Ndugu, Wanyakyusa hawatokei Chunya. Chunya wanaishi Wabungu na Wasafwa. Hilo ni jina la ukoo huko Chunya kama ilivyo ukoo wa Senge huko Singida
Nahisi kwa kikwao huku inamaanisha vingine ila kabla ya kuipa shule jina unatakiwa ugoogle kupata maana nyingine ya hilo jina kwa kiswahili lugha ambayo ni ya watanzania wengi. Kuna maneno mengine ya kikabila ni matusi makubwa kwa kiswahili mimi niliwahi kusoma na msichana wa kisukuma anaitwa kuhuma ilibidi tumpe nick name
Kwahyo kuna mtu anaweza kuitwa John Shoga
dah Tanzania ni zaid ya uijuavyo.. hivi kwel watu wamekaa weee wameumiza vichwa weee wakaamua kuiita SHULE YA MSINGI SHOGA!! soon utaskia bahsha high school
Tatizo mnabeba tafsiri ya Kiswahili kwa jina la Kibungu! Ni makosa. Waulize wanaotoka Chunya Mbeya, maana ya jina hilo.
Haswaaa. Au akaitwa Shoga Tito n.k. Wala haina tofauti na ukoo wa Mbo.ro kwa Wachagga.
Nimepigwa butwaa kukuta shule inaitwa hilo jina la SHOGA hasa ukizingatia mkanganyiko wa kimaadili unao ikumba nchi yetu kwasasa kutoka na kushamiri kwa vitendo vya Ushoga. Nashauri wizara ya Elimu ione umuhimu wa kubadilisha jina la shule hiyo.
View attachment 169131
kagera kuna mto ngono.mkuu wa mkoa masawe aliwambia wananchi wa uko hapendezwi na ilo jina na wao wakamjibu hawapendezwi na jina la masawe maana ni tusi pia