Shule baada ya Corona

fakhbros

JF-Expert Member
Sep 14, 2013
338
550
Baada ya kufunguliwa kwa shule za msingi na secondary wizara ya elimu imetoa muongozo wa kuongeza muda wa masomo katika shule na vyuo mbalimbali nchini

Jambo la kuongeza muda wa kujifunza ni jambo jema kabisa lakini changamoto ni uamuzi huo kutolewa pasina kuzingatia mazingira halisi ya upatikanaji elimu nchini

Kwa mazingira ya mijini na vijijini kuongeza muda wa kujifunza kutoka saa 8:00 hadi saa 11:00 hili nitatizo kwa wanafunzi waishio mbali na maeneo ya shule

Kuna maeneo nchini mwanafunzi hutembea zaidi ya kilometre tano mpaka kumi kuifata shule hasa katika maeneo ya vijijini ambako hakuna usafiri wa aina yoyote zaidi ya kutembea kwa miguu kwa umbali mrefu na kwa masaa mengi kabla ya kuifikia shule'

Ongezeko la masaa mawili lingezingatia pia usalama wa mwanafunzi hasa mtoto wa kike ambae yupo hatarini zaidi

Serikali kupitia wizara ya Elimu badala ya kufanya vitu kwa kuzingatia unafuu wa shule Binafsi ambazo kwa kiwango kikubwa wanafunzi wake huishi boarding ingefaa kuongeza miezi ya masomo kwa kuondoa likizo ya mwezi December na kuipeleka mwezi march

Kubadili miezi ya mwaka wa masomo ni rahisi zaidi kuliko kuongeza masaa ya masomo maana mwanafunzi anaweza kujifunza kwa kipindi kirefu zaidi na kwa uhuru kuliko kumuongezea masaa ya masomo ikumbukwe sera ya Elimu imekuwa ikibadilika kila mara kutokana na uhitaji katika sekta hiyo kulingana na mitaala yetu zamani miaka 1990-2000 muda wa masomo ulikuwa mchache tofauti na sasa lakini wanafunzi walihitimu na Taifa likapata wasomi kuanzia miaka hii ya 2000-2020 kumekuwa na mabadiliko ya mala kwa mala katika sekta ya Elimu kuanzia mitaala na muda wa kujifunza jambo linalo pelekea usumbufu kwa watahiniwa..

Serikali ni muhimu kuwashirikisha wadau wa Elimu kabla ya kutoa waraka na miongozo juu ya Elimu nchini kwa maana wadau wa Elimu ndio wabia katika sekta nzima ya Elimu wizara kazi yake ni kusimamia mapendekezo na kuyaingiza katika mfumo wa kiutendaji kazi ya wizara ya Elimu sio kutoa miongozo ambayo kwa namna nyingine inaweza kuleta athari kubwa kwa wananchi.

#Naipenda_Tanzania
9fd2186481e87c66236095b631d0235e.jpg
 
Shukrani za dhati kwa wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa kulifanyia kazi jambo hili tena kwa wakati nina Imani sasa watoto wakitanzania watasoma kwa Amani na upendo
 
Back
Top Bottom