baadae 3 & 6 enzi za mwalimu
 
Miguu tena mbio kutoka chumbani hadi shule
 
nilisoma South afrika from grade one to 11 na baadae tertiary university elimu ya bongo siijui.ila baba na mama wanatoka bongo
 
Nilikuwa napiga mguu aisee...tena zile shule za kubeba msosi wako..maana kutoka ni saa kumi na nusu jioni....iyo ilikuwa ni Butundwe geita huko...shule ya msingi Luhua
Asubuhi had kumi na nusu shule ya msingi mlikua mnasoma nini mkuu,sisi darasa la kwanza na la pili tulikua tunatoka saa 5 tu, la tatu na la nne tunaingia saa 4 tunatoka saa9, darasa la tano hadi la saba tunaingia saa 1 na nusu tunatoka saa 8 mchana.
 
Back
Top Bottom